ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 16,833
- 39,851
Muda ni nini hasa?🤔
Kwa wengi wetu, muda ni kipimo kinachotuonyesha sasa ni saa ngapi, ni asubuhi, mchana au usiku
Tunautambua kwa kuangalia saa, simu au hata mwendo wa jua
Lakini je, muda ni saa tu?
Mara nyingi tunasikia maneno kama
Tumia muda wako vizuri
Usichezee muda wako
Muda ni mali
Muda ukipita haurudi tena
Muda utasema
Hapo ndipo ninapojiuliza, muda ni nini hasa?
Je, ni sekunde, dakika na saa zinazopita?
Au ni nafasi tunayopewa kuishi, kupenda, kujifunza na kutimiza ndoto zetu?
Umewahi kunyimwa muda na mtu uliyekuwa unamhitaji?
Mimi niliwahi kumpenda mtu
Na nilivyo nikipenda mtu hua ni huyo huyo siwezani na stress za wapenzi wengi so hua nategemea vingi kutoka kwake kwa sababu nakua sina sehemu nyingine ya kuvipata
Kila nilipomuonesha nime m miss ghafla nilipokea SmS
Imethibitishwa umepokea kiasi fulani kutoka kwa fulani
Kisha ananiambia S, kanunue wine unywe
Kitu ambacho si kibaya ila sikua naitaji pesa yake tu nilimtaka yeye pia
Sasa sielewi labda nilikua nazidisha sana kumuitaji mpaka akachoka au la🤔
Nilifurahi kwa sababu alikuwa ananijali kwa namna yake
Lakini ukweli ni kwamba sikuwa nahitaji pesa pekee
Nilikuwa mpweke.
Nilitamani anipe muda wake
Kila nikisema Babe, I miss you
Badala ya mazungumzo marefu au muda wa kuwa pamoja, nilipokea tena pesa
Sio kwamba sikuthamini pesa (hapana)
Lakini wakati mwingine mtu hahitaji zawadi, anahitaji uwepo wako Anahitaji muda wako
Anahitaji kusikilizwa
Ndipo nikagundua kuwa kuna vitu ambavyo pesa haviwezi kununua, na kimojawapo ni muda wa mtu
Na si katika mapenzi tu
Kuna watu hunyimwa muda wa kujieleza
Kuna watu hunyimwa muda wa kuonyesha vipaji vyao
Kuna watu hunyimwa muda wa kusikilizwa
Kuna watu hunyimwa hata muda wa kuponya majeraha yao
Kuna watu hupoteza fursa mbali mbali kwa sababu walinyimwa mda
Basi, muda ni nini?
Unaelewa nini ukisikia neno mda?
Kwangu, muda ni maisha yenyewe
Kwa sababu kila kitu kinahitaji muda
kupenda, kusamehe, kukua, kupona, kufanikiwa na hata kuondoka
Na ndiyo maana tunasema
Muda ni mali, lakini zaidi ya mali, muda ni maisha
Ukimpa mtu muda wako, umempa sehemu ya maisha yako ambayo haitarudi tena ❤️⏳
ShesRise_1 🖐