Muda ambao Mungu anafungua milango hakuna cha kuzuia, endeleeni kupambana kutafuta fursa za ajira na tenda

Championship

JF-Expert Member
Aug 7, 2019
5,499
10,540
Kuna miaka kama mitatu hivi nilipitia changamoto na fursa zikawa haziji. Nilikuwa natamani hata kupata kazi ya kulipwa chini ya milioni na haikupatikana. Sasa hivi hata siamini namna miaka mitano tu inavyoweza kubadilisha maisha ya mtu.

Nikaendelea kuomba fursa karibu kila sehemu. Kumbuka nina uzoefu mkubwa kwenye telecom, IT kwa ujumla na usimamizi wa miradi. Lakini ni kama milango ilikuwa imefungwa. Nimetuma zaidi ya applications 500. Nimeitwa interview nne tu kwenye maombi yote hayo.

Nilomba consultancy kwenye NGO moja na walioomba walikuwa zaidi ya watu 200 Afrika nzima na walitaka mtu mmoja tu. Niliipata hii na monthly consultancy fee ni 5.5m (bado naifanya maana ni remote work).

Baada ya pale haikupita miezi 6 nikapata mkataba wa miaka miwili kwenye benki moja uliokuwa na thamani ya 160m. Yaani nilibakia kumshukuru sana Mungu. Ikafika mahali nikawa naweza ku-save mpaka 70m kwa mwaka.

Muhimu usiache kujiongezea thamani, fanya certification mbalimbali zinazotambulika kimataifa. Ukiweza fanya masters pia. Endelea kupambana na usikate tamaa, milango itafunguka muda sio mrefu. Na ukipata fursa, deliver without excuses.

Be encouraged by these few words.
 
Kuna miaka kama mitatu hivi nilipitia changamoto na fursa zikawa haziji. Nilikuwa natamani hata kupata kazi ya kulipwa chini ya milioni na haikupatikana...
Mkuu noma....umekuja wakat sahihi maana Kila siku na update CV na nme apply post 500+ nliitwa Moja nkapata af siku ya kuanza kazi wakanibadilikia.

yani bila hii post yako nilikua naamini nmelogwa ila now umenipa Imani Mungu pekee hajanifungulia naendelea kumtanguliza anifungulie.

Screenshot_20240125-000835_1.jpg
 
Ushauri wangu mkuu kazi za sekta binafsi usibweteke sana labda kama una lengo la kusave na kufanya biashara baadae.
Mkuu haiwezekani kubweteka maana nafanya kama consultant sehemu moja na nyingine ni mkataba wa miaka miwili na ku-renew.

Hela zipo kwenye uwekezaji wa hisa, bond na vipande. Biashara sina muda wa kufanya kwa sasa.
 
Mkuu haiwezekani kubweteka maana nafanya kama consultant sehemu moja na nyingine ni mkataba wa miaka miwili na ku-renew.

Hela zipo kwenye uwekezaji wa hisa, bond na vipande. Biashara sina muda wa kufanya kwa sasa.
Safi mkuu maana na mimi nilipitaga private sector nikaona nijazie nyama kidogo.
 
Back
Top Bottom