mpasta
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 917
- 1,997
Niende kwenye hoja Moja kwa moja. Nikiwa ni mnufaika wa mkopo wa HELSB,
Nilianza kulipa deni langu mwaka 2009 mpaka kufika 2014 nikawa nimemaliza deni langu lililoletwa kwa muajiri wangu.
Ghafla mwezi Septemba mwaka 2022 nikaona muajiri wangu ameanza kunikata deni upya tena kubwa kuliko deni langu halisi la mwanzoni. Nilipoenda kufuatilia na salary slips zangu za malipo wakaniomba samahani kuwa wamenibambikia deni la mtu mwingine ila Ile mwaka 2014 kuna deni nilibakiza.
Sikutaka majibizano nao nikakubali yaishe. Sasa nikaanza kukatwa na muajiri wangu baadae nikatafuta pesa pembeni nikalipa kwa control number. Sasa nafuatilia barua ya kuonyesha nimemaliza mkopo wangu ili nikampe muajiri wangu asitishe makato hawana majibu yanayoeleweka. Wanasema hazina hawajawapa bodi pesa za makato ya mwezi Januari 2023.
Binafsi siamini kama kweli hazina wanaweza kukata pesa ya mtumishi halafu wasiwasilishe sehemu husika kwa wakati.
Tunaomba bodi mtupe majibu ya kueleweka, mnawatesa watumishi ambao wameshamaliza mikopo yenu ya ngumi ya ndoige ya mandonga inayobadilika badilika kila wakati.
Tukipiga simu zenu za huduma kwa wateja hazipokelewi, zinaita mpaka zinakata