Yaweza kuwa vyombo vya mafuta na pia walitarajia utaratibu wa kupanga mstari lakini watu wakavamia kila mmoja anataka awe wa kwanza. Tuliza kichwa mkuu.
Kibwetere alikuwa na mahubiri na mafundisho tofauti sana mkuu, ndio maana nikahoji, kuna tatizo gani kwenye hayo mafundisho ya Mwamposa in relation to the incidence? Hoja iko hapo, mihemko pembeni. Ya kibwetere hata teolojia yake haikuwa salama kwa wanadamu, sasa teolojia ya Mwamposa ina tatizo gani kiusalama? Tuache chuki binafsi.
Mimi ni mpingaji namba moja wa teolojia. Hii ni elimu ya kum-define Mungu kwa mtazamo wa mtu ama kikundi cha watu. Huko ndiko huzaliwa viu kama statement of faith. Ni mambo haya yabteolojia yaliyoingiza imani potofu kwenye kanisa, ibada ambazo hazina sapoti ya biblia. Kumbe basi natazama Neno la Mungu zaidi kuliko kusikiliza mwana teolojia amesema nini.
Ni wapi imeandikwa mafuta ni matakatifu? Mafuta yatabaki mafuta tu, ila kwa imani watu huamini kilichonenwa juu ya mafuta hayo kitawapa matokeo. Kumwaga chini? Hapa sijakuelewa mkuu, mafuta huwekwa kwenye vyombo ili watu wakanyage, miguu ikiwa sehemu ya mwili.
Nachelea kuongea sana kwa sababu mimi pia siamini katika mafuta ila najenga tu hoja kwamba watu wanamhukumu Mwamposa kwa kufuata hisia binafsi juu ya huduma yake. Hakuna sehemu kwenye biblia inaposema ukimwaga mafuta mwenye vyombo watu wakanyage ni dharau.
Yesu aliponya kwa mate, nadhani ungekuwepo enzi hizo ungempiga mawe. Tatizo lako unadhani Mungu anaangalia heshima za nje ambazo kimsingi ni unafiki mkubwa, Mungu anaangalia ROHO YAKO. Hili ndilo lilipelekea Mungu kuwekwa kwenye vyombo makanisani pia, akatunzwa sakaristia. Matokeo yake wengine kama kina Bulldozer wamemweka kwenye mafuta, kwa nini basi uwanyooshee kidole?
Elimu itakupa maarifa ni kweli, lakaini maarifa ya dunia hii. Elimu ya Mungu itakupa ujuzi wa ufalme wa mbinguni. Hakuna chuo cha teolojia kina uwezo wa kufundisha hili zaidi ya mashindano ya doctrines kwamba kwa nini sisi tunaamini hivi na wao wanaamini vile.
Kumbuka tangu kale na HATA SASA Mungu alivichagua vitu vinyonge na vidhaifu ili kuviaibisha vikubwa na vyenye nguvu. Unaielewa hiyo?
Kama maprofesa wanakwenda kunywa kikombe cha babu, ama kukanyaga mafuta ya upako, yako wapi maarifa hayo unayosema? Elimu ya Mungu itabaki kuwa hivyo na ya dunia kadhalika.
Kuhusu kuzika vitu vitakatifu, Mungu wa leo hakai kwenye vitu bali akaa kwenye roho zao wamtafutao kwa bidii. Habari za ukigusa hostia utapatwa kichaa sio biblical bali ni mafundisho ya kibinadamu. Tusimshushe Mungu wetu hivyo, tumheshimu kama alivyotaka. Ndio maana leo hii hatuendi kuhiji Israeli kwa sababu hakuna tena ya kuabudu mlima huu wa ule.
Tusome biblia.
Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Mkuu inaonekana unasoma biblia na ukikutana na mtu ambaye unamzidi ufahamu wa Neno la Mungu atakubaliana na wewe,nimesomapost zako kuna maeneo uko sahihi na kuna maeneo hauko sahihi.
Unajua njia inayotumiwa na watumishi feki?Wewe unategemea wafundishe kinyume na biblia mwanzo mwisho?Watu hawa hufundisha kweli kwa sehemu na uongo kwa sehemu.Wanalitumia Neno la Mungu vibaya,mtumishi mmoja kutoka Mwanza analinganisha issue ya watu kufa na Ayubu kufiwa na watoto wake na mali zake.Mfano wake hauendani kabisa,Ayubu kama mtumishi wa Mungu alifiwa na wanawe wa damu yake na alipoteza mali zake, huko Kilimanjaro Mwamposa hajafiwa na watoto wake wa damu wala hajapoteza mali zake.Kwa hiyo kulinganisha majaribu ya Ayubu na hili la Mwamposa si sahihi.Kwa hiyo mtumishi wa Mwanza aliyelinganisha Ayubu na hayo ya kilimanjaro hajalitumia Neno la Mungu kwa usahihi.
Je unajua kama shetani muda mwingine huwa anasema ukweli?Ingawa ukichunguza unakuta anarudia kile ambacho Mungu amekwisha kukisema?
Matumizi ya mafuta kwenye biblia ni tofauti kabisa na yanavyotumiwa leo,kama watumiaji wa mafuta wanatumia biblia kusuport hili,ukisoma biblia utaona wanapingana nayo kwa jinsi ambavyo mafuta yalitumika.Na kwa sababu Mungu mwenyewe alituambia
1Yohana4:1 "Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. "
Sasa utachunguzaje roho?Hakuna njia nyingine zaidi ya kutumia Neno la Mungu,ndiyo maana maandiko yanasema katika kitabu cha
Wakolosai 3:16-17 "Neno la Kristo lidumu ndani yenu kwa wingi, mki fundisha na na kuonyana katika hekima yote; na huku mkiimba zab uri, nyimbo na tenzi za rohoni na mkiwa na shukrani kwa Mungu mioyoni mwenu. 17 Na lo lote mtakalofanya, ikiwa kwa neno au kwa tendo,
fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kupitia kwake "kwa bahati mbaya wengi wa wanaojiita wakristo wa leo hawasomi biblia matokeo yake wanakuwa "ni watoto wachanga kiroho hivyo wanayumbishwa na mafundisho potofu".Hapo "fanyeni yote katika jina la Bwana",leo watu wanafanya kwa jina la mafuta,chumvi,vitambaa na mengine mengi yatakuja.
Kwa nini hawa watu watakuwepo duniani na hawataweza kuzuiwa?Jibu ni rahisi mitume na manabii wa uongo watakuwepo duniani kwa sasabu kinywa cha Bwana kimenena hayo.Mungu mwenyewe alisema siku za mwisho kutakuwepo na mitume na manabii wa uongo.Neno la Mungu ni lazima litimie na hakuna wa kulizuia.Ila muda wao ukiisha hawataweza na haya ni maandalizi ya mpinga kristo,kumbuka yeye pia atakuwa na uwezo wa kufanya miujiza mikubwa.Si kila muujiza unatoka kwa Mungu.kwa hiyo kwa anayemjua Mungu wa kweli vita vyetu ni vya rohoni serikali ya nchi yeyote inaweza fanya kuwaondoa au kuwazuia hiyo itakuwa ni jitihada za mwilini na zinaweza zisifanikiwe au zikifanikiwa zitaleta madhala mengine katika jamii husika.
Nini cha kufanya?Tatizo siyo watumishi feki,suala la imani ni la mtu na Mungu wake,kiongozi kama mchungaji,padri,mtume au nabii wa kweli kazi yake ni kukuongoza wewe,hii haimanishi wewe usifanye bidii kujifunza Neno la Mungu.
Mathayo 7:13-14 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. Point yangu kwenye hili andiko ni kwamba yeyote anayejiita mkristo analojukumu la kufanya ili kuurithi ufalme wa mbinguni,anatakiwa asome Neno,adumu katika maombi,kitu kingine hawa jamaa ambao ni mbwa mwitu ndani ya ngozi ya kondoo waliojaa kote duniani wanapenda kuwaombea sana watu wao kuliko kuwafundisha wao kuomba.Yesu alisema ombeni mtapewa,tafuteni mtapata,bisheni hodi mtafunguliwa,hakusema watu wengine waombe kwa ajili yenu.Hii haimanishi kuombewa ni kosa kibiblia,kuna muda wa kumwombea mtu na kuna muda wa kumwacha aombe mwenyewe.Ukiona wewe unaombewa tu ,hufundishwi ukiwa na shida umtafute Mungu wewe mwenyewe mpaka uende kwa huyo kiongozi wako hapo pana shida.Mtoto hufundishwa jambo fulani akianza kulijua huachwa afanye mwenyewe.
Ukisoma biblia Elisha alipokea nguvu mara mbili kutoka kwa Eliya,mambo ya Mungu kuna kurithishana au kumwekea mtu mkono ili sehemu ya Roho inayofanya kazi kwako ifanye kazi kwake,utaona hata Mungu alimwambia Mussa atafute wasaidizi awawekee mikono.Hapa nataka tujifunze kitu
Kila mtumishi wa Mungu unayemfahamu lazima ana mzazi wake aliyemlea au kumfundisha huduma au kumwekea mikono kwa ajili ya huduma hiyo.
Swali langu kwako na kwa watanzani,haya watumishi wanaotumia mafuta,chumvi na vitu vingine vya upako baba zao wa kiroho tunaweza wajua?Je baba zao wanatumia hivi vitu?Kwa wale wanaofuatilia lilipoanzishwa jukwaa la injnili mitume na manabii walikutana wakajadili mambo yao fulani.Kiongozi wao akawaambia "msibishane nao kwenye mitandao".Lakini tujiulize injili ya kweli ya Mungu hukubalika kila sehmu,kama injili yako kuna sehemu wanaikataa maana yake ina shida,kama tunasema Roho atendaye kazi ni yule yule iweje huyu Roho kama ni yule yule ampe amani mtumishi "A" kwenye suala la vitu vya upako na amkoseshe amani mtumishi "B"?Roho wa Mungu hapingani,kama njia yako kuna watu inawachefua unatakiwa kuiangalia.Sasa kuokoa muda kuna mengi yakonyuma ya pazia ambayo wengi hawayajui,lakini ukinyenyekea kwa Mungu na kusoma Neno lake utaijua kweli nayo kweli itakuweka huru.
Ushauri wangu kwa unayesoma post hii:Shetani hajalala,amegundua kwa kuja kwa njia ya dini amewapata wengi kuliko kwa wachawi na waganga wa kienyeji,ni jukumu lako wewe binafsi kusoma biblia,kufanya maombi,kusikiliza mafundisho ya viongozi wako ila kama kuna sehemu yanapingana na Neno la Mungu omba ushauri kwa wakubwa katika mambo ya imani.
Haya mambo ni lazima yatimie ila ni kazi yetu kuwafundisha watu na kuwaonya wawe makini na hizi imani kama ambavyo maandiko yamesema "msiziamini kila Roho bali mzichunguze kama zinatoka kwa Mungu".
Kwa wale mnaowalaumu polisi Mungu aseme nanyi,kwenye mambo ya imani Mungu ndiye hulinda kwanza,polisi hawezi kupambana na roho za kuzimu ambazo hawezi kuziona.
Je kuna mtumishi katika mikutano yake alikuwa na watu wengi kama Reinhard Bonnke?Je ulishawahi kusikia watu wamekanyagana wakafa?Hii ni home work,muda mwingine Mungu huongea na watu lakini watu hushindwa kuielewa sauti yake.Mwenye masikio na asikie.
Roho ya mwanadamu ni ya thamani sana kuliko mali zote za dunia hii,tusicheze na maisha ya watu.
Wito kwa waletunaojii wakristo wa kweli
:Kuna sehemu hatujasimama vyema katika zamu zetu,naamini unajua kama kanisa likisimama vyema katika nafasi yake nini hutokea.Kanisa Amka ukayatende uliyoagizwa na Bwana.
NB:Tukumbuke kuliombea taifa letu huu ni mwaka wa uchaguzi,Mungu atusaidie tuvuke salama,anza leo kuombea uchaguzi usisubilie ufike ndiyo uanze.Kwa kuwa kila mamlaka inatoka kwa Mungu,Mungu atupatie viongozi ambao yeye amekusudia waiongoze nchi yetu katika kipindi hiki.
Je unahitaji kumpokea Yesu leo?Njoo inbox nikueleze yakupasayo kutenda,kuna jambo unataka kujua njoo inbox.