Muda wa ulimwengu na matukio yake tangu mwanzo wake

Muda wa ulimwengu na matukio yake tangu mwanzo wake

Monstgala

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2009
Posts
1,079
Reaction score
1,037
Nia ya mada hii ni kuuweka muda na matukio kwa ufupi sana kama wataalamu wanavyouona ili tujifunze na kutafakari kwa akili zetu tunapochanganya na ufahamu kutoka vyanzo tofauti. Binafsi huu si msimamo wangu bali uchunguzi katika vyanzo ambavyo vipo siku zote kwenye vitabu, machapisho, digital information sources, habari za kuambiwa au kusikia, kujifunza na kadhalika. Kama tulitokea kwa bahati basi tuione bahati hii kwa upana wake na kama tulikusudiwa tutokeaa basi tuone kusudio hilo lilivyo na nguvu za kipekee kwa kuangalia matukio yanayoelezewa na wataalam wa fani husika.

Pia katika kuupitia muda na matukio tunayoambiwa yalitokea na yatatokea, tunaweza kuona jinsi tulivyo muhimu au tusivyo muhimu katika muda huu mrefu wenye mambo makubwa yaliyotokea na yatakayotokea na hivyo kuufanya wakati huu kuwa wa kipekee sana.

Muda ni nini?

Ni swali zito na la zamani sana kabla sisi wote hatujazaliwa tayari wataalam wa fani mbali mbali wamejaribu kulijibu kwa upeo wa juu sana. Bado swali hili lipo tu kwa kuwa bado tunaendelea kujifunza jinsi ulimwegu ulivyo na unavyofanya kazi. Na hasa ukitaka kufafanua muda ni nini ugumu unakuja lakini kila mtu hata mtoto mdogo anauona muda kwa namna yake mwenyewe. Hivyo kila mtu kwa nafasi yake anaweza kuu-define muda kwa maana kila mtu anau-experience na analo jambo fulani linalomfanya auone muda kwa namna yake. Sitajikita katika kutafuta maana ya muda inayokubaliwa na wengi kwa kuwa kuna majibu mengi sana kutoka kwenye dhana tofauti na hiyo si mada hii ila nitajikita katika kuangalia matukio na tofauti ya muda wake kwa kuwa ndio yanatupa ule mstari wa kufikirika wa muda wenye past, present and future.

Kumbuka muda tumeamua wenyewe (binadamu) kuuweka katika vipimo (sekunde, dakika, mwaka etc) hivyo kuujengea kitu kama mstari ulionyooka katika fikra zetu. Kwamba mstari huu una uelekeo mmoja na sasa tuko katikati yake (tulipo) na yale yaliyopita yanajipanga upande mmoja wa tulikotoka na yajayo ambayo hatujayafikia yanajipanga katika upande mwingine wa mstari wa tunakoelekea.

Matukio yanayo/yatakayo na yaliyotokea yanatupa uelewa wa muda uliopita, wa sasa na ujao. Kitu cha kukumbuka na cha ajabu ni kwamba mstari huu wa muda (arrow of time) wala haupo katika zile sheria za msingi za physics na wala hauna muunganiko wowote na sheria hizi. Hivyo mstari huu wa muda ni katika ufahamu wetu na uwezo wa kuuona au kuufikiri kwa kuangalia matukio hivyo ni wa kufikirika au psychological arrow. Tusiuchanganye na thermodynamic arrow na cosmological arrow hizi zinasimama kama dhana tofauti na sio mada yetu kwa sasa.

Muda kwa kuangalia tangu kutokea kwa ulimwengu (universe)

NOTE. Kumbuka hapa baadhi ya maeneo theories, hypothesis na phenomena zenye ushawishi zinatumika. Wataalam wa theoretical phyisics, na Astrophicists wanashika hatamu hapa.

Umri wa sayari ya Dunia na Jua

Wataalam hawa wanatuambia umri wa jua na dunia umekaribiana wakiwa na maana kuna tofauti ya miaka milioni 60. Lakini muda huu si kidogo kwetu sisi binadamu ambao dakika zinatumika hata kwenye misemo ya kila siku. Kama unakumbuka ule wa "Nipe dakika mbili tu ntakua hapo"

Jua lilitokea katika wingu kubwa la gesi mbali mbali miaka bilioni 4.6 iliyopita (4.6 Ga). Baada ya hapo dunia ikatokea/tengenezwa kutoka kwenye mabaki ya milipuko ile ya gesi iliyokuwa iliyotengeneza jua. Baada ya hapa kikafuata kipindi kigumu sana ambacho dunia imewahi kupitia (Hadean Eon). Joto kali na lava katika uso wote wa dunia pamoja na milipuko mingi sana na kugongwa na mamilioni ya vimwondo, miale na mawe makubwa. Na hypothesis moja inasema katika kipindi hiki cha Hadean Eon ndipo mwezi ulipotokea baada ya dunia kugongwa na kitu kizito sana ambacho kinadhaniwa kuwa sayari ndogo au dwarf planet. Mkusanyiko wa mapande ya mawe, vumbi na madini yaliyosababishwa na mgongano huu wa dunia na aina fulani ya sayari ndogo ndio ulioutengeneza mwezi. Kumbuka ni process za muda mrefu sana hizi mamilioni ya miaka. Kipindi hiki cha Hadean Eon kinakadiriwa kuchukua takribani miaka bilioni moja(1 Billion) mpaka pale hali ya hewa ilipoanza kutulia taratibu na dunia kupoa.

Umri wa Ulimwengu (Universe)

Umri wa ulimwengu au universe unakadiriwa kutokana na ile theory ya Big Bang kuwa ni miaka bilioni 13.8 toka mlipuko huo mpaka sasa. Hivyo toka jua li-form kutoka kwenye mawingu fulani ya gesi na baadae dunia mpaka sasa.

Mwisho wa Jua

Na kama ulidhani muda unavyoenda mbele ndio mambo yanakuwa mazuri basi kaa vizuri uone muda ukiangaliwa huko mbeleni predictions za future zikoje. Baada ya miaka bilioni nane jua litapanuka mara 250 ya sasa na hivyo kumeza dunia na sayari zote. Lakini kabla ya hapo ndani ya miaka milioni mia nane (800yrs) kiwango cha carbondioxide kitashuka chini kabisa na kuisha na hii ina maana hakutakuwa na photosythesis na hivyo kukosekana kwa oygen ambayo ndio chanzo muhimu cha uhai. Baada ya miaka bilioni moja miale ya jua itakuwa mikali sana na kufanya maji yote katika dunia ya-evaporate na kupotelea anga za mbali.

Kabla ya universe

Wataalam wanatuambia hata muda ulizaliwa hapo hivyo kabla ya Big bang hakukuwa na muda. Mvurugano na mraruano uliopo ni kwamba hakuna theory yoyote nzuri inayoendana na uwezo wa akili ya mwanadamu kwa hili. Lakini si kwamba hazipo theory zinazojaribu kueleza nini hii kitu inayoitwa "kabla ya Big Bang".

Albert Eisten katika "theory of relativity" yeye anafafanua wazi jinsi muda ulivyozaliwa na kabla ya hapo muda ulikuwa umesimama au kwa lugha nyingine hauendi mbele wala nyuma. Na katika kipindi hiki ulimwengu mzima (universe) ulikuwa kitu kimoja kidogo sana zaidi ya sub-atomic particle yani huwezi kukiona hata kwa microscope.

Inflation theory inasuggest kuwepo kwa universe nyingine iliosababisha hii tuliyomo wakati ile ya multiverse au chaotic inflationary ikipendekeza kuwepo kwa universes nyingi kama bubbles zisizohesabika na hii ya kwetu ni mojawapo. Kuna ile ya "Extra dimensional membranes" (branes), White holes, Our universe being inside a big black hole na models nyinginezo katika kujaribu kutafuta jibu lenye ushawishi.

Wakati ujao wa ulimwengu (universe)

Baada ya jua kulipuka na kutoweka ama kuwa kitu kingine tofauti muda unaoendelea mbele ni wa kutisha na kusikitisha sana. Hapa sasa tunauangalia muda kwa kipindi kirefu sana kiasi kwamba namba zinazotumika kwa makadirio ili tuuone mwisho wa universe ni trillions za miaka (T).

Baada ya muda wa kati ya miaka trilioni moja na trillioni mia (1-100T) nyota zitaacha kuumbika au ku-form katika pande zote za ulimwengu mzima. Kumbuka nyota zinakufa na kuzaliwa kila siku kwa sasa. Baada ya kati ya miaka trilioni 110 na 120 (110-120T), nyota ya mwisho kabisa kuwepo inaishiwa nishati yake na kuzima/kufa. Baada ya miaka 10^10 [SUP]76 [/SUP], matter katika ulimwengu au universe sasa imeliwa yote na black holes na ndiyo yamebakia yakiranda-randa na kumezana/kuungana.

Baada ya miaka 10^10[SUP]120[/SUP] nishati yote katika ulimwengu(universe) imeisha hivyo hamna chochote kinachofanyika tena popote pale na inaitwa "Heat Death" wala haieleweki vizuri au mimi siielewi vizuri lakini ni model mojawapo yenye ushawishi kwa sasa.

Hitimisho:

Kutokana na information hizi za hawa wataalam, binadamu wa kawaida mwenye lugha na utamaduni (modern human) amekuwepo miaka 62,014 tu katika ulimwengu wenye miaka bilioni 13.8. Hii ni asilimia 0.000449% tu ya muda wote tangu kuanza kwa universe.

Na wataalam hawa wanamaanisha kwa lugha nyepesi - katika muda huu mrefu na matukio yake chini ya sheria za kifizikia zilizojiweka zenyewe au zilizowekwa umefanya baadhi ya zile gas zijiangalie, zijitambue na kuanza kuulizana na kubishana zilitoka wapi na muda uendavyo mbele(kama unaenda mbele) imagine gas hizi zitafanya nini?

Karibuni tujadili, kuongeza, kutoa opinion zetu na hata kujaribu kuelewa kwa urahisi nini watu wengine wanafikiri.
 
Mkuu,

Hii ni mada nzuri sana.Time has always been a mystery. Some say it is an illusion others say its part and parcel of fabric of the universe

Madaa yako imesema muda ni kama number line imenyooka.Kuna wataalam wengine waliseme muda ni duara yani unazunguka in a continous loop

Unaweza kurudi nyuma au kwenda mbele. Muda umeunga na space kutengeneza space-time continuum

Kwamba muda ni a space dimension kama length,width and height.Muda una facilitate motion.Huwez kusogea in zero second

Daah complex stuff.Endelea kutoa mambo mkuu
 
Mkuu, Asante kwa kuongeza dhana nyingine za muda. Huu mstari au arrow of time ni kwa jinsi sisi binadamu tunavyouona muda na hii ni kwa sababu ubongo wetu umekuwa fashioned that way. Lakini ukianza kuangalia logical reality ya muda basi unakutana na nadharia tofauti. Mimi nimejaribu kubase kwenye arrow of time ili kuelezea baadhi ya matukio tuliyoyashudia na tunayoambiwa yalitokea na yatatokea.
 
Aksante mkuu, hii topic mpk usome mara mbili kuielewa,hata hivyo siku nyingi conceptualise dunia,muda na Mungu..ili nijiridhishe kuwa mungu ni imani isiyo na mashiko kuamini, km muda ni évolution basi tunaitaj ufahamu zaidi.
 
its a shame how post like this doesn't get as many like as it deserve!!! au ndo kama kawaida zetu watanzania na zile data za IQ?????? hawakawii wanadini wakaja kuchafua hewa hapa na uzushi wao usio na mbele wala nyuma much less any proof!!!
 
hapa ndo unaona uwezo wa mwanadam na umuhimu wa kutunza kumbukumbu,

haya maneno yameelezwa vizuri saana na kama mtu ana muda angalia kuna documentary yake inaitwa cosmos a space time odyssey unaweza download na kujielimisha za kufungua ufaham na kuona maelezo yote na ushahidi pia

hizo black matter au black holes zimeelezewa vizuri na pengine inaaminika ndo inashikilia universe/ulimwengu
https://www.youtube.com/watch?v=kI2htibwWH4 iyo hapo ni trail yake you tube na unaweza download kutumia torrent kawaida

kama hivi vitu tunavyofanya tunatumia 10% mpaka 15% ya uwezo wa ubongo wetu itakuwaje siku hata tufike 50% ya uwezo wake!!!.

knowledge is power!
 
Dah! ........

Mkuu asante kwa mada murua sana

Nimejifunza mengi na nitajifunza mengi

Nilichokiona hapo ni nkuwa muda,kwa namna tunavyouona sisi sio kitu halisi bali ni dhana tuliyoijenga sisi na huenda iko tofauti sana

Ngoja nije nirudie kuisoma ......

Mkuu asante sana na Mungu akubariki sana .......!!
 
Nimesoma Vitu vingi hapo na nilikua sivifahamu kabisa,lakini kwa akili yetu sisi binadamu wa kawaida kabisa sehemu pekee unaweza kupata habari yenye angalau kueleweka na kupata maana ya jinsi ya ulimwengu huu ni kwenye biblia,matukio mengi ya kwenye biblia yamethibitishwa na wanasayansi na wanahistoria wa kale kabisa kuwa ni kweli,lakini kufomulate kitu kuwa seli yetu kati yangu mimi na mboga aina ya mchicha ni moja siwezi kukubali lazima kuwe na facts za kutosha kuiback up hiyo hoja ........
 
kwanini huwezi kukubali?
 
Aksante mkuu, hii topic mpk usome mara mbili kuielewa,hata hivyo siku nyingi conceptualise dunia,muda na Mungu..ili nijiridhishe kuwa mungu ni imani isiyo na mashiko kuamini, km muda ni évolution basi tunaitaj ufahamu zaidi.

Mkuu, evolution kwa maana ya mabadiliko kibailogia ya kitabia na kimaumbile yanayorithiwa na vizazi na vizazi vya viumbe hai, ina nafasi fupi sana katika theory nzima ya muda na matukio yake. Evolution peke yake ina ukomo na hivyo haiwezi mbadala wa maana ya muda au hata "the arrow of time" kama ulivyoiweka bali kipande kidogo cha theory kinachojaribu kuelezea mabadiliko ya kitabia na kimaumbile ya viumbe na pia sio kama chanzo cha uhai.

Kama unavyoona katika "arrow of time", uhai ni kipindi kifupi tu ukilinganisha na matukio mengine yaliyo katika theory hizi.
 
Arguments za science kutaka kujuwa uhai na maumbile ya mbingu na nchi zimebase kabisa kwenye kile biblia inasema.
mfano: Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Scientists katika kutaka kupima mwanzo Ni lini wanasema 13 billion years ago.
Biblia pia inasema, baada ya mbingu na nchi kuumbwa...mungu alifanya kazi ya kuumba na kutengeneza maumbile tofauti tofauti ya nchi na mbingu kwa siku sita mfano Jua, mwezi,nyota, maji na ardhi, na katika viumbe vyote venye uhai vilivyoumbwa na Mungu mfano mimea, samaki na wanyama wa mwitu, binadamu alikuwa kiumbe wa mwisho kuumbwa!! Science inasema binadamu katika time kimekuwa kiumbe cha mwisho ku-evolve about 6 million years ago na modern man is about 60,000 years old toka awepo kwenye sura ya Dunia na makeke yote.
Tuendelee kujifunza.
 
Nimeipenda hii mada....ukizingatia ya kuwa ina lenga hasa kutanua uwezo wa kufikiri.....kwa kutumia nadharia.
Lakini napata mashaka sana na nadharia zinazo jaribu kujitutumua kutrace origin ya universe(hii nikijaribu kutafakari ni vipi wameweza kutrace bilions of years way back???) and how sure they are kwamba wako correct.
Mi binafi yangu naona most of scientific theories a more utopian rather than logical,factual and proveable(mfano hili la evolution-binadamu kutoka sokwe!!?

Anyway,theories ndizo pia zinatupa muda wa kuchambua na kutafakari mambo.Big up kwako mleta mada!
 
Vipimo vya ages za vitu mfano fossils kwa wanyama na rocks ili kujua age of the Earth etc., kilicho na uhakika au kinachokubalika ni Radiometric dating. Hii kwa lugha nyepesi ni kupima the time of the decaying unstable atoms on the elements which make these stuffs. Vipimo vingine vya kizamani vilishaachwa ingawa kwa wakati huo viliaminika mpaka pale ilipokuja kugundulika knowledge kubwa zaidi na kuonesha haviko sahihi. Mfano Rock erosion iliyopendekezwa na Charles Darwin katika kupima age of the Earth ilikuja kuonekana si kipimo sahihi.
 
Nimesoma concept of time katika kozi ya AFRICAN PHILOSOPHY pale UDSM, course instructor akiwa DR. Adolf Mihanjo. Niliamini kwamba ninauelewa mkubwa kuhusu concept of time but I admit i understand nothing. Mkuu endelea kutupa shule.Pia usisahau uliahidi kama sijakosea kutuletea uzi kuhusu "Rosswell ufo Incidence."
 
Mkuu, Thanks. Muda ni mada pana sana, nimechukua approach ya upande mmoja ili tupate pa kuanzia. Nita-share pia kidogo ninachojua kuhusu issue ya possible intelligent civillizations nikipata wasaa lakini katika mada tofauti.
 
I fell in love with this one
Maada tamu saaana
GOD BLESS YOU HOMIE

.made in mby city.
 
I fell in love with this one
Maada tamu saaana
GOD BLESS YOU HOMIE

.made in mby city.

Hahah! great. It is something to think and express our views since everybody experience the time flow and its directionality.
 
Dah! ........

Mkuu asante kwa mada murua sana

Nimejifunza mengi na nitajifunza mengi

Nilichokiona hapo ni nkuwa muda,kwa namna tunavyouona sisi sio kitu halisi bali ni dhana tuliyoijenga sisi na huenda iko tofauti sana

Ngoja nije nirudie kuisoma ......

Mkuu asante sana na Mungu akubariki sana .......!!

Sure Mkuu, jinsi ubongo wa mwanadamu unazaliwa na aina mpangilio wa kuuona muda kwa namna tunayouona na tunavyokua na kuanza ku-perceive things around us mfano, usiku na mchana, sunrise na sunset na matendo mengine mengi yanaushape ubongo kuuona muda kwa namna ya pekee ambayo kama binadamu itakuwa na faida kwake. Mtu akiwa conscious anakuwa na specific experience of time na hii ni kwa kuwa ubongo unafanya kazi kwa kusaidiana na information nyingi zinazoletwa na milango ya fahamu kuhusu matendo na matukio at the moment na kumbukumbu zilizotunzwa. Katika sub-concious state experience ya muda inakuwa tofauti kwa kiwango fulani.

Kwa mfano ndoto anayoota mtu kwa dakika 10 hadi 15 inaweza kuwa na details nyingi ambazo kwa kawaida ndani ya dakika 15 ukiwa conscious huwezi kuzipanga au haziwezi ku-fit kikawaida. Kwa hiyo perception zetu ambazo ziko biased zinatufanya tuuone muda kwa jinsi tofauti lakini yenye maana kwetu. Mfano ubongo una-skip milliseconds za muda na kuziunga kana kwamba millisecond moja haina tofauti na millisecond 10. Binadamu akiishi mazingira tofauti yasiyo na muda tunaoupima kwa saa na vitu vingine anaweza kuwa na experience tofauti kidogo ya muda ulivyo.
 
Kwahiyo mkuu,muda ni kitu halisi au sio halisi?

Au ni kitu halisi lakini sisi tunakiona tofauti?

Au ni kitu halisi lakini ni kwa hapa kwetu duniani tu lakini pia kipo mahali pengine na huko pengine kipo tofauti na hapa kwetu?
 
Back
Top Bottom