Mkuu kadoda, karibu nawe uchangie kidogo katika mjadala huu.
Niliwahi kuweka uzi kuhusu mwanzo wa universe katika Quran lakin watu wakaanza ubishi na kukejeli hivyo niliacha kuwajibu..ieleweke kua niliweka hivyo kwa lengo la kuongea kitu ambacho kipo na hakukua na haja ya kubisha...Uzi ulikua unasoma kama hivi "ni kweli big bang imezungumziwa katika Quran?" ..kama mtaridhika na mtakua tayari kuelimishana bila kejeli au kwenda nje ya mada basi ntachangia kuhusu mwanzo wa ulimwengu,muda uliopo katika ulimwengu na ujao pia....samahani sana tusiwe na udini bila sababu...nasuburu ruhusa yenu wakuu na makubaliano ya kaelimishana bila kejeli. Natanguliza shukrani
Mkuu, Thanks. Muda ni mada pana sana, nimechukua approach ya upande mmoja ili tupate pa kuanzia. Nita-share pia kidogo ninachojua kuhusu issue ya possible intelligent civillizations nikipata wasaa lakini katika mada tofauti.
Niliwahi kuweka uzi kuhusu mwanzo wa universe katika Quran lakin watu wakaanza ubishi na kukejeli hivyo niliacha kuwajibu..ieleweke kua niliweka hivyo kwa lengo la kuongea kitu ambacho kipo na hakukua na haja ya kubisha...Uzi ulikua unasoma kama hivi "ni kweli big bang imezungumziwa katika Quran?" ..kama mtaridhika na mtakua tayari kuelimishana bila kejeli au kwenda nje ya mada basi ntachangia kuhusu mwanzo wa ulimwengu,muda uliopo katika ulimwengu na ujao pia....samahani sana tusiwe na udini bila sababu...nasuburu ruhusa yenu wakuu na makubaliano ya kaelimishana bila kejeli. Natanguliza shukrani
Mkuu MONSTGALA a.k.a MGALANJUKA nina hamu na hiyo ki2 ya "POSSIBLE INTELLIGENT CIVILIZATIONS" au "ROSSWELL UFO INCIDENT"
Tangu nimeanza kukusoma kwenye post kadhaa nikaona ndugu yetu una mengi ya kutufunza tunao hitaji ku stretch brain zaidi
Karibu MONSTGALA/MGALANJUKA kutiririka maelimu ya msingi
.made in mby city.
Asante mkuu , hiyo inakuja muda si mrefu. Niliona ni vyema kuongelea mambo mengine ya msingi kwanza ili tukienda huko kwenye mkanganyiko tuwe na urahisi wa kueleweshana.
HII KITU NI MUHIMU SANA MTU KUJIFUNZA ILA NI LAZIMA UIACHILIE AKILI YAKO YOTE IFIKIRI NA UKIACHIA AKILI IFIKIRI VIZURI BASI SI RAHISI SANA KUKWEPA KUHUSISHA NA IMANI ZETU...mimi naamini katika mungu na pia mungu mwenyewe vingine ndiye ajuaye(hivi tunavyosema bil years ago)kwa kuwa hii ni thiory poaNia ya mada hii ni kuuweka muda na matukio kwa ufupi sana kama wataalamu wanavyouona ili tujifunze na kutafakari kwa akili zetu tunapochanganya na ufahamu kutoka vyanzo tofauti. Binafsi huu si msimamo wangu bali uchunguzi katika vyanzo ambavyo vipo siku zote kwenye vitabu, machapisho, digital information sources, habari za kuambiwa au kusikia, kujifunza na kadhalika. Kama tulitokea kwa bahati basi tuione bahati hii kwa upana wake na kama tulikusudiwa tutokeaa basi tuone kusudio hilo lilivyo na nguvu za kipekee kwa kuangalia matukio yanayoelezewa na wataalam wa fani husika.
Pia katika kuupitia muda na matukio tunayoambiwa yalitokea na yatatokea, tunaweza kuona jinsi tulivyo muhimu au tusivyo muhimu katika muda huu mrefu wenye mambo makubwa yaliyotokea na yatakayotokea na hivyo kuufanya wakati huu kuwa wa kipekee sana.
Muda ni nini?
Ni swali zito na la zamani sana kabla sisi wote hatujazaliwa tayari wataalam wa fani mbali mbali wamejaribu kulijibu kwa upeo wa juu sana. Bado swali hili lipo tu kwa kuwa bado tunaendelea kujifunza jinsi ulimwegu ulivyo na unavyofanya kazi. Na hasa ukitaka kufafanua muda ni nini ugumu unakuja lakini kila mtu hata mtoto mdogo anauona muda kwa namna yake mwenyewe. Hivyo kila mtu kwa nafasi yake anaweza kuu-define muda kwa maana kila mtu anau-experience na analo jambo fulani linalomfanya auone muda kwa namna yake. Sitajikita katika kutafuta maana ya muda inayokubaliwa na wengi kwa kuwa kuna majibu mengi sana kutoka kwenye dhana tofauti na hiyo si mada hii ila nitajikita katika kuangalia matukio na tofauti ya muda wake kwa kuwa ndio yanatupa ule mstari wa kufikirika wa muda wenye past, present and future.
Kumbuka muda tumeamua wenyewe (binadamu) kuuweka katika vipimo (sekunde, dakika, mwaka etc) hivyo kuujengea kitu kama mstari ulionyooka katika fikra zetu. Kwamba mstari huu una uelekeo mmoja na sasa tuko katikati yake (tulipo) na yale yaliyopita yanajipanga upande mmoja wa tulikotoka na yajayo ambayo hatujayafikia yanajipanga katika upande mwingine wa mstari wa tunakoelekea.
Matukio yanayo/yatakayo na yaliyotokea yanatupa uelewa wa muda uliopita, wa sasa na ujao. Kitu cha kukumbuka na cha ajabu ni kwamba mstari huu wa muda (arrow of time) wala haupo katika zile sheria za msingi za physics na wala hauna muunganiko wowote na sheria hizi. Hivyo mstari huu wa muda ni katika ufahamu wetu na uwezo wa kuuona au kuufikiri kwa kuangalia matukio hivyo ni wa kufikirika au psychological arrow. Tusiuchanganye na thermodynamic arrow na cosmological arrow hizi zinasimama kama dhana tofauti na sio mada yetu kwa sasa.
Muda kwa kuangalia tangu kutokea kwa ulimwengu (universe)
NOTE. Kumbuka hapa baadhi ya maeneo theories, hypothesis na phenomena zenye ushawishi zinatumika. Wataalam wa theoretical phyisics, na Astrophicists wanashika hatamu hapa.
Umri wa sayari ya Dunia na Jua
Wataalam hawa wanatuambia umri wa jua na dunia umekaribiana wakiwa na maana kuna tofauti ya miaka milioni 60. Lakini muda huu si kidogo kwetu sisi binadamu ambao dakika zinatumika hata kwenye misemo ya kila siku. Kama unakumbuka ule wa Nipe dakika mbili tu ntakua hapo
Jua lilitokea katika wingu kubwa la gesi mbali mbali miaka bilioni 4.6 iliyopita (4.6 Ga). Baada ya hapo dunia ikatokea/tengenezwa kutoka kwenye mabaki ya milipuko ile ya gesi iliyokuwa iliyotengeneza jua. Baada ya hapa kikafuata kipindi kigumu sana ambacho dunia imewahi kupitia (Hadean Eon). Joto kali na lava katika uso wote wa dunia pamoja na milipuko mingi sana na kugongwa na mamilioni ya vimwondo, miale na mawe makubwa. Na hypothesis moja inasema katika kipindi hiki cha Hadean Eon ndipo mwezi ulipotokea baada ya dunia kugongwa na kitu kizito sana ambacho kinadhaniwa kuwa sayari ndogo au dwarf planet. Mkusanyiko wa mapande ya mawe, vumbi na madini yaliyosababishwa na mgongano huu wa dunia na aina fulani ya sayari ndogo ndio ulioutengeneza mwezi. Kumbuka ni process za
Na wataalam hawa wanamaanisha kwa lugha nyepesi - katika muda huu mrefu na matukio yake chini ya sheria za kifizikia zilizojiweka zenyewe au zilizowekwa umefanya baadhi ya zile gas zijiangalie, zijitambue na kuanza kuulizana na kubishana zilitoka wapi na muda uendavyo mbele(kama unaenda mbele) imagine gas hizi zitafanya nini?
Karibuni tujadili, kuongeza, kutoa opinion zetu na hata kujaribu kuelewa kwa urahisi nini watu wengine wanafikiri.
Shukrani sana mkuu kwa ushirikiano wako kwenye hii elimu adimu sana
nina maswali ya kukuuliza kule kwenye uzi wa "ALIENS AND UFO, JE TUKO PEKE YETU?" nitahitaji ushirikiano wako mkuu
.made in mby city.
Asante mkuu , hiyo inakuja muda si mrefu. Niliona ni vyema kuongelea mambo mengine ya msingi kwanza ili tukienda huko kwenye mkanganyiko tuwe na urahisi wa kueleweshana.
Dah! ........
Mkuu asante kwa mada murua sana
Nimejifunza mengi na nitajifunza mengi
Nilichokiona hapo ni nkuwa muda,kwa namna tunavyouona sisi sio kitu halisi bali ni dhana tuliyoijenga sisi na huenda iko tofauti sana
Ngoja nije nirudie kuisoma ......
Mkuu asante sana na Mungu akubariki sana .......!!
Mkuu monstgala.. marekani huwa kwa kipindi flani wanasogeza saa mbele au wanarudisha nyuma. Hii kitu mpaka naondoka huko sikupata jibu muafaka. Please nidadavulie hapa pls..
Mkuu Bouncer nadhani utakuwa unamaanisha ule mfumo wa DST uliopitishwa au unaofanywa katika nchi nyingi zenye majira ya baridi (winter) na (joto) hasa Ulaya na Marekani. Hawa watu wana majira ya baridi na joto na kwa kuwa winter inakuwa na usiku mrefu zaidi ya mchana au giza linakuwepo masaa mengi zaidi ya mwanga, na summer inakuwa na mchana mrefu kuliko usiku basi wakaona ni vyema kusogeza mbele saa (mara nyingi one hour) wakati wa kabla ya summer ili watu waamke mapema zaidi na kupata muda zaidi wa kuwa katika mchana na baadae kurudisha nyuma saa moja mara baada ya summer kuisha pale winter inapoanza kuingia.
Wenzetu hawa kwa kuwa wanafuata sana saa/muda na wamezoea hali hii hii sio shida sana kwao na huenda sawa na mabadiliko haya ila kwa wageni huwa ni kitu cha ajabu kidogo. Kinachofanyika ni utaratibu wa nchi kuamua kufuata mfumo huu na si lazima nchi yoyote yenye majira haya ifuate au kufanya mabadiliko ya muda katika winter na summer. Niliwahi kutembelea arctic circle huko Nordland Norway na katikati kabisa ya majira ya joto, jua halikuzama hivyo kulikuwa na siku nzima isiyokuwa na usiku. Hii ilikuwa ajabu kwangu na kitu fulani cha kukumbuka. Niliambiwa vivyo hivyo wakati wa katikati ya winter mchana ni mfupi sana waweza kuwa masaa machache tu.[/QUOTE^]
Thanks mkuu monstgala... Now kwa maana nyingine haya mambo ya saa kama waliowahi wangeamua siku nzima iwe masaa 12 yaan mchana 6 na usiku 6 basi ingekuwa hivyo right?
Kuna kitu sijaelewa hapo juu.. umesema our universy imeanza 4 billion yrs ago while our galaxy milkyway imeanza 13 bilion yrs ago na galaxy ilianza kwa big bang.. na universy yetu ya sun nayo ilianza kwa big bang.. now does it mean it was a big bang inside a galaxy?

Sawa mkuu.. ile niliipitia sema utofauti wa galaxy na universy ndio ulikuwa haujakaa mahala pake kichwani kwangu.Hapana. Katika hili naomba unisome vizuri. Katika Universe kuna trillions of galaxies kwa hiyo haiwezi kuwa kinyume kama ulivyokuote. Galaxi yetu ni moja kati ya nyingi sana zilizo ndani ya universe. 4.5 billion years utakuwa umri wa Jua (sun) ambalo ni moja ya nyota nyingi sana katika galaxi tuliyomo (milkyway). Kuna thread moja hapa jukwaani ya Mambo ya kustaajabisha ya nyota naomba uipitie ina maelezo mazuri sana kuhusu hiyo kitu.
Mkuu NICOLAX , Ule uzi sikuanzisha mimi ila nilichangia kidogo tu. Mada ile ina maudhui ya jumla sana ambayo yanahusisha vitu vingine ambavyo si vya uhakika mfano; madai ya kuona UFO hapa duniani au kukutana na alien creatures kwenye shamba fulani. Part niliyochangia mimi ni ile ya Possible Intelligent beings with advanced civilization ambayo kimaudhui ni pana zaidi na yenye grounds za kueleweka vizuri. Nitaweka uzi wenye hii kitu soon ili tudiscuss zaidi.
Nia ya mada hii ni kuuweka muda na matukio kwa ufupi sana kama wataalamu wanavyouona ili tujifunze na kutafakari kwa akili zetu tunapochanganya na ufahamu kutoka vyanzo tofauti. Binafsi huu si msimamo wangu bali uchunguzi katika vyanzo ambavyo vipo siku zote kwenye vitabu, machapisho, digital information sources, habari za kuambiwa au kusikia, kujifunza na kadhalika. Kama tulitokea kwa bahati basi tuione bahati hii kwa upana wake na kama tulikusudiwa tutokeaa basi tuone kusudio hilo lilivyo na nguvu za kipekee kwa kuangalia matukio yanayoelezewa na wataalam wa fani husika.
Pia katika kuupitia muda na matukio tunayoambiwa yalitokea na yatatokea, tunaweza kuona jinsi tulivyo muhimu au tusivyo muhimu katika muda huu mrefu wenye mambo makubwa yaliyotokea na yatakayotokea na hivyo kuufanya wakati huu kuwa wa kipekee sana.
Muda ni nini?
Ni swali zito na la zamani sana kabla sisi wote hatujazaliwa tayari wataalam wa fani mbali mbali wamejaribu kulijibu kwa upeo wa juu sana. Bado swali hili lipo tu kwa kuwa bado tunaendelea kujifunza jinsi ulimwegu ulivyo na unavyofanya kazi. Na hasa ukitaka kufafanua muda ni nini ugumu unakuja lakini kila mtu hata mtoto mdogo anauona muda kwa namna yake mwenyewe. Hivyo kila mtu kwa nafasi yake anaweza kuu-define muda kwa maana kila mtu anau-experience na analo jambo fulani linalomfanya auone muda kwa namna yake. Sitajikita katika kutafuta maana ya muda inayokubaliwa na wengi kwa kuwa kuna majibu mengi sana kutoka kwenye dhana tofauti na hiyo si mada hii ila nitajikita katika kuangalia matukio na tofauti ya muda wake kwa kuwa ndio yanatupa ule mstari wa kufikirika wa muda wenye past, present and future.
Kumbuka muda tumeamua wenyewe (binadamu) kuuweka katika vipimo (sekunde, dakika, mwaka etc) hivyo kuujengea kitu kama mstari ulionyooka katika fikra zetu. Kwamba mstari huu una uelekeo mmoja na sasa tuko katikati yake (tulipo) na yale yaliyopita yanajipanga upande mmoja wa tulikotoka na yajayo ambayo hatujayafikia yanajipanga katika upande mwingine wa mstari wa tunakoelekea.
Matukio yanayo/yatakayo na yaliyotokea yanatupa uelewa wa muda uliopita, wa sasa na ujao. Kitu cha kukumbuka na cha ajabu ni kwamba mstari huu wa muda (arrow of time) wala haupo katika zile sheria za msingi za physics na wala hauna muunganiko wowote na sheria hizi. Hivyo mstari huu wa muda ni katika ufahamu wetu na uwezo wa kuuona au kuufikiri kwa kuangalia matukio hivyo ni wa kufikirika au psychological arrow. Tusiuchanganye na thermodynamic arrow na cosmological arrow hizi zinasimama kama dhana tofauti na sio mada yetu kwa sasa.
Muda kwa kuangalia tangu kutokea kwa ulimwengu (universe)
NOTE. Kumbuka hapa baadhi ya maeneo theories, hypothesis na phenomena zenye ushawishi zinatumika. Wataalam wa theoretical phyisics, na Astrophicists wanashika hatamu hapa.
Umri wa sayari ya Dunia na Jua
Wataalam hawa wanatuambia umri wa jua na dunia umekaribiana wakiwa na maana kuna tofauti ya miaka milioni 60. Lakini muda huu si kidogo kwetu sisi binadamu ambao dakika zinatumika hata kwenye misemo ya kila siku. Kama unakumbuka ule wa Nipe dakika mbili tu ntakua hapo
Jua lilitokea katika wingu kubwa la gesi mbali mbali miaka bilioni 4.6 iliyopita (4.6 Ga). Baada ya hapo dunia ikatokea/tengenezwa kutoka kwenye mabaki ya milipuko ile ya gesi iliyokuwa iliyotengeneza jua. Baada ya hapa kikafuata kipindi kigumu sana ambacho dunia imewahi kupitia (Hadean Eon). Joto kali na lava katika uso wote wa dunia pamoja na milipuko mingi sana na kugongwa na mamilioni ya vimwondo, miale na mawe makubwa. Na hypothesis moja inasema katika kipindi hiki cha Hadean Eon ndipo mwezi ulipotokea baada ya dunia kugongwa na kitu kizito sana ambacho kinadhaniwa kuwa sayari ndogo au dwarf planet. Mkusanyiko wa mapande ya mawe, vumbi na madini yaliyosababishwa na mgongano huu wa dunia na aina fulani ya sayari ndogo ndio ulioutengeneza mwezi. Kumbuka ni process za muda mrefu sana hizi mamilioni ya miaka. Kipindi hiki cha Hadean Eon kinakadiriwa kuchukua takribani miaka bilioni moja(1 Billion) mpaka pale hali ya hewa ilipoanza kutulia taratibu na dunia kupoa.
Umri wa Ulimwengu (Universe)
Umri wa ulimwengu au universe unakadiriwa kutokana na ile theory ya Big Bang kuwa ni miaka bilioni 13.8 toka mlipuko huo mpaka sasa. Hivyo toka jua li-form kutoka kwenye mawingu fulani ya gesi na baadae dunia mpaka sasa.
Mwisho wa Jua
Na kama ulidhani muda unavyoenda mbele ndio mambo yanakuwa mazuri basi kaa vizuri uone muda ukiangaliwa huko mbeleni predictions za future zikoje. Baada ya miaka bilioni nane jua litapanuka mara 250 ya sasa na hivyo kumeza dunia na sayari zote. Lakini kabla ya hapo ndani ya miaka milioni mia nane (800yrs) kiwango cha carbondioxide kitashuka chini kabisa na kuisha na hii ina maana hakutakuwa na photosythesis na hivyo kukosekana kwa oygen ambayo ndio chanzo muhimu cha uhai. Baada ya miaka bilioni moja miale ya jua itakuwa mikali sana na kufanya maji yote katika dunia ya-evaporate na kupotelea anga za mbali.
Kabla ya universe
Wataalam wanatuambia hata muda ulizaliwa hapo hivyo kabla ya Big bang hakukuwa na muda. Mvurugano na mraruano uliopo ni kwamba hakuna theory yoyote nzuri inayoendana na uwezo wa akili ya mwanadamu kwa hili. Lakini si kwamba hazipo theory zinazojaribu kueleza nini hii kitu inayoitwa "kabla ya Big Bang".
Albert Eisten katika theory of relativity yeye anafafanua wazi jinsi muda ulivyozaliwa na kabla ya hapo muda ulikuwa umesimama au kwa lugha nyingine hauendi mbele wala nyuma. Na katika kipindi hiki ulimwengu mzima (universe) ulikuwa kitu kimoja kidogo sana zaidi ya sub-atomic particle yani huwezi kukiona hata kwa microscope.
Inflation theory inasuggest kuwepo kwa universe nyingine iliosababisha hii tuliyomo wakati ile ya multiverse au chaotic inflationary ikipendekeza kuwepo kwa universes nyingi kama bubbles zisizohesabika na hii ya kwetu ni mojawapo. Kuna ile ya Extra dimensional membranes (branes), White holes, Our universe being inside a big black hole na models nyinginezo katika kujaribu kutafuta jibu lenye ushawishi.
Wakati ujao wa ulimwengu (universe)
Baada ya jua kulipuka na kutoweka ama kuwa kitu kingine tofauti muda unaoendelea mbele ni wa kutisha na kusikitisha sana. Hapa sasa tunauangalia muda kwa kipindi kirefu sana kiasi kwamba namba zinazotumika kwa makadirio ili tuuone mwisho wa universe ni trillions za miaka (T).
Baada ya muda wa kati ya miaka trilioni moja na trillioni mia (1-100T) nyota zitaacha kuumbika au ku-form katika pande zote za ulimwengu mzima. Kumbuka nyota zinakufa na kuzaliwa kila siku kwa sasa. Baada ya kati ya miaka trilioni 110 na 120 (110-120T), nyota ya mwisho kabisa kuwepo inaishiwa nishati yake na kuzima/kufa. Baada ya miaka 10^10 [SUP]76 [/SUP], matter katika ulimwengu au universe sasa imeliwa yote na black holes na ndiyo yamebakia yakiranda-randa na kumezana/kuungana.
Baada ya miaka 10^10[SUP]120[/SUP] nishati yote katika ulimwengu(universe) imeisha hivyo hamna chochote kinachofanyika tena popote pale na inaitwa Heat Death wala haieleweki vizuri au mimi siielewi vizuri lakini ni model mojawapo yenye ushawishi kwa sasa.
Hitimisho:
Kutokana na information hizi za hawa wataalam, binadamu wa kawaida mwenye lugha na utamaduni (modern human) amekuwepo miaka 62,014 tu katika ulimwengu wenye miaka bilioni 13.8. Hii ni asilimia 0.000449% tu ya muda wote tangu kuanza kwa universe.