Muda ni kitu gani?

Muda ni kitu gani?

Babu mjukuu wako nipo vizuri kicwani ukiachana na zile mada zangu zingine🤪

🤔🤔

Subiri kwanza nitarudi acha nifikilie hili swali fupi ila jibu lake linataka utulivu

Karibu babu England 1 wengine 0 😀😀
Ndio maana nakupenda mjukuu, sema tu hujui!
 
Muda ni nini hasa?🤔

Kwa wengi wetu, muda ni kipimo kinachotuonyesha sasa ni saa ngapi, ni asubuhi, mchana au usiku

Tunautambua kwa kuangalia saa, simu au hata mwendo wa jua

Lakini je, muda ni saa tu?
Mara nyingi tunasikia maneno kama

Tumia muda wako vizuri

Usichezee muda wako

Muda ni mali

Muda ukipita haurudi tena

Muda utasema

Hapo ndipo ninapojiuliza, muda ni nini hasa?

Je, ni sekunde, dakika na saa zinazopita?

Au ni nafasi tunayopewa kuishi, kupenda, kujifunza na kutimiza ndoto zetu?

Umewahi kunyimwa muda na mtu uliyekuwa unamhitaji?

Mimi niliwahi kumpenda mtu
Na nilivyo nikipenda mtu hua ni huyo huyo siwezani na stress za wapenzi wengi so hua nategemea vingi kutoka kwake kwa sababu nakua sina sehemu nyingine ya kuvipata

Kila nilipomuonesha nime m miss ghafla nilipokea SmS
Imethibitishwa umepokea kiasi fulani kutoka kwa fulani
Kisha ananiambia S, kanunue wine unywe

Kitu ambacho si kibaya ila sikua naitaji pesa yake tu nilimtaka yeye pia
Sasa sielewi labda nilikua nazidisha sana kumuitaji mpaka akachoka au la🤔

Nilifurahi kwa sababu alikuwa ananijali kwa namna yake

Lakini ukweli ni kwamba sikuwa nahitaji pesa pekee
Nilikuwa mpweke.

Nilitamani anipe muda wake

Kila nikisema Babe, I miss you
Badala ya mazungumzo marefu au muda wa kuwa pamoja, nilipokea tena pesa

Sio kwamba sikuthamini pesa (hapana)
Lakini wakati mwingine mtu hahitaji zawadi, anahitaji uwepo wako Anahitaji muda wako
Anahitaji kusikilizwa

Ndipo nikagundua kuwa kuna vitu ambavyo pesa haviwezi kununua, na kimojawapo ni muda wa mtu

Na si katika mapenzi tu

Kuna watu hunyimwa muda wa kujieleza

Kuna watu hunyimwa muda wa kuonyesha vipaji vyao

Kuna watu hunyimwa muda wa kusikilizwa

Kuna watu hunyimwa hata muda wa kuponya majeraha yao

Kuna watu hupoteza fursa mbali mbali kwa sababu walinyimwa mda

Basi, muda ni nini?
Unaelewa nini ukisikia neno mda?

Kwangu, muda ni maisha yenyewe
Kwa sababu kila kitu kinahitaji muda

kupenda, kusamehe, kukua, kupona, kufanikiwa na hata kuondoka

Na ndiyo maana tunasema
Muda ni mali, lakini zaidi ya mali, muda ni maisha

Ukimpa mtu muda wako, umempa sehemu ya maisha yako ambayo haitarudi tena ❤️⏳

ShesRise_1 🖐
Ukimpa mtu muda wako, umempa sehemu ya maisha yako ambayo haitarudi tena ❤️
b15d7dcf-1d64-4c0c-b4b6-5b23099fde26.jpeg
 
kati ya vitu nimetumia muda mwingi kuvisoma ni muda wenyewe, hapa nimeanzia zama za mawe hadi digital age, mifumo yote ya kalenda nimepitia mpaka zile siku 11 zilizopotea zilizoleta kizaazaaa, mifumo yote ya saa na technologies zote za saa mpaka cesium-133 atom na atomic clock,

International Meridian Conference in Washington na zero longitude kupita Greenwich bila time haya yote yasinge kuwepo, kitendo cha ku link time na positioning systems hapa ndo nikaanza kuamini time and space are two side of the coin na huwezi kivitofautisha, hapa ndo hayo mambo ya kupoteza muda, hakunipa muda, yote ni kuchanganya space na time ambayo ni kitu kimoja space-time

sikuishia hapo, nikaenda traditional astronomy mpaka precisely observation maana bila muda kosingetokea kitu, Kepler's planetary motions mpaka principia mathematica, nikaachana na classical physics mpaka quantum physics, relativity and time travel, hakuna kitu kimenipotezea muda kama theoretical physics hapa nili base kwenye haya mambo ya muda.

Hili suala la muda ni mada ndefu sana na ni very interesting, sekunde moja ni kubwa sana ukitaka kujua ukubwa wa sekunde fanya software development halafu function zako ziwe zina excute for 2 seconds wakati inatakiwa less than 20ms

Watu wengi hawajui hata kwanini siku ina masaa 24 wakati tunaweza tukaamua tu siku nzima iwe ni saa moja? hawajui kwanini masaa 24 ndo optimum choice. wazee kwenye muda hapa kuna madesa mengi kuliko vitu vyote ulivyosoma shule.

Mimi nikiwa na muda basi nadili na huohuo muda maana kunamambo mengi bado nataka kuyajua kuhusu muda
Shukrani kaka nina mengi natamani tuongee please ukipata mda tufanye ka mdahalo nijiokotee maarifa
 
Basi, muda ni nini?
Unaelewa nini ukisikia neno mda?

Kwangu, muda ni maisha yenyewe
Kwa sababu kila kitu kinahitaji muda

kupenda, kusamehe, kukua, kupona, kufanikiwa na hata kuondoka

Na ndiyo maana tunasema
Muda ni mali, lakini zaidi ya mali, muda ni maisha

Ukimpa mtu muda wako, umempa sehemu ya maisha yako ambayo haitarudi tena ❤️⏳
Hakika!
 
Back
Top Bottom