Mtumishi akitaka kujua deni lake analodaiwa HESLB aombe Loan Statement, deni halisi ni tofauti sana na linaloonekana kwenye Salary slip

Ndugu walimu wenzangu na wanufaika wote waliosomeshwa kwa fedha ya serikali yaani BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB),,, Juzi Jumatatu tarehe 28.12.2020 niliomba LOAN STATEMENT ya deni langu kutoka Bodi ya mikopo ili niweze kuclear deni baki ambalo kwa mujibu wa SALARY SLIP yangu ya 31.12.2020 Deni linasomeka Tsh. Mil 4.65

Aidha, cha kushangaza na kushtua jana HESLB wakanitumia kwa njia ya email statement ya deni langu ambapo Deni langu linasomeka nadaiwa Tsh. Mil 12.087 wakati kwenye Salary slip ya mwezi deni ni Tsh. Mil 4.65. Kiukweli nilichanganyikiwa nikawatumia ujumbe Bodi ya mikopo kuomba ufafanuzi wa hiki na leo Jumatano asbh nikajibiwa kuwa hakuna kilichokosewa kwenye statement waliyonitumia jana.

Baada ya kuona sielewi imelazimika nisafiri hadi Halmashauri kuonana na AFISA UTUMISHI ili aweze kunipa ufafanuzi wa jambo hili, nilipofika akampigia simu AFISA kutoka makao makuu ya HESLB ambaye ndo anashugulika na makato ya fedha zote kutoka kwa wanufaika wote nchini, alimpigia palepale mbele yangu na akaweka Loud speaker yule Afisa wa Bodi akaelez a mambo mengi sanaa kuhusiana na fedha hii.

Ambapo kiujumla amesema kwamba watumishi wote tunaokatwa kupitia mishahara yetu deni tunaloliona kwenye hizo salary kama linapungua sio deni halisi bali deni la halisi analodaiwa mnufaika wanalo wao Bodi kwenye mfumo wao ambao mfumo wao hauna mahusiano yyte na Mfumo wa Lawson, hivyo deni letu halisi huwa haliwi updated kwenye salary slip ndo maana tunaona kila mwezi linapungua ila kiuhalisia ni hapana.

Akaendelea kusema mtumishi yeyote akitaka ajue deni lake halisi analodaiwa basi aombe Loan Statement kutoka Bodi hapo ndo anaweza kujua deni lake halisi ambalo ni tofauti sanaaa na linaloonekana kwenye Salary slip zetu.

Akasema tena deni lililopo kwenye salary slip linapokwisha mtumishi anaweza akaona kama vile kamaliza deni, kumbe kuna deni kule bodi bado wanamdai. Hivyo akasema sasahv wapo kwenye mchakato wa kuandaa barua kuwatumia waajiri wote nchini madeni mapya ya wale wote ambao washakamilisha kulipa deni la kwenye salary slip ili makato yaendelee kama kawaida.

Mwisho Afisa huyo akamuomba Afisa Utumishi anipatie mimi namba ya huyo Afisa ili kama mahali nitakuwa sijamwelewa vzr niweze kumpigia wkt wwte kwa maelezo ya kina.

Hivyo ndugu watumishi na walimu wenzangu ambao ni wahanga wa hili tusijipe matumaini ya kuclear hili deni tunaweza hata kustaafu nalo. Tupambaneni kutafuta hela ili watoto wetu tuwanusuru na kuingia kwenye hili janga la Bodi ya mikopo ili tuwasomeshe kwa fedha zetu hata kwa kujibana maana inauma sanaaa.

Yeyote atakayehitaji namba ya simu ya huyu Afisa kutoka HESLB kwa ajili ya maelezo ya ziada anaweza kunitafuta inbox nikamtumia. Asante

BY. MWL MUSSA A. IDDY
NAMONGE SEKONDARI
Pole ndugu yangu hata mimi yalinikuta mwajiri wangu kamaliza kulipa sikatwi nikasikia wenzangu wanalia kuwa wamebambikiwa madeni na loan board nikaenda kuchukua statement nikakuta kuna deni la 1.4m nikataka ufafanuzi wakaniambia ni malimbikizo ya riba da kwa nini hamkujumlisha ili mwajili alipe hawana majibu.nina mashaka wanacheza na system yao kuwatapeli watu.haiwezekani kila mtu analalamikia loan board kwa nini? Kuna haja ya vyombo vya serikali kufanya uchunguzi pale pana tatizo kubwa
 
Hakuna mkopo usio na ukomo sajo
Nenda bodi kule watakupa ulichokopeshwa, gharama za mkopo, muda uliokaa na mkopo, muda ulioanza marejesho, muda wa kumaliza.... pamoja na riba zake
Nilichomaanisha ni hiki, benki umekopa milioni 1 kwa miaka 3, unaambiwa deni na riba ni milioni 3; hili litabaki hivi hata kama utalipa baada ya miaka 10

Bodi ya mkopo: Mkopo milioni 2, umeenda leo utapewa statimenti kuwa deni na riba na retention ni milioni 4. Hujalipa chochote, baada ya miezi 12 utaambiwa deni lote ni milioni 5, mwaka ujao ni milioni 8 nk
Pole ndugu yangu hata mimi yalinikuta mwajiri wangu kamaliza kulipa sikatwi nikasikia wenzangu wanalia kuwa wamebambikiwa madeni na loan board nikaenda kuchukua statement nikakuta kuna deni la 1.4m nikataka ufafanuzi wakaniambia ni malimbikizo ya riba da kwa nini hamkujumlisha ili mwajili alipe hawana majibu.nina mashaka wanacheza na system yao kuwatapeli watu.haiwezekani kila mtu analalamikia loan board kwa nini? Kuna haja ya vyombo vya serikali kufanya uchunguzi pale pana tatizo kubwa
Vyombo gani vya serikali vifanye uchunguzi? Na hayo makato yanayofanyika kwani yanaenda mifukoni mwa watendaji wa bodi au kwa fuko la serikali?
 
Kusomesha sio lelemama cocastic, wazazi wanajinyima sana ili watoto wapate kilicho bora

Wewe ukimaliza washukuru sana na ukianza kupata kipato weka standing order bank pesa iwe inaingia kwenye account yao moja kwa moja kama shukrani
Wachaa kabisaa mama, nilishawaambia na wao wenyewe wanajua, nikibahatika kupata ajira, yaan mshahara wa miez 3 ya mwanzo ni wao.
Ni shukrani zangu kwao.
 
Nilichomaanisha ni hiki, benki umekopa milioni 1 kwa miaka 3, unaambiwa deni na riba ni milioni 3; hili litabaki hivi hata kama utalipa baada ya miaka 10

Bodi ya mkopo: Mkopo milioni 2, umeenda leo utapewa statimenti kuwa deni na riba na retention ni milioni 4. Hujalipa chochote, baada ya miezi 12 utaambiwa deni lote ni milioni 5, mwaka ujao ni milioni 8 nk

Vyombo gani vya serikali vifanye uchunguzi? Na hayo makato yanayofanyika kwani yanaenda mifukoni mwa watendaji wa bodi au kwa fuko la serikali?
Vyombo kama takukuru nk wakachunguze mifumo yao ya kutunza kumbukumbu haiwezekani mlete deni kwa mwajiri nimalize kulipa alafu nijikute nadaiwa tena
 
Wachaa kabisaa mama, nilishawaambia na wao wenyewe wanajua, nikibahatika kupata ajira, yaan mshahara wa miez 3 ya mwanzo ni wao.
Ni shukrani zangu kwao.
Mshahara wa kwanza shukrani kwa Mungu wengine hufanya maulid, wengine sadaka ya shukrani, mshahara wa kwanza kwa wazazi🙏 Sasa ukiahidi halafu ukashindwa kutekeleza ni mbaya mnooo. Ila kamwe usiache kumshukuru Mungu na wazazi

Japo mshahara haujawahi kutosha hata siku moja😂😂😂😂
 
Ndugu walimu wenzangu na wanufaika wote waliosomeshwa kwa fedha ya serikali yaani BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB),,, Juzi Jumatatu tarehe 28.12.2020 niliomba LOAN STATEMENT ya deni langu kutoka Bodi ya mikopo ili niweze kuclear deni baki ambalo kwa mujibu wa SALARY SLIP yangu ya 31.12.2020 Deni linasomeka Tsh. Mil 4.65

Aidha, cha kushangaza na kushtua jana HESLB wakanitumia kwa njia ya email statement ya deni langu ambapo Deni langu linasomeka nadaiwa Tsh. Mil 12.087 wakati kwenye Salary slip ya mwezi deni ni Tsh. Mil 4.65. Kiukweli nilichanganyikiwa nikawatumia ujumbe Bodi ya mikopo kuomba ufafanuzi wa hiki na leo Jumatano asbh nikajibiwa kuwa hakuna kilichokosewa kwenye statement waliyonitumia jana.

Baada ya kuona sielewi imelazimika nisafiri hadi Halmashauri kuonana na AFISA UTUMISHI ili aweze kunipa ufafanuzi wa jambo hili, nilipofika akampigia simu AFISA kutoka makao makuu ya HESLB ambaye ndo anashugulika na makato ya fedha zote kutoka kwa wanufaika wote nchini, alimpigia palepale mbele yangu na akaweka Loud speaker yule Afisa wa Bodi akaelez a mambo mengi sanaa kuhusiana na fedha hii.

Ambapo kiujumla amesema kwamba watumishi wote tunaokatwa kupitia mishahara yetu deni tunaloliona kwenye hizo salary kama linapungua sio deni halisi bali deni la halisi analodaiwa mnufaika wanalo wao Bodi kwenye mfumo wao ambao mfumo wao hauna mahusiano yyte na Mfumo wa Lawson, hivyo deni letu halisi huwa haliwi updated kwenye salary slip ndo maana tunaona kila mwezi linapungua ila kiuhalisia ni hapana.

Akaendelea kusema mtumishi yeyote akitaka ajue deni lake halisi analodaiwa basi aombe Loan Statement kutoka Bodi hapo ndo anaweza kujua deni lake halisi ambalo ni tofauti sanaaa na linaloonekana kwenye Salary slip zetu.

Akasema tena deni lililopo kwenye salary slip linapokwisha mtumishi anaweza akaona kama vile kamaliza deni, kumbe kuna deni kule bodi bado wanamdai. Hivyo akasema sasahv wapo kwenye mchakato wa kuandaa barua kuwatumia waajiri wote nchini madeni mapya ya wale wote ambao washakamilisha kulipa deni la kwenye salary slip ili makato yaendelee kama kawaida.

Mwisho Afisa huyo akamuomba Afisa Utumishi anipatie mimi namba ya huyo Afisa ili kama mahali nitakuwa sijamwelewa vzr niweze kumpigia wkt wwte kwa maelezo ya kina.

Hivyo ndugu watumishi na walimu wenzangu ambao ni wahanga wa hili tusijipe matumaini ya kuclear hili deni tunaweza hata kustaafu nalo. Tupambaneni kutafuta hela ili watoto wetu tuwanusuru na kuingia kwenye hili janga la Bodi ya mikopo ili tuwasomeshe kwa fedha zetu hata kwa kujibana maana inauma sanaaa.

Yeyote atakayehitaji namba ya simu ya huyu Afisa kutoka HESLB kwa ajili ya maelezo ya ziada anaweza kunitafuta inbox nikamtumia. Asante

BY. MWL MUSSA A. IDDY
NAMONGE SEKONDARI
Ukweli ni huo kwamba pana tofauti kubwa ya updates na kinachochangia ni rentention fee,,,jumanne ya Tarehe 5 January niliomba statement yangu niangalie balance,,kweli it was a surprise to me! Nilishangaa sana kuona Kuna kiasi kimeongezeka cha retention fee karibia 600k,,,rate for retention ni kubwa mno na kiukweli serikali yetu sikivu ni muhimu kuliangalia maana tunaweza jikuta ni isidingo
 
Wazazi wako walikupenda sana wazazi wako Infantry Soldier, hawakutaka uanze kudaiwa mapema
Kuwashukuru zaidi unaweza kuanza kuweka standing order bank na wao wakaanza kupokea marejesho🤣🤣🤣
🤣🤣🤣🤣 hakika huu ni ushauri mzuri sana. Mungu atafungua milango ya baraka na wazazi watafurahia matunda yangu
 
Ndugu walimu wenzangu na wanufaika wote waliosomeshwa kwa fedha ya serikali yaani BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB),,, Juzi Jumatatu tarehe 28.12.2020 niliomba LOAN STATEMENT ya deni langu kutoka Bodi ya mikopo ili niweze kuclear deni baki ambalo kwa mujibu wa SALARY SLIP yangu ya 31.12.2020 Deni linasomeka Tsh. Mil 4.65

Aidha, cha kushangaza na kushtua jana HESLB wakanitumia kwa njia ya email statement ya deni langu ambapo Deni langu linasomeka nadaiwa Tsh. Mil 12.087 wakati kwenye Salary slip ya mwezi deni ni Tsh. Mil 4.65. Kiukweli nilichanganyikiwa nikawatumia ujumbe Bodi ya mikopo kuomba ufafanuzi wa hiki na leo Jumatano asbh nikajibiwa kuwa hakuna kilichokosewa kwenye statement waliyonitumia jana.

Baada ya kuona sielewi imelazimika nisafiri hadi Halmashauri kuonana na AFISA UTUMISHI ili aweze kunipa ufafanuzi wa jambo hili, nilipofika akampigia simu AFISA kutoka makao makuu ya HESLB ambaye ndo anashugulika na makato ya fedha zote kutoka kwa wanufaika wote nchini, alimpigia palepale mbele yangu na akaweka Loud speaker yule Afisa wa Bodi akaelez a mambo mengi sanaa kuhusiana na fedha hii.

Ambapo kiujumla amesema kwamba watumishi wote tunaokatwa kupitia mishahara yetu deni tunaloliona kwenye hizo salary kama linapungua sio deni halisi bali deni la halisi analodaiwa mnufaika wanalo wao Bodi kwenye mfumo wao ambao mfumo wao hauna mahusiano yyte na Mfumo wa Lawson, hivyo deni letu halisi huwa haliwi updated kwenye salary slip ndo maana tunaona kila mwezi linapungua ila kiuhalisia ni hapana.

Akaendelea kusema mtumishi yeyote akitaka ajue deni lake halisi analodaiwa basi aombe Loan Statement kutoka Bodi hapo ndo anaweza kujua deni lake halisi ambalo ni tofauti sanaaa na linaloonekana kwenye Salary slip zetu.

Akasema tena deni lililopo kwenye salary slip linapokwisha mtumishi anaweza akaona kama vile kamaliza deni, kumbe kuna deni kule bodi bado wanamdai. Hivyo akasema sasahv wapo kwenye mchakato wa kuandaa barua kuwatumia waajiri wote nchini madeni mapya ya wale wote ambao washakamilisha kulipa deni la kwenye salary slip ili makato yaendelee kama kawaida.

Mwisho Afisa huyo akamuomba Afisa Utumishi anipatie mimi namba ya huyo Afisa ili kama mahali nitakuwa sijamwelewa vzr niweze kumpigia wkt wwte kwa maelezo ya kina.

Hivyo ndugu watumishi na walimu wenzangu ambao ni wahanga wa hili tusijipe matumaini ya kuclear hili deni tunaweza hata kustaafu nalo. Tupambaneni kutafuta hela ili watoto wetu tuwanusuru na kuingia kwenye hili janga la Bodi ya mikopo ili tuwasomeshe kwa fedha zetu hata kwa kujibana maana inauma sanaaa.

Yeyote atakayehitaji namba ya simu ya huyu Afisa kutoka HESLB kwa ajili ya maelezo ya ziada anaweza kunitafuta inbox nikamtumia. Asante

BY. MWL MUSSA A. IDDY
NAMONGE SEKONDARI
Mshana Jr upo? tulishakuwa na wasiwasi uko wapi.. si unajua kutekana hakujaisha
 
Loan board statement inasoma deni la 13mlns , salary slip inasoma 6mlns zimebaki.
We have a problem with loan board, why they should continue adding rendition fund ?
 
Deni la bodi linakatisha tamaa sana.
Mimi nilimaliza kwenye salary slip mwaka jana septemba hivyo hawanikati tena.
Sitaenda kudai hilo deni halisi kama wanavyosema maana mbona kuna watu watu hawajapata ajira n a wengine hawajaanza kukatwa hadi leo. Wao siku wakinipata wanikate tu.
Cha ajabu niliongeza elimu ndo nikasomeshwa na bodi lakini elimu niliyoongeza haijawahi kuniongeza mshahara zaidi ni deni nalipa.
😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom