Prophet -a person regarded as an inspired teacher or proclaimer of the will of God.
awali ya yote ; imekuwaje Nabii Mwamposya asipewe ishara na Mwenyezi Mungu kwamba haya yatatokea...?
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio bila basi wewe...bila kuwaambia abiria wafunge mikanda. Mikutano mingapi inafanyika salama?Bila basi watu wangekufa? Hiyo logic haijakaa sawa. Bila boti watu wangezama? Flawed logic
Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Yote imekuwa dummy, uzushi wa mageti kufungwa umeshajibiwa.FACT: Mkutano wa injili ulikuwa ni wa Mwamposa
FACT: Watu walimiminika kwa wingi lengo ni kuhudhuria ibada hiyo ya Mwamposa
FACT: Kibali kilitolewa na mwisho wa kibali ilikuwa saa kumi na mbili jioni
FACT: Kulikuwa na zoezi la kukanyaga mafuta ambaye mwanzilishi wake ni Mwamposa
FACT: Zoezi lilifanyika baada ya muda wa kibali kwisha
FACT: Milango mingine saba ya kutokea ilifungwa na kutumika mmoja tu uliowekwa turubai lililomwagiwa mafuta
FACT: Mafuta juu ya turubai na mwendo wa binadamu upo uwezekano mkubwa wa kula mwereka juu ya turubai
FACT: Wenye matatizo ni wengi wanaotafuta kutatua kwa njia ya muujiza
FACT: Kukukosa kukanyaga mafuta kwenye ibada ya kukanyaga mafuta ni kama ukufika kwenye ibada
FACT: Walioaminishwa hilo nilazima watakwenda kwenye zoezi hilo la kukanyaga mafuta
FACT: Waamini hao walikanyagana na kukosekana kwa mwanga, zoezi la kukanyagana liliendelea kwa muda mrefu
FACT: Watu ishirini wamefariki dunia, watoto wawili, mwanaume mmoja na waliobaki ni akina mama
FACT: Kumi na sita ni majeruhi
FACT: Mwamposa alitafutwa baada ya tukio, vizuizi viliwekwa, vizuizi alivikwepa, alikamatwa mji mwngine kabisa mbali na eneo la tukio (alikamatwa hakwenda mwenyewe kituoni)
FACT: Uchunguzi unaendelea
FACT: Mwamposa yupo ndani anaisaidia polisi
Speculation: Wataalamu wa mambo ya sheria huyu atakaa ndani kwa muda gani mpaka kesi yake itakapokuwa na uwezo wa kupewa dhamana? miezi sita? Mwaka? miaka miwili? zaidi ya miaka miwili?
Iman ya katoliki sio iman ya bibilia so kila mtu haeshimu imani yakeUwanja unabeba watu 10,000 na una mageti 8 unaweza kuniambia sababu zilizomfanya afungue geti moja pekee
Kwa hali why tusilifananishe na tukio la kibwetere la Uganda
Then umezungumzia kuhusu theology unajua elimu hii inasema nini kuhusu huu uongo wa hawa wanajiita mitume na manabii?
Unapozungumzia mafuta mafuta kile kitu ni sacred ni kitakatifu kama kitu ni kitakatifu unaweza kukimwaga chini chini ili watu wakanyage?.....unajua tafsiri ya kukanyaga kitu ni ishara ya dharau na kukikosea kitu thamani
Alafu unatuaminisha mafuta ya upako kitu kitakatifu kinatunzwa na kama wangekuwa kweli wanaelewa wasingekikosea heshima hivi.....sababu hii ilitosha kabisa kuona huyu ni MUONGO na TAPELI
Kwa kanisa katoliki mafuta matakatifu ya Krisma yanatumika mwaka mzima yanayobaki HUZIKWA kwa heshima maana ni kitu kitakatifu
Tusitetee uongo elimu haitoshi tu kutuondolea ujinga pia itongezee maarifa
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu inaonekana unasoma biblia na ukikutana na mtu ambaye unamzidi ufahamu wa Neno la Mungu atakubaliana na wewe,nimesomapost zako kuna maeneo uko sahihi na kuna maeneo hauko sahihi.
Unajua njia inayotumiwa na watumishi feki?Wewe unategemea wafundishe kinyume na biblia mwanzo mwisho?Watu hawa hufundisha kweli kwa sehemu na uongo kwa sehemu.Wanalitumia Neno la Mungu vibaya,mtumishi mmoja kutoka Mwanza analinganisha issue ya watu kufa na Ayubu kufiwa na watoto wake na mali zake.Mfano wake hauendani kabisa,Ayubu kama mtumishi wa Mungu alifiwa na wanawe wa damu yake na alipoteza mali zake, huko Kilimanjaro Mwamposa hajafiwa na watoto wake wa damu wala hajapoteza mali zake.Kwa hiyo kulinganisha majaribu ya Ayubu na hili la Mwamposa si sahihi.Kwa hiyo mtumishi wa Mwanza aliyelinganisha Ayubu na hayo ya kilimanjaro hajalitumia Neno la Mungu kwa usahihi.
Juwa anasema ukweli?Ingawa ukichunguza unakuta anarudia kile ambacho Mungu amekwisha kukisema?
Matumizi ya mafuta kwenye biblia ni tofauti kabisa na yanavyotumiwa leo,kama watumiaji wa mafuta wanatumia biblia kusuport hili,ukisoma biblia utaona wanapingana nayo kwa jinsi ambavyo mafuta yalitumika.Na kwa sababu Mungu mwenyewe alituambia 1Yohana4:1 "Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. "
Sasa utachunguzaje roho?Hakuna njia nyingine zaidi ya kutumia Neno la Mungu,ndiyo maana maandiko yanasema katika kitabu cha Wakolosai 3:16-17 "Neno la Kristo lidumu ndani yenu kwa wingi, mki fundisha na na kuonyana katika hekima yote; na huku mkiimba zab uri, nyimbo na tenzi za rohoni na mkiwa na shukrani kwa Mungu mioyoni mwenu. 17 Na lo lote mtakalofanya, ikiwa kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kupitia kwake "kwa bahati mbaya wengi wa wanaojiita wakristo wa leo hawasomi biblia matokeo yake wanakuwa "ni watoto wachanga kiroho hivyo wanayumbishwa na mafundisho potofu".Hapo "fanyeni yote katika jina la Bwana",leo watu wanafanya kwa jina la mafuta,chumvi,vitambaa na mengine mengi yatakuja.
Kwa nini hawa watu watakuwepo duniani na hawataweza kuzuiwa?Jibu ni rahisi mitume na manabii wa uongo watakuwepo duniani kwa sasabu kinywa cha Bwana kimenena hayo.Mungu mwenyewe alisema siku za mwisho kutakuwepo na mitume na manabii wa uongo.Neno la Mungu ni lazima litimie na hakuna wa kulizuia.Ila muda wao ukiisha hawataweza na haya ni maandalizi ya mpinga kristo,kumbuka yeye pia atakuwa na uwezo wa kufanya miujiza mikubwa.Si kila muujiza unatoka kwa Mungu.kwa hiyo kwa anayemjua Mungu wa kweli vita vyetu ni vya rohoni serikali ya nchi yeyote inaweza fanya kuwaondoa au kuwazuia hiyo itakuwa ni jitihada za mwilini na zinaweza zisifanikiwe au zikifanikiwa zitaleta madhala mengine katika jamii husika.
Nini cha kufanya?Tatizo siyo watumishi feki,suala la imani ni la mtu na Mungu wake,kiongozi kama mchungaji,padri,mtume au nabii wa kweli kazi yake ni kukuongoza wewe,hii haimanishi wewe usifanye bidii kujifunza Neno la Mungu.Mathayo 7:13-14 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. Point yangu kwenye hili andiko ni kwamba yeyote anayejiita mkristo analojukumu la kufanya ili kuurithi ufalme wa mbinguni,anatakiwa asome Neno,adumu katika maombi,kitu kingine hawa jamaa ambao ni mbwa mwitu ndani ya ngozi ya kondoo waliojaa kote duniani wanapenda kuwaombea sana watu wao kuliko kuwafundisha wao kuomba.Yesu alisema ombeni mtapewa,tafuteni mtapata,bisheni hodi mtafunguliwa,hakusema watu wengine waombe kwa ajili yenu.Hii haimanishi kuombewa ni kosa kibiblia,kuna muda wa kumwombea mtu na kuna muda wa kumwacha aombe mwenyewe.Ukiona wewe unaombewa tu ,hufundishwi ukiwa na shida umtafute Mungu wewe mwenyewe mpaka uende kwa huyo kiongozi wako hapo pana shida.Mtoto hufundishwa jambo fulani akianza kulijua huachwa afanye mwenyewe.
Ukisoma biblia Elisha alipokea nguvu mara mbili kutoka kwa Eliya,mambo ya Mungu kuna kurithishana au kumwekea mtu mkono ili sehemu ya Roho inayofanya kazi kwako ifanye kazi kwake,utaona hata Mungu alimwambia Mussa atafute wasaidizi awawekee mikono.Hapa nataka tujifunze kitu
Kila mtumishi wa Mungu unayemfahamu lazima ana mzazi wake aliyemlea au kumfundisha huduma au kumwekea mikono kwa ajili ya huduma hiyo.
Swali langu kwako na kwa watanzani,haya watumishi wanaotumia mafuta,chumvi na vitu vingine vya upako baba zao wa kiroho tunaweza wajua?Je baba zao wanatumia hivi vitu?Kwa wale wanaofuatilia lilipoanzishwa jukwaa la injnili mitume na manabii walikutana wakajadili mambo yao fulani.Kiongozi wao akawaambia "msibishane nao kwenye mitandao".Lakini tujiulize injili ya kweli ya Mungu hukubalika kila sehmu,kama injili yako kuna sehemu wanaikataa maana yake ina shida,kama tunasema Roho atendaye kazi ni yule yule iweje huyu Roho kama ni yule yule ampe amani mtumishi "A" kwenye suala la vitu vya upako na amkoseshe amani mtumishi "B"?Roho wa Mungu hapingani,kama njia yako kuna watu inawachefua unatakiwa kuiangalia.Sasa kuokoa muda kuna mengi yakonyuma ya pazia ambayo wengi hawayajui,lakini ukinyenyekea kwa Mungu na kusoma Neno lake utaijua kweli nayo kweli itakuweka huru.
Ushauri wangu kwa unayesoma post hii:Shetani hajalala,amegundua kwa kuja kwa njia ya dini amewapata wengi kuliko kwa wachawi na waganga wa kienyeji,ni jukumu lako wewe binafsi kusoma biblia,kufanya maombi,kusikiliza mafundisho ya viongozi wako ila kama kuna sehemu yanapingana na Neno la Mungu omba ushauri kwa wakubwa katika mambo ya imani.
Haya mambo ni lazima yatimie ila ni kazi yetu kuwafundisha watu na kuwaonya wawe makini na hizi imani kama ambavyo maandiko yamesema "msiziamini kila Roho bali mzichunguze kama zinatoka kwa Mungu".
Kwa wale mnaowalaumu polisi Mungu aseme nanyi,kwenye mambo ya imani Mungu ndiye hulinda kwanza,polisi hawezi kupambana na roho za kuzimu ambazo hawezi kuziona.
Je kuna mtumishi katika mikutano yake alikuwa na watu wengi kama Reinhard Bonnke?Je ulishawahi kusikia watu wamekanyagana wakafa?Hii ni home work,muda mwingine Mungu huongea na watu lakini watu hushindwa kuielewa sauti yake.Mwenye masikio na asikie.
Roho ya mwanadamu ni ya thamani sana kuliko mali zote za dunia hii,tusicheze na maisha ya watu.
Wito kwa waletunaojii wakristo wa kweli:Kuna sehemu hatujasimama vyema katika zamu zetu,naamini unajua kama kanisa likisimama vyema katika nafasi yake nini hutokea.Kanisa Amka ukayatende uliyoagizwa na Bwana.
NB:Tukumbuke kuliombea taifa letu huu ni mwaka wa uchaguzi,Mungu atusaidie tuvuke salama,anza leo kuombea uchaguzi usisubilie ufike ndiyo uanze.Kwa kuwa kila mamlaka inatoka kwa Mungu,Mungu atupatie viongozi ambao yeye amekusudia waiongoze nchi yetu katika kipindi hiki.
Je unahitaji kumpokea Yesu leo?Njoo inbox nikueleze yakupasayo kutenda,kuna jambo unataka kujua njoo inbox.
Hujanielewa vizuri, mimi sio wa injili nyepesi. Naishi kwenye neno mkuu, hayo mahubiri ni chakula kwenu usiosoma maandiko. Nje ya hapo elewa maana ya bandiko hili, sikuweka hili bandiko kuhubiri imani ipi ni sahihi. Lengo ni kuonyesha chanzo cha tatizo kwamba sio mafuta, basi.Umetumia muda wako wenye thamani kutengeneza bandiko rejea bila mzuka kama mm.
Asipoelewa hapa ni basi!!
Umeshasema WANAPOSEMA!! Unaelewa maana ya imani?? Maswali yako ni very basic ndio maana nilikujibu kirahisi tuKwa hiyo hao mitume wako huwa wanawadanganya wanaposema hapa kuna uwepo wa Mungu siyo!,maana apimae ni Mungu na wao siyo Mungu
Sent using Jamii Forums mobile app
Huo wa Bonnke nimeshajibu, ni mojawapo ya mifano duni mno. Nani hajui kikutano ya Bonnke ilikuwa ikilindwa na dola? Kwa nini polisi hawakuwepo hapo kwa Mwamposa?Sio bila basi wewe...bila kuwaambia abiria wafunge mikanda. Mikutano mingapi inafanyika salama?
Umepewa mpaka mfano wa Bonke. Labda husomi wanachokujibu!!!!
Umejibu vyema sana tena sana! Ubarikiwe mno.Ni kweli, majaribu ya Mwamposa yaweza yasiwe majaribu pia. Kwa ujumla ibada yabkuabudu mafuta siikubali kabisa, ila niliona watu wenye misimamo mibaya wakijarinbu kutumia tukio hilo kuukashifu ukristo ama wokovu kwa ujumla.
Ninachosema ni kuww pamoja na watu kufatiki,sio jukumu la serikali kupima maandiko na kuamua kipi ni sahihi. Ndio maana nikaandika haya kupinga tamko la waziri na baadhi wa watu waliohojiwa kwenye vyombo vya habari kutaka kuhalialisha jambo hili. Ni kweli kwa upande wa kiimani siamininkama biblia imeagiza hayo, kwani hakuna maandiko, bali kiserikali pia wako ambao hawakuwajibika.
Naam, hapo nadhani tunajadili mambo ya kiimani zaidi ambayo hakuna waziri anaweza kuingia. Kusema vibanda kanisa ni kuutukana ukristo, waziri alipaswa kuongelea sababu za vifo. Kama mafuta yaliua baada ya kuyakanyaga hilo ni tatizo na mkemia alipaswa kuhusika. Lakini tukio halikuwa hivyo, ni uzembe. Kumbe basi mimi siongelei UHALALI wa Mwamposa kutumia mafuta kwenye ibada zake, bali mazingira ya vifo. Nadhani umenielewa.
Unalijua Jina la Bwana? Umesema sawa, yote yafanyike kwa jina hilo. Hata wanaotoa mafuta watasema hufanya hayo kwa Jina la Bwana, hivyo hatuna haki ya kuwashambulia. Unasemaje hapa?
Sasa hapa umekuja kwenye kusudi la mada hii, kwamba serikali haina uwezo kuwachagulia watu kwamba huyu ni Mungu sahihi na huyu sio. Ni kwamba mambo hayo ni ya rohoni kwa kadri mtu mwenyewe anavyoamini.
Ni sawa, nyakati za mwisho haya yote yatatukia. Ndio maana huwa siogopi kwa sababu tu kuna manabii wengi wanachipuka kila leo, hili lipo ili maandiko yatimie. Pia kumbuka NJIA NI NYEMBAMBA NA NI WACHACHE WANAOIONA. Usitishwe na wmakunndi makubwa makubwa kwa sababu wokovu ni uhusiano binafsi na Mungu wala si kitu cha jumuiya.
Hapa napo pana tatizo. Hawa wazazi wa kiroho wa sasa kila mmoja ana doctrine yake, wengi wamekengeuka na kuchanganya injili na matakwa yao. Ndio maana kuna makanisa mengi kwa sababu ya tofauti ndogo ndogo na kubwa.
Ni nani mzazi wa kweli? Hili linahitaji mjadala, lakini hakuna jambo jema kama kudumu katika Neno. Wengi wetu hatujuinkwamba tumepewa agizo la KUIHUBIRI INJILI ULIMWENGUNI KOTE. Hapa hakuna pastor, mwinjilisti, padre n.k. ni waamini wote tumetakiwa kuhubiri. Kwa kufanya hivyo tutaepuka kuwa wakristo wa jumapili na hivyo kulishwa matangopori.
Mfano wa TALANTA unahusika hapa. Aliyepewa tano huyo ndio ana vipawa mbalimbali. Yesu atakaporudi atamdai zaidi. Mwenye mbili naye alipewa kiasi fulani akazalisha. Huyu naye Bwana atakaporudi atamdai matunda yake. Mwenye moja ndio wengi wetu tuko hapo. Tunadhani kuhubiri injili ni mpaka uwe na uwezo wa kutabiri, kufufua wafu, kutenda miujiza n.k. Siku Bwana atakaporudi atatudai hiyo talanta moja aliyotupa (neno la maarifa) ambayo kila mmoja wetu aliyeamini anapaswa kuwa nayo kupitia maandiko. Wengi wetu bila kujua tutakuwa tumemjibu Bwana kwamba ni mwenye roho ngumu, anakusanya asipotawanya. Kwamba alitupa kitu kimoja tu, NENO, nasi tukaamua tutalizika ardhini kumsubiri arudi. Why? Na sisi tulitaka tuwe na uwezo wa kuzuia mvua kama nabii Elisha, ama kuponya wagonjwa kwa kivuli kama Petro. Bila hayo tunajiona hatuna uwezo wa kuhubiri injili, japo kwenye maeneo yetu ya kazi, ama kwa jamaa zetu tunaowasiliana nao kila siku.
Baba wa kiroho: eneo hili ndilo linatumika kueneza doctrine mbalimbali kwa mujibu wa tafsiri za watu. Hakuna baba bora kama Roho mtakatifu. Nawashauri wakristo mjizoeshe na kujibidiisha kusoma maandiko, sio kujaza notisi za sunday school pekee. Chunguzeni maandiko kwani humo ndimo mlimo chemichemi ya uzima. Msibebwe na mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu. Nakupa mifano michache tu kwa hiki unachokipigania:
1. JKK inaundwa na Askofu Gamanywa, Askofu Kakobe na Mtume Fernandes. Kila mmoja ana mambo ambayo anatofautiana kiimani na mwingine. Je, tukiwapeleka waumini wa Gwajima kwa Kakobe watapokea mafumdisho sawa?
2. Je, unadhani kuvaa jeans kwa Gamanywa ni dhambi? Vipi kwa Kakobe?
3. Unasemaje kuhusu uvaaji wa mawigi, kwa Fernandes ni dhambi kama ilivyo kwa Kakobe?
Nimekupa mifano michache tu uone nguvu ya mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu. Hawa JKK wanaweza kujionyesha wenye nia njema, lakini kwanza kabisa iliwapasa kukaa pamoja na kuyachunguza mqandiko ili kumaliza tofauti zao, sio tu kuungana kwa sababu ya ibada ya mafuta na vitambaa vya upako. Yapo mambo mengi tu ya msingi wameyaacha na kuelekeza nguvu zao kwenye eneo moja tu.
Wengi mnamtafuta shetani nje ya kanisa, ni upofu mliopewa. Shetani hapati taabu juu ya walio nje ya Kristo kwa sababu hao ni wake. Mashambulizi yake yataelekezwa NDANI YA KANISA ndio maana atawadanganya yumkini hata waamini. Ni makosa makubwa kumsaka shetani nje ya kanisa kwani huko yupo wazi tu, vita kubwa kwa wakristo itatoka ndani ya kanisa, ndio maana tumeonywa mbele tuwe makini na chukizo la uharibifu ambalo litaikamata MADHABAHU.
Usihukumu mkuu, kwani huna uhakika kama Bonnke alikuwa kweli na Roho wa Mungu. Sisi tunahukumu kwa nje, Mungu anahukumu kwa ndani. Hata hilo la Mwamposa wala sio lazima iwe utakavyo. Halafu lazima uheshimu nafasi ya polisi kikatiba, kwani imetupasa kutii mamlaka. Wakati mwingine Mungu hupitia kwenye utendaji wa watumishi hawa ili kuokoa nafsi za watu. Ni makosa kudhani Mungu atasimama kukulinda hata pale alipobariki taratibu za dunia. Imeandikwa usimjaribu Bwana Mungu wako. Kama una njaa pika ule, sio uingie kuomba. Kama kunamajambazi wamefunga njia na umejua mapema badili njia. Usijidanganye eti una Mungu hivyo utapita tu, Mungu hadhihakiwi. Ndipo na hapa utaratibu wa ulinzi wa mikutano upo, Mungu amebariki hilo. Sasa yanapotokea majanga kwa sababunya uzembe wetu hutafuta wa kumshutumu. Mungu ni mwenye haki.
AMINA
Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
AminaUmejibu vyema sana tena sana! Ubarikiwe mno.
Maana nami kuna jambo nimejifunza kupitia hiki ulichokijibu hapa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Umeshasema WANAPOSEMA!! Unaelewa maana ya imani?? Maswali yako ni very basic ndio maana nilikujibu kirahisi tu
Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Umesahau BABU wa LOLIONDO na kikombe cha plastic na maji taka; ni Mlutheri yule. Hatumfahamu Mungu kwa madigirii/PHD etc.; wasingekuwa walevi, wavuta sigara wazinzi, wapigadili wa kawaida dhambi lukuki. Neno la Mungu ni ROHO na linatambulikana kwa ROHO mtakatifu sio kwenda shule za kidunia. Yako makanisa yanayofundisha kweli yote ya biblia na Mcchungaji anajua kusoma na kuandika tu. Hawa wamepita chuo gani?; Mwakasege, Mzee Kulola(RIP)Degrees in theology or further is the solution
For instance Catholic,Lutheran and Adventist clergies are well trained in theology...u never hear this kind of drama in RC,Lutheran or even Muslims
Kilichofanyika kwenye ibada ya mwamposa,ni ushetani tu,hata utetee vp,hata wakatoriki tuna utaratibu wa kula mikate,na divai lakini hatukanyagani,na kuuana kama mang'ombe,kushiriki meza ya bwana,kama tunavyoita,ni utaratibu uliowekwa wazi,kwa kila muumini,Nimekuwa nikitafakari kile kinachoendelea kufuatia tukio la vifo vya watu 20 vilivyotokea huko Moshi kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa "Bulldozer." Baada ya tukio hilo kumekuwa na maoni mengi na mitazamo tofauti kwa ujumla kutokana na jinsi ukio hilo lilivyotokea, nami nimeona nitoe mtazamo wangu juu ya jambo hili.
Chanzo cha vifo ni kipi hasa?
Hapa nimeona nichambue kwa kina tatizo hasa ni nini. Kumekuwa na mitazamo hasi kuhusiana na chanzo hasa cha vifo kiasi kwamba kumekuww na hasira kali juu ya imani ya baadhi ya watu.
1. Je vifo vimetokana na mafuta?
Ukitafakari kwa kina utaona hili si kweli. Mafuta hayakusababisha hivyo vifo kwa sababu hayuko hata mmoja aliyetumia mafuta hayo na kufariki. Mafuta hayo yamekuwa yakikanyagwa mara nyingi, kwa miaka mingi pasipo kuwa na madhara kwa watumiaji.
2. Je vifo vimesababishwa na mafundisho?
Ni muhimu kupima mafundisho kama ndio chanzo hasa cha vifo hivi. Kwamba kile kilichohubiriwa siku hiyo ndicho kilichopelekea watu kukanyagana hata vifo kutokea. Kama siku hiyo waliambiwa watakuokuwa wa kwanza kukanyaga mafuta watapokea upako kiasi cha kuwalazimu waamini kugombania nafasi ya kwanza basi hilo ni tatizo. Lakini kama fundisho lilikuwa ni kwamba kukanyaga mafuta tu ni kupokea baraka, basi haijalishi kama ni wa kwanza ama ni wa mwisho.
3. Je vifo vimesababishwa na mafundisho potofu?
Hili ni suala pana kwa sababu limelenga mambo ya kiimani. Nilishangaa jana pale nilipomsikiliza waziri Simbachawene akielezea jinsi ambavyo huwa anaangalia baadhi ya mafundisho na kujiuliza kama kuna Mungu pale. Siamini kama ni jukumu la waziri kupima wapi pana Mungu wa kweli na wapi hapana Mungu.
Mwenye jukumu la kupima usahihi wa mafundisho ni nani hasa linapokuja suala la imani? Nimesikia hoja yabkuwa na wahubiri wenye digrii ya teolojia. Je, ni sehemu gani kwenye Biblia ambapo Yesu alianzisha chuo cha teolojia ama kuagiza kianzishwe? Teolojia ni elimu ya kimfafanua Mungu KWA MTAZAMO WA ANAYEFUNDISHA. Hili ni tatizo. Tukifika hapo itabidi waprotestanti, wasabato, wakatoliki, moraviani, waanglikana na walutheri wakalishwe chini kuamua mafundisho yapi ni ya Mungu wa kweli. Itabidi tuamue teolojia ipi ni ya kweli na ndiyo hasa anayoikubali Mwenyezi Mungu.
Labda tujiulize mafundisho potofu ni nini? Hapo ndipo penye mgogoro na si vinginevyo. Sisemi haya kutetea mambo ya mafuta na maji ya upako, hasha. Nasema kwa sababu naona suala hili linachukua mkondo wa kidunia zaidi, kumpima Mungu kwa elimu ya kidunia wakati kumbe elimi ya Mungu wala haichangamani na hiyo.
4. Je, vifo vimesababishwa na usimamizi mbovu?
Nadhani hapa ndipo penye tatizo. Kilichotokea ni wazi kuwa ni usimamizi mbovu, ama uzembe kwenye kusimamia uendeshaji wa tukio la kukanyaga mafuta. Habari ya kwa nini watu wanaamini katika mafuta haina uhusiano hata kidogo na vifo hivyo. Ni sawa na kuhoji kwa nini watu wanaamini katika mkate na divai, ama katika kuchoma udi n.k. Tatizo liko kwenye utaratibu wa waamini kukipata kile wanachokiaminia.
Mambo ya kiimani yanabaki kuwa juu ya mhusika mwenyewe, hivyo ni ujinga kumwona anayeamininhayo kuwa mjinga. Nikutafuta kuwaingizia wengine imani yako kwa lazima, hivyo kuondoa maana ya uhuru wa kuabudu bila kuvunja sheria. Kama sheria imevunjwa, sio sheria ya kukanyaga mafuta bali sheria ya kushindwa kusimamia kusanyiko kwa usalama.
Hivyo basi hoja yangu imelenga kuonyesha kuwa sio sahihi kuanza kushambulia imani ya watu kwa vigezo vya nini sisi wengine tunakiamini, bali yatupasa kuwafundisha uzuri wa imani zetu na ubaya wa imani yao ili waamini habari zetu waachane na hayo yao.
Ni makosa makubwa kuwaaminisha wau kuwa tukio la mwamposa inashabihiana na lile la Kibwetee wa Uganda. Hii ni namna ya kutafuta kushambulia imani nyingine kwa mgongo wa nyuma na ndipo hoja za wenye imani tofauti zilipojikita. Mpaka sasa sielewi ni kwa vipi tukio la Moshi limefanana na lile la Kibwetere. Ni uongo na uzushi mkubwa wa wenye kuishambulia imani.
Nawasihi utafakari kwa kina tatizo lilipo, tuachane na mihemkoa bali tuwe wakweli kwani kweli itatuweka huru.
Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Nabii ambaye ameshindwa hata kujua kwamba hili tukio litatokea,kwanini hakuoteshwa,tukio limetokea,akakimbilia Dar,watu wamekufa kanisani kwako,hata kubaki kutoa pole,wewe unakimbia unakimbilia Dar,kuogopa mikono ya polisiNimekuwa nikitafakari kile kinachoendelea kufuatia tukio la vifo vya watu 20 vilivyotokea huko Moshi kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa "Bulldozer." Baada ya tukio hilo kumekuwa na maoni mengi na mitazamo tofauti kwa ujumla kutokana na jinsi ukio hilo lilivyotokea, nami nimeona nitoe mtazamo wangu juu ya jambo hili.
Chanzo cha vifo ni kipi hasa?
Hapa nimeona nichambue kwa kina tatizo hasa ni nini. Kumekuwa na mitazamo hasi kuhusiana na chanzo hasa cha vifo kiasi kwamba kumekuww na hasira kali juu ya imani ya baadhi ya watu.
1. Je vifo vimetokana na mafuta?
Ukitafakari kwa kina utaona hili si kweli. Mafuta hayakusababisha hivyo vifo kwa sababu hayuko hata mmoja aliyetumia mafuta hayo na kufariki. Mafuta hayo yamekuwa yakikanyagwa mara nyingi, kwa miaka mingi pasipo kuwa na madhara kwa watumiaji.
2. Je vifo vimesababishwa na mafundisho?
Ni muhimu kupima mafundisho kama ndio chanzo hasa cha vifo hivi. Kwamba kile kilichohubiriwa siku hiyo ndicho kilichopelekea watu kukanyagana hata vifo kutokea. Kama siku hiyo waliambiwa watakuokuwa wa kwanza kukanyaga mafuta watapokea upako kiasi cha kuwalazimu waamini kugombania nafasi ya kwanza basi hilo ni tatizo. Lakini kama fundisho lilikuwa ni kwamba kukanyaga mafuta tu ni kupokea baraka, basi haijalishi kama ni wa kwanza ama ni wa mwisho.
3. Je vifo vimesababishwa na mafundisho potofu?
Hili ni suala pana kwa sababu limelenga mambo ya kiimani. Nilishangaa jana pale nilipomsikiliza waziri Simbachawene akielezea jinsi ambavyo huwa anaangalia baadhi ya mafundisho na kujiuliza kama kuna Mungu pale. Siamini kama ni jukumu la waziri kupima wapi pana Mungu wa kweli na wapi hapana Mungu.
Mwenye jukumu la kupima usahihi wa mafundisho ni nani hasa linapokuja suala la imani? Nimesikia hoja yabkuwa na wahubiri wenye digrii ya teolojia. Je, ni sehemu gani kwenye Biblia ambapo Yesu alianzisha chuo cha teolojia ama kuagiza kianzishwe? Teolojia ni elimu ya kimfafanua Mungu KWA MTAZAMO WA ANAYEFUNDISHA. Hili ni tatizo. Tukifika hapo itabidi waprotestanti, wasabato, wakatoliki, moraviani, waanglikana na walutheri wakalishwe chini kuamua mafundisho yapi ni ya Mungu wa kweli. Itabidi tuamue teolojia ipi ni ya kweli na ndiyo hasa anayoikubali Mwenyezi Mungu.
Labda tujiulize mafundisho potofu ni nini? Hapo ndipo penye mgogoro na si vinginevyo. Sisemi haya kutetea mambo ya mafuta na maji ya upako, hasha. Nasema kwa sababu naona suala hili linachukua mkondo wa kidunia zaidi, kumpima Mungu kwa elimu ya kidunia wakati kumbe elimi ya Mungu wala haichangamani na hiyo.
4. Je, vifo vimesababishwa na usimamizi mbovu?
Nadhani hapa ndipo penye tatizo. Kilichotokea ni wazi kuwa ni usimamizi mbovu, ama uzembe kwenye kusimamia uendeshaji wa tukio la kukanyaga mafuta. Habari ya kwa nini watu wanaamini katika mafuta haina uhusiano hata kidogo na vifo hivyo. Ni sawa na kuhoji kwa nini watu wanaamini katika mkate na divai, ama katika kuchoma udi n.k. Tatizo liko kwenye utaratibu wa waamini kukipata kile wanachokiaminia.
Mambo ya kiimani yanabaki kuwa juu ya mhusika mwenyewe, hivyo ni ujinga kumwona anayeamininhayo kuwa mjinga. Nikutafuta kuwaingizia wengine imani yako kwa lazima, hivyo kuondoa maana ya uhuru wa kuabudu bila kuvunja sheria. Kama sheria imevunjwa, sio sheria ya kukanyaga mafuta bali sheria ya kushindwa kusimamia kusanyiko kwa usalama.
Hivyo basi hoja yangu imelenga kuonyesha kuwa sio sahihi kuanza kushambulia imani ya watu kwa vigezo vya nini sisi wengine tunakiamini, bali yatupasa kuwafundisha uzuri wa imani zetu na ubaya wa imani yao ili waamini habari zetu waachane na hayo yao.
Ni makosa makubwa kuwaaminisha wau kuwa tukio la mwamposa inashabihiana na lile la Kibwetee wa Uganda. Hii ni namna ya kutafuta kushambulia imani nyingine kwa mgongo wa nyuma na ndipo hoja za wenye imani tofauti zilipojikita. Mpaka sasa sielewi ni kwa vipi tukio la Moshi limefanana na lile la Kibwetere. Ni uongo na uzushi mkubwa wa wenye kuishambulia imani.
Nawasihi utafakari kwa kina tatizo lilipo, tuachane na mihemkoa bali tuwe wakweli kwani kweli itatuweka huru.
Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Mwamposa ni MTUME, hilo la unabii mnalijua ninyi huko kwenye imani yenu.
Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Nimekuelewa vizuri,na umenijibu vizuri na nimekufahamu kwa kisasi kuliko post yako ya kwanza ilivyokaa.Sasa kuhusu uhalali wa mafuta umesema siyo mada,niliheshimu hilo.Ni kweli, majaribu ya Mwamposa yaweza yasiwe majaribu pia. Kwa ujumla ibada yabkuabudu mafuta siikubali kabisa, ila niliona watu wenye misimamo mibaya wakijarinbu kutumia tukio hilo kuukashifu ukristo ama wokovu kwa ujumla.
Ninachosema ni kuww pamoja na watu kufatiki,sio jukumu la serikali kupima maandiko na kuamua kipi ni sahihi. Ndio maana nikaandika haya kupinga tamko la waziri na baadhi wa watu waliohojiwa kwenye vyombo vya habari kutaka kuhalialisha jambo hili. Ni kweli kwa upande wa kiimani siamininkama biblia imeagiza hayo, kwani hakuna maandiko, bali kiserikali pia wako ambao hawakuwajibika.
AMINA
Sent from my SM-T355Y using Tapatalk