Mtume Mwamposa na jaribu la imani

Mtume Mwamposa na jaribu la imani

Sana.
lakini kwakua wamewateka hawataelewa. kuna interview niliionaga mwezi jana , kuhusu jamaa mmoja aliteswa na mchungaji huko bukoba inafungua sana akili
Wakati huo huo huwa wanaaminisha watu kuwa wanaongozwa na kulindwa na mahali walipo pana nguvu na ulinzi wa Mungu,
Waache kulitaja burebure jina la mtakatifu azidiye utakatifu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Prophet -a person regarded as an inspired teacher or proclaimer of the will of God.

awali ya yote ; imekuwaje Nabii Mwamposya asipewe ishara na Mwenyezi Mungu kwamba haya yatatokea...?

Sent using Jamii Forums mobile app
inashangaza sana..nabii anakosa channel ya kuconnect na mungu.......looooohhh

hapo hapo waweza kukuta katika mafundisho yake amewahi kusema kwamba ..mungu kaniotesha hivi na vile
 
Yaweza kuwa vyombo vya mafuta na pia walitarajia utaratibu wa kupanga mstari lakini watu wakavamia kila mmoja anataka awe wa kwanza. Tuliza kichwa mkuu.

Kibwetere alikuwa na mahubiri na mafundisho tofauti sana mkuu, ndio maana nikahoji, kuna tatizo gani kwenye hayo mafundisho ya Mwamposa in relation to the incidence? Hoja iko hapo, mihemko pembeni. Ya kibwetere hata teolojia yake haikuwa salama kwa wanadamu, sasa teolojia ya Mwamposa ina tatizo gani kiusalama? Tuache chuki binafsi.

Mimi ni mpingaji namba moja wa teolojia. Hii ni elimu ya kum-define Mungu kwa mtazamo wa mtu ama kikundi cha watu. Huko ndiko huzaliwa viu kama statement of faith. Ni mambo haya yabteolojia yaliyoingiza imani potofu kwenye kanisa, ibada ambazo hazina sapoti ya biblia. Kumbe basi natazama Neno la Mungu zaidi kuliko kusikiliza mwana teolojia amesema nini.

Ni wapi imeandikwa mafuta ni matakatifu? Mafuta yatabaki mafuta tu, ila kwa imani watu huamini kilichonenwa juu ya mafuta hayo kitawapa matokeo. Kumwaga chini? Hapa sijakuelewa mkuu, mafuta huwekwa kwenye vyombo ili watu wakanyage, miguu ikiwa sehemu ya mwili.

Nachelea kuongea sana kwa sababu mimi pia siamini katika mafuta ila najenga tu hoja kwamba watu wanamhukumu Mwamposa kwa kufuata hisia binafsi juu ya huduma yake. Hakuna sehemu kwenye biblia inaposema ukimwaga mafuta mwenye vyombo watu wakanyage ni dharau.

Yesu aliponya kwa mate, nadhani ungekuwepo enzi hizo ungempiga mawe. Tatizo lako unadhani Mungu anaangalia heshima za nje ambazo kimsingi ni unafiki mkubwa, Mungu anaangalia ROHO YAKO. Hili ndilo lilipelekea Mungu kuwekwa kwenye vyombo makanisani pia, akatunzwa sakaristia. Matokeo yake wengine kama kina Bulldozer wamemweka kwenye mafuta, kwa nini basi uwanyooshee kidole?

Elimu itakupa maarifa ni kweli, lakaini maarifa ya dunia hii. Elimu ya Mungu itakupa ujuzi wa ufalme wa mbinguni. Hakuna chuo cha teolojia kina uwezo wa kufundisha hili zaidi ya mashindano ya doctrines kwamba kwa nini sisi tunaamini hivi na wao wanaamini vile.

Kumbuka tangu kale na HATA SASA Mungu alivichagua vitu vinyonge na vidhaifu ili kuviaibisha vikubwa na vyenye nguvu. Unaielewa hiyo?

Kama maprofesa wanakwenda kunywa kikombe cha babu, ama kukanyaga mafuta ya upako, yako wapi maarifa hayo unayosema? Elimu ya Mungu itabaki kuwa hivyo na ya dunia kadhalika.

Kuhusu kuzika vitu vitakatifu, Mungu wa leo hakai kwenye vitu bali akaa kwenye roho zao wamtafutao kwa bidii. Habari za ukigusa hostia utapatwa kichaa sio biblical bali ni mafundisho ya kibinadamu. Tusimshushe Mungu wetu hivyo, tumheshimu kama alivyotaka. Ndio maana leo hii hatuendi kuhiji Israeli kwa sababu hakuna tena ya kuabudu mlima huu wa ule.

Tusome biblia.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk

Kama huamini kama kuna mafuta matakatifu iweje ukubaliane na hoja ya kuwa huyu jamaa sio tapeli

Kuhusu kukataa theologia hawa wachungaji wanapoenda hivyo vyuo vya biblia wanafundishwa na kina nani

Kuhusu point ya kuwafungulia watu geti moja umepuyanga huna point ya msingi umeandika consipirancy juu ya wazo lako ndio maana ukaanza na neno “ inawezekana”

Tunahimizwa kumpenda Mungu kwa nguvu zetu zote, na akili zetu zote......ndugu zetu mnapotea kwa kuwa mnampenda Mungu kwa mhemuko akili mnaacha ndio maana mkiambiwa kunyweni jiki mnakunywa

Unasema tusome biblia ni wapi kwenye biblia pameandika tukanyage mafuta ili tupate baraka

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu umedadavua vizuri ila kuna wakati unajichanganya. Unasema ni makosa kumfananisha mwamposa na kibwetere. Mi sioni tofauti zao. Wa mwamposa wanaona wa kibwetere potofu na wa kibwetere wanaona wa mwamposa potofu. Wote wameruhusiwa na mamlaka za nchi zao kueneza neno. Mimi naona wote wawili ni potofu.

Kibwetere alifunga milango ya kanisa waumini wakateketea. Mwamposa kuweka mafuta kwenye mlango wa geti moja maelfu ya waumini wapite wakikanyaga, wakafa. Kwangu mimi sioni tofauti. Yote ni makosa yatokanayo na kukosa busara ya kimungu.

Wewe mwenyewe umeweka swali "Mwenye jukumu la kupima usahihi wa mafundisho ni nani hasa linapokuja suala la imani?". Sasa kama unaona ni ngumu kupima usahihi wa mafundisho ya kiimani, ni kwa nini unabeza imani ya kina kibwetere? Kubali kila mtu abaki na imani yake. We unaona ya mwamposa sawa, kibwetere anaona yake sawa, mi naona ya wamposa na kibwetere si sawa ni utapeli, bali imani yangu ndio sawa.

Kwa kifupi hautafanikiwa kutetea usahihi wa imani ya mwamposa, achilia mbali kumuondoa kwenye hatia ya vifo vilivyotokana na aliyofanya.

Na ni bora baada ya hii kesi ashauriwe aachane na jina "bulldozer". Ame bulldoze watu to death!!!

Mkuu umemaliza kila kitu🤙🏻🤙🏻

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kama huamini kama kuna mafuta matakatifu iweje ukubaliane na hoja ya kuwa huyu jamaa sio tapeli

Kuhusu kukataa theologia hawa wachungaji wanapoenda hivyo vyuo vya biblia wanafundishwa na kina nani

Kuhusu point ya kuwafungulia watu geti moja umepuyanga huna point ya msingi umeandika consipirancy juu ya wazo lako ndio maana ukaanza na neno “ inawezekana”

Tunahimizwa kumpenda Mungu kwa nguvu zetu zote, na akili zetu zote......ndugu zetu mnapotea kwa kuwa mnampenda Mungu kwa mhemuko akili mnaacha ndio maana mkiambiwa kunyweni jiki mnakunywa

Unasema tusome biblia ni wapi kwenye biblia pameandika tukanyage mafuta ili tupate baraka

Sent from my iPhone using JamiiForums
yaani mtoa post ana tetea ule ujangili wa mwamposa...?..no wonder kwanini sijalisoma bandiko lake
 
Nimekuwa nikitafakari kile kinachoendelea kufuatia tukio la vifo vya watu 20 vilivyotokea huko Moshi kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa "Bulldozer." Baada ya tukio hilo kumekuwa na maoni mengi na mitazamo tofauti kwa ujumla kutokana na jinsi ukio hilo lilivyotokea, nami nimeona nitoe mtazamo wangu juu ya jambo hili.

Chanzo cha vifo ni kipi hasa?

Hapa nimeona nichambue kwa kina tatizo hasa ni nini. Kumekuwa na mitazamo hasi kuhusiana na chanzo hasa cha vifo kiasi kwamba kumekuww na hasira kali juu ya imani ya baadhi ya watu.

1. Je vifo vimetokana na mafuta?
Ukitafakari kwa kina utaona hili si kweli. Mafuta hayakusababisha hivyo vifo kwa sababu hayuko hata mmoja aliyetumia mafuta hayo na kufariki. Mafuta hayo yamekuwa yakikanyagwa mara nyingi, kwa miaka mingi pasipo kuwa na madhara kwa watumiaji.

2. Je vifo vimesababishwa na mafundisho?
Ni muhimu kupima mafundisho kama ndio chanzo hasa cha vifo hivi. Kwamba kile kilichohubiriwa siku hiyo ndicho kilichopelekea watu kukanyagana hata vifo kutokea. Kama siku hiyo waliambiwa watakuokuwa wa kwanza kukanyaga mafuta watapokea upako kiasi cha kuwalazimu waamini kugombania nafasi ya kwanza basi hilo ni tatizo. Lakini kama fundisho lilikuwa ni kwamba kukanyaga mafuta tu ni kupokea baraka, basi haijalishi kama ni wa kwanza ama ni wa mwisho.

3. Je vifo vimesababishwa na mafundisho potofu?
Hili ni suala pana kwa sababu limelenga mambo ya kiimani. Nilishangaa jana pale nilipomsikiliza waziri Simbachawene akielezea jinsi ambavyo huwa anaangalia baadhi ya mafundisho na kujiuliza kama kuna Mungu pale. Siamini kama ni jukumu la waziri kupima wapi pana Mungu wa kweli na wapi hapana Mungu.

Mwenye jukumu la kupima usahihi wa mafundisho ni nani hasa linapokuja suala la imani? Nimesikia hoja yabkuwa na wahubiri wenye digrii ya teolojia. Je, ni sehemu gani kwenye Biblia ambapo Yesu alianzisha chuo cha teolojia ama kuagiza kianzishwe? Teolojia ni elimu ya kimfafanua Mungu KWA MTAZAMO WA ANAYEFUNDISHA. Hili ni tatizo. Tukifika hapo itabidi waprotestanti, wasabato, wakatoliki, moraviani, waanglikana na walutheri wakalishwe chini kuamua mafundisho yapi ni ya Mungu wa kweli. Itabidi tuamue teolojia ipi ni ya kweli na ndiyo hasa anayoikubali Mwenyezi Mungu.

Labda tujiulize mafundisho potofu ni nini? Hapo ndipo penye mgogoro na si vinginevyo. Sisemi haya kutetea mambo ya mafuta na maji ya upako, hasha. Nasema kwa sababu naona suala hili linachukua mkondo wa kidunia zaidi, kumpima Mungu kwa elimu ya kidunia wakati kumbe elimi ya Mungu wala haichangamani na hiyo.

4. Je, vifo vimesababishwa na usimamizi mbovu?
Nadhani hapa ndipo penye tatizo. Kilichotokea ni wazi kuwa ni usimamizi mbovu, ama uzembe kwenye kusimamia uendeshaji wa tukio la kukanyaga mafuta. Habari ya kwa nini watu wanaamini katika mafuta haina uhusiano hata kidogo na vifo hivyo. Ni sawa na kuhoji kwa nini watu wanaamini katika mkate na divai, ama katika kuchoma udi n.k. Tatizo liko kwenye utaratibu wa waamini kukipata kile wanachokiaminia.

Mambo ya kiimani yanabaki kuwa juu ya mhusika mwenyewe, hivyo ni ujinga kumwona anayeamininhayo kuwa mjinga. Nikutafuta kuwaingizia wengine imani yako kwa lazima, hivyo kuondoa maana ya uhuru wa kuabudu bila kuvunja sheria. Kama sheria imevunjwa, sio sheria ya kukanyaga mafuta bali sheria ya kushindwa kusimamia kusanyiko kwa usalama.

Hivyo basi hoja yangu imelenga kuonyesha kuwa sio sahihi kuanza kushambulia imani ya watu kwa vigezo vya nini sisi wengine tunakiamini, bali yatupasa kuwafundisha uzuri wa imani zetu na ubaya wa imani yao ili waamini habari zetu waachane na hayo yao.

Ni makosa makubwa kuwaaminisha wau kuwa tukio la mwamposa inashabihiana na lile la Kibwetee wa Uganda. Hii ni namna ya kutafuta kushambulia imani nyingine kwa mgongo wa nyuma na ndipo hoja za wenye imani tofauti zilipojikita. Mpaka sasa sielewi ni kwa vipi tukio la Moshi limefanana na lile la Kibwetere. Ni uongo na uzushi mkubwa wa wenye kuishambulia imani.

Nawasihi utafakari kwa kina tatizo lilipo, tuachane na mihemkoa bali tuwe wakweli kwani kweli itatuweka huru.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Muheshimiwa Mwaiposa naona umekuja kuzima moto kidogo...
 
Kiuhalisia sio kwamba alikimbia alikuwa anawahi usafiri kwa ajili ya Ibada ya kesho yake jijini Dar. Na huwa akimaliza kuhudumu kwa maana ya mahubiri na maombezi huondoka na kuacha kazi ya kukanyaga mafuta ikisimamiwa na wahudumu wake kama sikosei.
Atawahi vipi ilhali kaacha majanga ya vifo huku nyuma??
Na kuwahi kwenyewe ndio kutumia usafiri was gari kuliko wa ndege maana alijua atadakwa airport
 
Nimekuwa nikitafakari kile kinachoendelea kufuatia tukio la vifo vya watu 20 vilivyotokea huko Moshi kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa "Bulldozer." Baada ya tukio hilo kumekuwa na maoni mengi na mitazamo tofauti kwa ujumla kutokana na jinsi ukio hilo lilivyotokea, nami nimeona nitoe mtazamo wangu juu ya jambo hili.

Chanzo cha vifo ni kipi hasa?

Hapa nimeona nichambue kwa kina tatizo hasa ni nini. Kumekuwa na mitazamo hasi kuhusiana na chanzo hasa cha vifo kiasi kwamba kumekuww na hasira kali juu ya imani ya baadhi ya watu.

1. Je vifo vimetokana na mafuta?
Ukitafakari kwa kina utaona hili si kweli. Mafuta hayakusababisha hivyo vifo kwa sababu hayuko hata mmoja aliyetumia mafuta hayo na kufariki. Mafuta hayo yamekuwa yakikanyagwa mara nyingi, kwa miaka mingi pasipo kuwa na madhara kwa watumiaji.

2. Je vifo vimesababishwa na mafundisho?
Ni muhimu kupima mafundisho kama ndio chanzo hasa cha vifo hivi. Kwamba kile kilichohubiriwa siku hiyo ndicho kilichopelekea watu kukanyagana hata vifo kutokea. Kama siku hiyo waliambiwa watakuokuwa wa kwanza kukanyaga mafuta watapokea upako kiasi cha kuwalazimu waamini kugombania nafasi ya kwanza basi hilo ni tatizo. Lakini kama fundisho lilikuwa ni kwamba kukanyaga mafuta tu ni kupokea baraka, basi haijalishi kama ni wa kwanza ama ni wa mwisho.

3. Je vifo vimesababishwa na mafundisho potofu?
Hili ni suala pana kwa sababu limelenga mambo ya kiimani. Nilishangaa jana pale nilipomsikiliza waziri Simbachawene akielezea jinsi ambavyo huwa anaangalia baadhi ya mafundisho na kujiuliza kama kuna Mungu pale. Siamini kama ni jukumu la waziri kupima wapi pana Mungu wa kweli na wapi hapana Mungu.

Mwenye jukumu la kupima usahihi wa mafundisho ni nani hasa linapokuja suala la imani? Nimesikia hoja yabkuwa na wahubiri wenye digrii ya teolojia. Je, ni sehemu gani kwenye Biblia ambapo Yesu alianzisha chuo cha teolojia ama kuagiza kianzishwe? Teolojia ni elimu ya kimfafanua Mungu KWA MTAZAMO WA ANAYEFUNDISHA. Hili ni tatizo. Tukifika hapo itabidi waprotestanti, wasabato, wakatoliki, moraviani, waanglikana na walutheri wakalishwe chini kuamua mafundisho yapi ni ya Mungu wa kweli. Itabidi tuamue teolojia ipi ni ya kweli na ndiyo hasa anayoikubali Mwenyezi Mungu.

Labda tujiulize mafundisho potofu ni nini? Hapo ndipo penye mgogoro na si vinginevyo. Sisemi haya kutetea mambo ya mafuta na maji ya upako, hasha. Nasema kwa sababu naona suala hili linachukua mkondo wa kidunia zaidi, kumpima Mungu kwa elimu ya kidunia wakati kumbe elimi ya Mungu wala haichangamani na hiyo.

4. Je, vifo vimesababishwa na usimamizi mbovu?
Nadhani hapa ndipo penye tatizo. Kilichotokea ni wazi kuwa ni usimamizi mbovu, ama uzembe kwenye kusimamia uendeshaji wa tukio la kukanyaga mafuta. Habari ya kwa nini watu wanaamini katika mafuta haina uhusiano hata kidogo na vifo hivyo. Ni sawa na kuhoji kwa nini watu wanaamini katika mkate na divai, ama katika kuchoma udi n.k. Tatizo liko kwenye utaratibu wa waamini kukipata kile wanachokiaminia.

Mambo ya kiimani yanabaki kuwa juu ya mhusika mwenyewe, hivyo ni ujinga kumwona anayeamininhayo kuwa mjinga. Nikutafuta kuwaingizia wengine imani yako kwa lazima, hivyo kuondoa maana ya uhuru wa kuabudu bila kuvunja sheria. Kama sheria imevunjwa, sio sheria ya kukanyaga mafuta bali sheria ya kushindwa kusimamia kusanyiko kwa usalama.

Hivyo basi hoja yangu imelenga kuonyesha kuwa sio sahihi kuanza kushambulia imani ya watu kwa vigezo vya nini sisi wengine tunakiamini, bali yatupasa kuwafundisha uzuri wa imani zetu na ubaya wa imani yao ili waamini habari zetu waachane na hayo yao.

Ni makosa makubwa kuwaaminisha wau kuwa tukio la mwamposa inashabihiana na lile la Kibwetee wa Uganda. Hii ni namna ya kutafuta kushambulia imani nyingine kwa mgongo wa nyuma na ndipo hoja za wenye imani tofauti zilipojikita. Mpaka sasa sielewi ni kwa vipi tukio la Moshi limefanana na lile la Kibwetere. Ni uongo na uzushi mkubwa wa wenye kuishambulia imani.

Nawasihi utafakari kwa kina tatizo lilipo, tuachane na mihemkoa bali tuwe wakweli kwani kweli itatuweka huru.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
huwa nafuatilia maandiko yako mengi sana hapa jamvini ndugu Nyenyere ......... unajua kujenga hoja hongera sana!

mimi kama m-pentekoste ninayeijua imani yangu naamini kabisa kwa sehemu kubwa bado watumishi wengi hawamjui Mungu hasa ndio maana tunalazimishwa kumfuata Mungu kwa matakwa ya taasisi zetu na sio vile Mungu atakavyo!

hili la Mwamposa nadhan ni matokeo ya taasisi za kidini nyingi kumhodhi Mungu kama mali yao, yani wanamfanya Mungu kama wa kwao na vile wanavyosema wao ndivyo alivyo which i think is totally wrong!....

sasa, ukifuatilia matamko mengi na maneno mengi mitaani inaonekana Mwamposa (binafsi simfahamu hata) ni mtume wa uongo n.k kwa sababu tu ameenda tofauti na yule Mungu wao wanataka wote tumfuate!......

hawa hawa wanaomkosoa mwamposa walipanga foleni kule Loliondo kunywa mitishamba katika mazingira machafu sana, hata wakatengeneza barabara ndani ya wiki sijui mwezi! UNAFIKI mtupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli kabisa mleta mada ana hoja za kimsingi. Ameweka msingi wa kuchambua. Bahati mbaya sana wengi wetu hapa tumejikita kwenye ushabiki, kejeli na hisia.

Binafsi ninaona Mwamposa anapaswa kuwajibika moja kwa moja na tukio hili kwa sababu hizi....

(i)Tukio lile limetokea katika kongamano lake. Hakuna mtu mwingine zaidi yake aliyepaswa kuwajibika ikiwa kulikuwa kuna mapungufu ya kiusalama. (Mwamposa alipaswa kuona mapungufu kabla, kuchukua tahadhari na kuepusha haya yote yasitokee)

(ii)Tukio hili limetokea katika utekelezaji wa fundisho lake la kukanyaga mafuta ambalo limekuwa ni sehemu ya huduma yake inayomtambulisha na anayokazia siku zote. (Hamasa na shauku ya juu ya watu kwenda kukanyaga mafuta vimechangia haya kutokea)

(iii)Mwamposa alishindwa kuwajibika au kuonyesha kama ameguswa na tukio hili wakati lilipotokea na baada ya kutokea. (Huenda vifo au majeruhi wangepungua ikiwa angewajibika ipasavyo wakati hayo yakitokea)

(iv)Kulikuwa na uzembe wa wazi kabisa kutoka kwake yeye mwenyewe ambao huenda umechangia hayo kutokea.
(Kivipi? Wito wa watu kwenda kukanyaga mafuta aliutoa yeye mwenyewe wakati tayari hali ilikuwa hairuhusu kabisa. Kwanza ilikuwa ni Usiku (giza? Setting zote za mkutano zililenga mkutano wa mchana na sio usiku), Pili hali ya hewa ilikuwa mbaya (Mvua? Matope? Utelezi? Dalili za mvua nzito kunyesha zaidi?) na tatu ilikuwa muda wa mkutano kupitiliza sana (Kugombania? Waumini wengi huenda walivumilia kukaa na kuchelewa kwenda makwao kwa sababu tukio la kukanyaga mafuta lilikuwa bado kuruhusiwa, hivyo wito wa Mwamposa kuufunga mkutano na kuwaambia watu wakakanyage mafuta ilikuwa ni kupiga filimbi ya kuyakimbilia mafuta yalipo.)

IMANI YA KUKANYAGA MAFUTA
Huu ni mjadala mwingine na hauwezi kupata hitimisho milele hapa JF. Kwanini? Hatuna misingi sawa ya kuweza kuamini.

Nikizungumza katika context za kibiblia (kitabu ambacho mtu yoyote anaweza kukisoma na kukichambua yeye binafsi regardless wa dini gani), Binafsi imani hii ya kukanyaga mafuta naiona kama ubagani fulani. Kiukweli kabisa sioni tofauti yoyote na imani ya kulishwa mkate na divai na kuaminishwa dhambi zimefutwa au utaingia mbinguni, kujipaka maji ya baraka, kutembea na misalaba huku ukiamini itakusaidia, kuamini kuwa rozali inaweza kukulinda nk. Zote hizo ni kama hirizi tu. Ukristo ni Yesu kristo tu. Kama Yesu kristo pekee hawezi kumtosheleza mkristo binafsi katika maisha yake basi hakuna kitu kingine cha ziada kinaweza kuziba hilo umbwe kwa huyo mtu.
 
Back
Top Bottom