Mtume Mwamposa na jaribu la imani

Mtume Mwamposa na jaribu la imani

Pia waweza kuuliza hivi, ni kwa nini Mwenyezi Mungu asimpe ishara kuwa haya yatatokea? Hilo swali lako lapaswa kujibiwa ya huyo Mwenyezi Mungu unayemtuhumu kutotoa ishara.



Sent from my SM-T355Y using Tapatalk

Hapa anatuhumiwa nabii koko, hana cha unabii wala unini ni utapeli, wizi na uzandiki
 
Mkuu umedadavua vizuri ila kuna wakati unajichanganya. Unasema ni makosa kumfananisha mwamposa na kibwetere. Mi sioni tofauti zao. Wa mwamposa wanaona wa kibwetere potofu na wa kibwetere wanaona wa mwamposa potofu. Wote wameruhusiwa na mamlaka za nchi zao kueneza neno. Mimi naona wote wawili ni potofu.

Kibwetere alifunga milango ya kanisa waumini wakateketea. Mwamposa kuweka mafuta kwenye mlango wa geti moja maelfu ya waumini wapite wakikanyaga, wakafa. Kwangu mimi sioni tofauti. Yote ni makosa yatokanayo na kukosa busara ya kimungu.

Wewe mwenyewe umeweka swali "Mwenye jukumu la kupima usahihi wa mafundisho ni nani hasa linapokuja suala la imani?". Sasa kama unaona ni ngumu kupima usahihi wa mafundisho ya kiimani, ni kwa nini unabeza imani ya kina kibwetere? Kubali kila mtu abaki na imani yake. We unaona ya mwamposa sawa, kibwetere anaona yake sawa, mi naona ya wamposa na kibwetere si sawa ni utapeli, bali imani yangu ndio sawa.

Kwa kifupi hautafanikiwa kutetea usahihi wa imani ya mwamposa, achilia mbali kumuondoa kwenye hatia ya vifo vilivyotokana na aliyofanya.

Na ni bora baada ya hii kesi ashauriwe aachane na jina "bulldozer". Ame bulldoze watu to death!!!
Hapa umepiga siasa mkuu. Kibwetere alisimama kama mkristo, akitumia biblia. Mwisho wa siku aliwaambia waumini wake mwisho wa dunia umefika akawafungia ndani na kuwacchoma moto. Swali kwako, hilo fundisho LA KUUA limo kwenye biblia ama ni serikali ipi duniani ingeruhusu mtu binafsi kuhujumu maisha ya mwingine?

Mwamposa ni wapi aliwafungia waumini akawamwagia mafuta akawachoma moto? Ama labda amewapa mafuta yenye sumu wakafa? Yeye kafundisha anachoamini kamaliza, akafanya zoezi la kukanyaga mafuta ambalo hufanyika kwenye ibada zake mara zote, kilichotokea kwa sababu ya kushindwa ukontroo watu wakarundikana na kukanyagana.

Kwa mtazamo wako Mwamposa na Kibwetere wana kesi sawa ya kujibu? Aliyewasha moto na kuwachoma watu na yule aliyeweka mafuta watu wakanyage badala yake wakarundikana n kukanyagana wao wenyewe? Haya nionyeshe wapi kufanana kwao. Kosa la kibwetere ni la mauaji, kosa la Mwamposa hapo ni lipi?



Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Umejibu vizuri ila swali la mwanzo kuhusu kuweka mafuta mlango moja kati ya milango nane hujalijibu vizuri. Vipi tuendelee kusubiria majibu au tuomboleze kwanza?
Nimeelezea nafharia yangu, kuweka mlango mmoja yaweza kuwa ni kwa ajili ya kukontroo watu, ila wakawazidi nguvu kila mmoja anataka kuwahi. Nikuulize swali, umewahi kuona utaratibu unaotumika kwenye ibada zake kanisani? Je huwa ana kawaida ya kuweka vipi hayo mafuta? Think

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Msijifanamishe na Yesu ninyi ni binadamu wa kawaida zaidi ya ukawaida wenyewe,KASOMENI,tafuteni ELIMU,mshikeni sana ELIMU,
unvyosema Yesu hakuanzisha chuo mbona hausemi Yesu hakuanzisha kukanyagisha watu mafuta,
Afu skieni bana acheni kujitutumua kwa kujidai mnafanya aliyofanya Masihi,km ndo mnavyofnya mbona mmekimbilia kuwazika marehemu na hamkuwafufua km Yesu alivyomfufua Lazaro ama Paulo alivyofnya?
Jifunzeni kujinyenyekeza siyo kunyenyekewa,utumishi wa kujipa mbaya

Sent using Jamii Forums mobile app
Hoja yako haieleweki. Unadhani wakati wa Yesu wote waliokufa walifufuliwa? Soma biblia. Kuhusu elimu wala sijakukataza, nachosema sio kigezo cha kumhubiri Kristo. Hilo ni jwa wale wenye kuelewa maandiko, the great commission.

Kujitutumua ni feelings zako tu, biblia imetaka kumfuata Kristo kama mfano, sasa wewe unapinga, sijakuelewa unakusudia nini.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Swali jingine,
Ni kweli uwepo wa Mungu ulikuwepo pale km wanavyojidai?
Mkutano kwa yaliyotokea unaonesha ulikuwa na kibali cha nani,muuaji ama mponyaji,
Mungu ama shetani?,
Utaskia oooo katika ulimwengu wa roho!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Swali hili waweza kulijibu wewe, mimi sina huo uwezo kujua uwepo wa Mungu. Kwani mitume walipokuwa magerezani wafungwa wengine wakifa wao wanaishi (kama Patmo alikofungwa Yohana) kwani Mungu alikuwepo? Maswali hayo ni ya Mungu mwenyewe, niulize maswali yanayonistahili?

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Sitaki kuhukumu lakini Injili ya kweli iletayo wokovu siku hizi ni nadra. Watu wamejikita kwenye shida za watu na ahadi za mafanikio, kinyume kabisa na Yesu alivyoagiza kwamba utafuteni kwanza ufalme wa mbinguni na hayo yote mtazidishiwa. Watu wamejikita kwenye kuhangaika na mambo ya ziada kuliko kuponya roho na nafsi zao zimgeukie Mungu.

Hawa watu wangekua na mafundisho ya kweli wakamjua Mungu vyema hekima naaarifa ya kuwatanguliza wengine au kuona hsijalishi upite wa kwanza au wa mwisho baraka zipo pale pale.

Yesu aliwahi kukemea kizazi kinachofuata ishara na miujiza. Lakini leoanabii wengi ndicho wanachokifanya. Hii ndio kuangamia kwa kukosa maarifa.
 
Kama huamini kama kuna mafuta matakatifu iweje ukubaliane na hoja ya kuwa huyu jamaa sio tapeli

Kuhusu kukataa theologia hawa wachungaji wanapoenda hivyo vyuo vya biblia wanafundishwa na kina nani

Kuhusu point ya kuwafungulia watu geti moja umepuyanga huna point ya msingi umeandika consipirancy juu ya wazo lako ndio maana ukaanza na neno “ inawezekana”

Tunahimizwa kumpenda Mungu kwa nguvu zetu zote, na akili zetu zote......ndugu zetu mnapotea kwa kuwa mnampenda Mungu kwa mhemuko akili mnaacha ndio maana mkiambiwa kunyweni jiki mnakunywa

Unasema tusome biblia ni wapi kwenye biblia pameandika tukanyage mafuta ili tupate baraka


Sent from my iPhone using JamiiForums

Kuhusu mafuta matakatifu ni mambo ya torati, sasa tunaye Roho Mtakatifu.

Kuhusu utapeli hilo ni lako kwa sababu Yesu aliwaagiza wanafunzi wake pia waende wakawapake wagonjwa mafuta wawapoze. Kuhukumu si kazi yangu ndugu.

Kuhusu teolojia mimi binafsi ndio sipendi huo utaratibu. Hawa kina Mwamposa wanaweza kuwa wanaamini katika hilo, ila mimi naona ni utaratibu unaopandikiza imani potofu kwa kutwist maandiko.

Kuhusu geti moja mimi naandika nachofikiri on the positive side kwa sababu kila mmoja wenu amekuja na lake, wengine uxchawi, wengine kafara n.k. Ni kawaida kwa haters kukimbilia huko pale linapotokea tatizo. Mwamposa huweka mafuta kila mara kwa utaratibu huo huo, watu hupanga mstari na kukanyaga wakatoka nje. Nini kilichotolea hapo Moshi ni kushindwa kuwadhibiti watu waliokimbilia kuwahi mbele ili kila mtu awahi kwenda kwake. Utaratibu ungefuatwa wala tusingejua kama Mwamposa alikuwa Moshi. Hicho ndicho ninachokiamini mimi.

Kumpenda Mungu unajua ni nini? Ndio maana nakusisitiza soma biblia uwe huru katika Kristo. Kwa hiyo kunywa jik ni kumpenda Mungu? Ama unadhani kubusu msalaba ni kumpenda Mungu. Biblia inasema hivi kuhusu hilo:

Yohana 14

²³ Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
²⁴ Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka.


Kumpenda Mungu ni kulishika Neno lake, sio kwenda chuo kikuu. Hiyo haikatazi mtu kusoma hata kuwa na phd, bali phd yako si kipimo cha kumpenda Mungu.

Habari za kunywa jik ni ujinga wa kutosoma maandiko. Haipishani na kufanya ibada za kuabudu ekaristi ambazo hazimo kwenye biblia. Yako mengi ambayo teolojia imetunga na kuyafanya ya Mungu. Kwa hiyo wasiosoma maandiko hunaswa na mtego wa shetani.

Biblia haijaandika kukanyaga mafuta huleta baraka. Mimi sio mwamini wa mafuta, ila naweza kusema tu, kwa logic yako, wapi biblia imesema watu wabusu msalaba? Sidhani kama hiyo ni logic nzuri. Heri ungeuliza ni wapi biblia inazungumzia habari ya mafuta? Peteo aliponya watu kwa kivuli chake tu, ni wapi Yesu alifanya hilo?

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
huwa nafuatilia maandiko yako mengi sana hapa jamvini ndugu Nyenyere ......... unajua kujenga hoja hongera sana!


mimi kama m-pentekoste ninayeijua imani yangu naamini kabisa kwa sehemu kubwa bado watumishi wengi hawamjui Mungu hasa ndio maana tunalazimishwa kumfuata Mungu kwa matakwa ya taasisi zetu na sio vile Mungu atakavyo!


hili la Mwamposa nadhan ni matokeo ya taasisi za kidini nyingi kumhodhi Mungu kama mali yao, yani wanamfanya Mungu kama wa kwao na vile wanavyosema wao ndivyo alivyo which i think is totally wrong!....


sasa, ukifuatilia matamko mengi na maneno mengi mitaani inaonekana Mwamposa (binafsi simfahamu hata) ni mtume wa uongo n.k kwa sababu tu ameenda tofauti na yule Mungu wao wanataka wote tumfuate!......


hawa hawa wanaomkosoa mwamposa walipanga foleni kule Loliondo kunywa mitishamba katika mazingira machafu sana, hata wakatengeneza barabara ndani ya wiki sijui mwezi! UNAFIKI mtupu

Sent using Jamii Forums mobile app

Tuko pamoja mkuu. Nimependa hapo, taasisi kumhodhi Mungu. Huo ndio msingi mkuu wa tatizo.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Hapa anatuhumiwa nabii koko, hana cha unabii wala unini ni utapeli, wizi na uzandiki
Mwamposa ni MTUME, hilo la unabii mnalijua ninyi huko kwenye imani yenu.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Ila hiyo theology haizuii watato kulawitiwa
Degrees in theology or further is the solution

For instance Catholic,Lutheran and Adventist clergies are well trained in theology...u never hear this kind of drama in RC,Lutheran or even Muslims

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitaki kuhukumu lakini Injili ya kweli iletayo wokovu siku hizi ni nadra. Watu wamejikita kwenye shida za watu na ahadi za mafanikio, kinyume kabisa na Yesu alivyoagiza kwamba utafuteni kwanza ufalme wa mbinguni na hayo yote mtazidishiwa. Watu wamejikita kwenye kuhangaika na mambo ya ziada kuliko kuponya roho na nafsi zao zimgeukie Mungu.

Hawa watu wangekua na mafundisho ya kweli wakamjua Mungu vyema hekima naaarifa ya kuwatanguliza wengine au kuona hsijalishi upite wa kwanza au wa mwisho baraka zipo pale pale.

Yesu aliwahi kukemea kizazi kinachofuata ishara na miujiza. Lakini leoanabii wengi ndicho wanachokifanya. Hii ndio kuangamia kwa kukosa maarifa.
Umenena iliyo kweli mkuu, leo hii mafundisho mengi hayalengi kumtafuta Mungu na kujenga ufalme wake. Tunatafuta sana ufalme wa dunia hii kwa sababu ya starehe zake zinazoonekana kwa macho. Wajanja wachache wametumia nafasi hii kuwakamua masikini.

Biashara ya injili

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Umenena iliyo kweli mkuu, leo hii mafundisho mengi hayalengi kumtafuta Mungu na kujenga ufalme wake. Tunatafuta sana ufalme wa dunia hii kwa sababu ya starehe zake zinazoonekana kwa macho. Wajanja wachache wametumia nafasi hii kuwakamua masikini.

Biashara ya injili

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk

Kwa sababu kama ni kweli nia na lengo la haya makanisa ni kuihubiri Injili ya Yesu Kristo, kwanini wote wanarundikana mjini ambapo tayari makanisa na watumishi wengi wapo wakimtangaza Kristo?

Walitakiwa waende vijijini kwenye ukame na uhaba wa watumishi wawapelekee wahitaji habari njema. Hii ya kung'ang'ania mjini inazidi kuleta fikra kwamba lengo kuu ni biashara na sio roho zinazopotea dhambini.
 
Mtoa mada anatetea ujinga, kwenye maandiko, wapi imeandikwa kuna kukanyaga mafuta halafu madhehebu yaangalie kama kuna ukweli, wakati ni uongo. Huna neno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuwa nikitafakari kile kinachoendelea kufuatia tukio la vifo vya watu 20 vilivyotokea huko Moshi kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa "Bulldozer." Baada ya tukio hilo kumekuwa na maoni mengi na mitazamo tofauti kwa ujumla kutokana na jinsi ukio hilo lilivyotokea, nami nimeona nitoe mtazamo wangu juu ya jambo hili.

Chanzo cha vifo ni kipi hasa?

Hapa nimeona nichambue kwa kina tatizo hasa ni nini. Kumekuwa na mitazamo hasi kuhusiana na chanzo hasa cha vifo kiasi kwamba kumekuww na hasira kali juu ya imani ya baadhi ya watu.

1. Je vifo vimetokana na mafuta?
Ukitafakari kwa kina utaona hili si kweli. Mafuta hayakusababisha hivyo vifo kwa sababu hayuko hata mmoja aliyetumia mafuta hayo na kufariki. Mafuta hayo yamekuwa yakikanyagwa mara nyingi, kwa miaka mingi pasipo kuwa na madhara kwa watumiaji.

2. Je vifo vimesababishwa na mafundisho?
Ni muhimu kupima mafundisho kama ndio chanzo hasa cha vifo hivi. Kwamba kile kilichohubiriwa siku hiyo ndicho kilichopelekea watu kukanyagana hata vifo kutokea. Kama siku hiyo waliambiwa watakuokuwa wa kwanza kukanyaga mafuta watapokea upako kiasi cha kuwalazimu waamini kugombania nafasi ya kwanza basi hilo ni tatizo. Lakini kama fundisho lilikuwa ni kwamba kukanyaga mafuta tu ni kupokea baraka, basi haijalishi kama ni wa kwanza ama ni wa mwisho.

3. Je vifo vimesababishwa na mafundisho potofu?
Hili ni suala pana kwa sababu limelenga mambo ya kiimani. Nilishangaa jana pale nilipomsikiliza waziri Simbachawene akielezea jinsi ambavyo huwa anaangalia baadhi ya mafundisho na kujiuliza kama kuna Mungu pale. Siamini kama ni jukumu la waziri kupima wapi pana Mungu wa kweli na wapi hapana Mungu.

Mwenye jukumu la kupima usahihi wa mafundisho ni nani hasa linapokuja suala la imani? Nimesikia hoja yabkuwa na wahubiri wenye digrii ya teolojia. Je, ni sehemu gani kwenye Biblia ambapo Yesu alianzisha chuo cha teolojia ama kuagiza kianzishwe? Teolojia ni elimu ya kimfafanua Mungu KWA MTAZAMO WA ANAYEFUNDISHA. Hili ni tatizo. Tukifika hapo itabidi waprotestanti, wasabato, wakatoliki, moraviani, waanglikana na walutheri wakalishwe chini kuamua mafundisho yapi ni ya Mungu wa kweli. Itabidi tuamue teolojia ipi ni ya kweli na ndiyo hasa anayoikubali Mwenyezi Mungu.

Labda tujiulize mafundisho potofu ni nini? Hapo ndipo penye mgogoro na si vinginevyo. Sisemi haya kutetea mambo ya mafuta na maji ya upako, hasha. Nasema kwa sababu naona suala hili linachukua mkondo wa kidunia zaidi, kumpima Mungu kwa elimu ya kidunia wakati kumbe elimi ya Mungu wala haichangamani na hiyo.

4. Je, vifo vimesababishwa na usimamizi mbovu?
Nadhani hapa ndipo penye tatizo. Kilichotokea ni wazi kuwa ni usimamizi mbovu, ama uzembe kwenye kusimamia uendeshaji wa tukio la kukanyaga mafuta. Habari ya kwa nini watu wanaamini katika mafuta haina uhusiano hata kidogo na vifo hivyo. Ni sawa na kuhoji kwa nini watu wanaamini katika mkate na divai, ama katika kuchoma udi n.k. Tatizo liko kwenye utaratibu wa waamini kukipata kile wanachokiaminia.

Mambo ya kiimani yanabaki kuwa juu ya mhusika mwenyewe, hivyo ni ujinga kumwona anayeamininhayo kuwa mjinga. Nikutafuta kuwaingizia wengine imani yako kwa lazima, hivyo kuondoa maana ya uhuru wa kuabudu bila kuvunja sheria. Kama sheria imevunjwa, sio sheria ya kukanyaga mafuta bali sheria ya kushindwa kusimamia kusanyiko kwa usalama.

Hivyo basi hoja yangu imelenga kuonyesha kuwa sio sahihi kuanza kushambulia imani ya watu kwa vigezo vya nini sisi wengine tunakiamini, bali yatupasa kuwafundisha uzuri wa imani zetu na ubaya wa imani yao ili waamini habari zetu waachane na hayo yao.

Ni makosa makubwa kuwaaminisha wau kuwa tukio la mwamposa inashabihiana na lile la Kibwetee wa Uganda. Hii ni namna ya kutafuta kushambulia imani nyingine kwa mgongo wa nyuma na ndipo hoja za wenye imani tofauti zilipojikita. Mpaka sasa sielewi ni kwa vipi tukio la Moshi limefanana na lile la Kibwetere. Ni uongo na uzushi mkubwa wa wenye kuishambulia imani.

Nawasihi utafakari kwa kina tatizo lilipo, tuachane na mihemkoa bali tuwe wakweli kwani kweli itatuweka huru.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Najua neno moja tu; Kwa jina la YESU, pepo wanatoka, vilema wanatembea, vipofu wanaona etc.......Yote yamethibitishwa na neno la MUNGU. Sio kwa jina lingine liwalo lolote. Hebu fuatilia mahubiri ya watumishi wa Mungu wakati wa uzinduzi wa jukwaa la JKK pale BCC Mbezi kwa Askofu Gwamanya
 
Back
Top Bottom