Mtume Mwamposa na jaribu la imani

Mtume Mwamposa na jaribu la imani

Pia waweza kuuliza hivi, ni kwa nini Mwenyezi Mungu asimpe ishara kuwa haya yatatokea? Hilo swali lako lapaswa kujibiwa ya huyo Mwenyezi Mungu unayemtuhumu kutotoa ishara.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Mungu ni Boss wa maboss wote; haulizwi kwanini, huo ni utovu wa nidhamu. Chukua neno hili la Biblia;;;.WATU WANGU HUANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA''. Maarifa ni kulifahamu neno sahihi la Mungu
 
Hapa umepiga siasa mkuu. Kibwetere alisimama kama mkristo, akitumia biblia. Mwisho wa siku aliwaambia waumini wake mwisho wa dunia umefika akawafungia ndani na kuwacchoma moto. Swali kwako, hilo fundisho LA KUUA limo kwenye biblia ama ni serikali ipi duniani ingeruhusu mtu binafsi kuhujumu maisha ya mwingine?

Mwamposa ni wapi aliwafungia waumini akawamwagia mafuta akawachoma moto? Ama labda amewapa mafuta yenye sumu wakafa? Yeye kafundisha anachoamini kamaliza, akafanya zoezi la kukanyaga mafuta ambalo hufanyika kwenye ibada zake mara zote, kilichotokea kwa sababu ya kushindwa ukontroo watu wakarundikana na kukanyagana.

Kwa mtazamo wako Mwamposa na Kibwetere wana kesi sawa ya kujibu? Aliyewasha moto na kuwachoma watu na yule aliyeweka mafuta watu wakanyage badala yake wakarundikana n kukanyagana wao wenyewe? Haya nionyeshe wapi kufanana kwao. Kosa la kibwetere ni la mauaji, kosa la Mwamposa hapo ni lipi?

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk

Wewe unaandika hivi sababu hujafiwa. unatetea imani yako na mwamposa tu.

Kibwetere na mwamposa hawana tofauti. kesi yao ni ileile KUDANGANYA kwa kutumia imani na KUTENGENEZA MAZINGIRA yaliyosababisha vifo.

Kibwetere alitumia bible kuona mwisho wa dunia, mwamposa anatumia bible kutibu HIV, mimba, kuwapa wa2 utajiri, nk.

Hivi unafahamu sehemu kubwa ya waliokufa kwa mwamposa ni WATOTO na KINAMANA? Mwanamme mtu mzima aliekufa ni mmoja tu. Utawekaje WATOTO na WAGONJWA wakanyage mafuta katika mazingira yale?

Hivi unafahamu mwamposa kaua WATOTO na KINAMAMA au unatetea tu? Kwa nini WATOTO na KINAMAMA ambao kati yao ni WAGONJWA wasingepewa mafuta kwa njia nyingine?

Kuanzia sasa usiseme mwamposa kaua WATU, sema kaua KINAMANA, WATOTO, WAGONJWA. Nadhani ukisema hivi itakusaidia kujua kosa lake. Ile ni stampede ya wanaume wenye nguvu kuua KINAMAMA na WATOTO kati yao WAGONJWA. Mwanamme mtu mzima kafa mmoja tu!!!
 
Mkuu samahani lakini kama nimekukwaza. Mie mkristo mwenzako na hiyo bible naisoma na kuielewa.
Ila kwa hili la kutetea vifo vya kinamama, watoto na wagonjwa ni big no!!!
 
Simtuhumu!
proclaimer of the will of God. anakosaje ishara? kukosa ishara ni ishara kwamba Sio Nabii kama mnavyosema.
Na Mwenyezi Mungu sio mkatili kutoa jaribu juu ya roho za watu. majaribu yapo mengi magumu yasiyodhurumu nafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
"Mungu" wakati anamuumba "Shetani" alikosa ishara kuwa "Shetani" atakuja kuleta "matatizo"?
Vipi wakati anaumba ulimwengu, hakupata ishara kuwa kutakuwa na " natural calamities" kama matetemeko ya ardhi na milipuko ya volcano?
Kama "Mungu" alishindwa kupata ishara hakuna ajabu lolote Mwamposa akishindwa kupata ishara.
 
Mimi binafsi kutoka juzi sijachangia chochote kuhusu hili tukio ila nakubaliana na wanaosema aina ya mafundisho yanachangia, nasema hivi kwa sababu sisi sote huwa tunaenda kanisani, tunajua taratibu za ibada zetu kuwa hakuna mambo ya fujo na kukanyagana.
Hii inadhihirisha wazi kuwa watu waliokuwepo kwenye ule mkutano hawajahubiriwa habari njema ya wokovu, mtu anatoka huko kulewa, kufanya ukahaba hana shida na habari ya wokovu anachotaka akakanyage mafuta apate baraka full stop

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwamposa alimpasa asubiri zoezi lote limeisha na watu wote wameondoka ndio aondoke.
Mwamposa alikuwa na haraka ya kupanda ndege ili awahi ibada ya Daresalaam.
Mwamposa inabidi ajifunze kwa hili tukio kuwa kazi yake isiwe kukimbilia sadaka sehemu nyingine badi kuhakikisha usalama wa watu kila anapofanya kazi yake.
Mwamposa alitakiwa kuwaongoza watu wakanya hayo mafuta kwa utaratibu wa usalama hadi waishe wote ndio aondoke.
Badara yake akawaachia vijana wa Arachuga wasimamie.
Hilo zoezi kwake halikuwa na maana yoyote ndio maana akaondoka zake.
Mwamposa inabidi atambue anaongoza Roho za watu zenye thamani sana, kama anataka kuendelea na kazi yake lazima awaheshimu na kuwasimamia kwa umakini mkubwa.
Watu wanafariki kwenye zoezi lake na yeye kukimbia na kuendelea kuhubiri sehemu nyingine ni dharau kubwa sana.
Mwamposa lazima ajue kuwa
Kama atasababisha tena watu kufariki kwenye mkutano wake hataachwa salama.
Iwe Mwanzo na Mwisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada anatetea ujinga, kwenye maandiko, wapi imeandikwa kuna kukanyaga mafuta halafu madhehebu yaangalie kama kuna ukweli, wakati ni uongo. Huna neno

Sent using Jamii Forums mobile app
Sipendi mabishano yasiyo faida. Nadhani hujaelewa msingi wa mada hii, mimi si muumini wa mafuta. Soma tena uelewe lengo

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Sitaki kuhukumu lakini Injili ya kweli iletayo wokovu siku hizi ni nadra. Watu wamejikita kwenye shida za watu na ahadi za mafanikio, kinyume kabisa na Yesu alivyoagiza kwamba utafuteni kwanza ufalme wa mbinguni na hayo yote mtazidishiwa. Watu wamejikita kwenye kuhangaika na mambo ya ziada kuliko kuponya roho na nafsi zao zimgeukie Mungu.

Hawa watu wangekua na mafundisho ya kweli wakamjua Mungu vyema hekima naaarifa ya kuwatanguliza wengine au kuona hsijalishi upite wa kwanza au wa mwisho baraka zipo pale pale.

Yesu aliwahi kukemea kizazi kinachofuata ishara na miujiza. Lakini leoanabii wengi ndicho wanachokifanya. Hii ndio kuangamia kwa kukosa maarifa.
Umesema vyema boss

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuwa nikitafakari kile kinachoendelea kufuatia tukio la vifo vya watu 20 vilivyotokea huko Moshi kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa "Bulldozer." Baada ya tukio hilo kumekuwa na maoni mengi na mitazamo tofauti kwa ujumla kutokana na jinsi ukio hilo lilivyotokea, nami nimeona nitoe mtazamo wangu juu ya jambo hili.

Chanzo cha vifo ni kipi hasa?

Hapa nimeona nichambue kwa kina tatizo hasa ni nini. Kumekuwa na mitazamo hasi kuhusiana na chanzo hasa cha vifo kiasi kwamba kumekuww na hasira kali juu ya imani ya baadhi ya watu.

1. Je vifo vimetokana na mafuta?
Ukitafakari kwa kina utaona hili si kweli. Mafuta hayakusababisha hivyo vifo kwa sababu hayuko hata mmoja aliyetumia mafuta hayo na kufariki. Mafuta hayo yamekuwa yakikanyagwa mara nyingi, kwa miaka mingi pasipo kuwa na madhara kwa watumiaji.

2. Je vifo vimesababishwa na mafundisho?
Ni muhimu kupima mafundisho kama ndio chanzo hasa cha vifo hivi. Kwamba kile kilichohubiriwa siku hiyo ndicho kilichopelekea watu kukanyagana hata vifo kutokea. Kama siku hiyo waliambiwa watakuokuwa wa kwanza kukanyaga mafuta watapokea upako kiasi cha kuwalazimu waamini kugombania nafasi ya kwanza basi hilo ni tatizo. Lakini kama fundisho lilikuwa ni kwamba kukanyaga mafuta tu ni kupokea baraka, basi haijalishi kama ni wa kwanza ama ni wa mwisho.

3. Je vifo vimesababishwa na mafundisho potofu?
Hili ni suala pana kwa sababu limelenga mambo ya kiimani. Nilishangaa jana pale nilipomsikiliza waziri Simbachawene akielezea jinsi ambavyo huwa anaangalia baadhi ya mafundisho na kujiuliza kama kuna Mungu pale. Siamini kama ni jukumu la waziri kupima wapi pana Mungu wa kweli na wapi hapana Mungu.

Mwenye jukumu la kupima usahihi wa mafundisho ni nani hasa linapokuja suala la imani? Nimesikia hoja yabkuwa na wahubiri wenye digrii ya teolojia. Je, ni sehemu gani kwenye Biblia ambapo Yesu alianzisha chuo cha teolojia ama kuagiza kianzishwe? Teolojia ni elimu ya kimfafanua Mungu KWA MTAZAMO WA ANAYEFUNDISHA. Hili ni tatizo. Tukifika hapo itabidi waprotestanti, wasabato, wakatoliki, moraviani, waanglikana na walutheri wakalishwe chini kuamua mafundisho yapi ni ya Mungu wa kweli. Itabidi tuamue teolojia ipi ni ya kweli na ndiyo hasa anayoikubali Mwenyezi Mungu.

Labda tujiulize mafundisho potofu ni nini? Hapo ndipo penye mgogoro na si vinginevyo. Sisemi haya kutetea mambo ya mafuta na maji ya upako, hasha. Nasema kwa sababu naona suala hili linachukua mkondo wa kidunia zaidi, kumpima Mungu kwa elimu ya kidunia wakati kumbe elimi ya Mungu wala haichangamani na hiyo.

4. Je, vifo vimesababishwa na usimamizi mbovu?
Nadhani hapa ndipo penye tatizo. Kilichotokea ni wazi kuwa ni usimamizi mbovu, ama uzembe kwenye kusimamia uendeshaji wa tukio la kukanyaga mafuta. Habari ya kwa nini watu wanaamini katika mafuta haina uhusiano hata kidogo na vifo hivyo. Ni sawa na kuhoji kwa nini watu wanaamini katika mkate na divai, ama katika kuchoma udi n.k. Tatizo liko kwenye utaratibu wa waamini kukipata kile wanachokiaminia.

Mambo ya kiimani yanabaki kuwa juu ya mhusika mwenyewe, hivyo ni ujinga kumwona anayeamininhayo kuwa mjinga. Nikutafuta kuwaingizia wengine imani yako kwa lazima, hivyo kuondoa maana ya uhuru wa kuabudu bila kuvunja sheria. Kama sheria imevunjwa, sio sheria ya kukanyaga mafuta bali sheria ya kushindwa kusimamia kusanyiko kwa usalama.

Hivyo basi hoja yangu imelenga kuonyesha kuwa sio sahihi kuanza kushambulia imani ya watu kwa vigezo vya nini sisi wengine tunakiamini, bali yatupasa kuwafundisha uzuri wa imani zetu na ubaya wa imani yao ili waamini habari zetu waachane na hayo yao.

Ni makosa makubwa kuwaaminisha wau kuwa tukio la mwamposa inashabihiana na lile la Kibwetee wa Uganda. Hii ni namna ya kutafuta kushambulia imani nyingine kwa mgongo wa nyuma na ndipo hoja za wenye imani tofauti zilipojikita. Mpaka sasa sielewi ni kwa vipi tukio la Moshi limefanana na lile la Kibwetere. Ni uongo na uzushi mkubwa wa wenye kuishambulia imani.

Nawasihi utafakari kwa kina tatizo lilipo, tuachane na mihemkoa bali tuwe wakweli kwani kweli itatuweka huru.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Hivi utume kwa Wakristo ni kitu gani na unabii ni kitu gani na unapatikanaje ?

Kwetu sisi Waislamu hakuna mtume wala nabii baada ya mtume Muhammad amani ya Allah iwe juu yake.

Na tunasema hivi, kila mtume ni nabii lakini si kila nabii ni mtume. Hawi mtume isipokuwa anafikishiwa ujumbe na Malaika Muheshimiwa Jibril amani ya Allah iwe juu yake.

Mitume hawakuwa washirikina bali waliupiga vita Ushirikina na hali zake zote.

Nasubiri unipe muongozo wa haya maneno mawili yaani Utume na Unabii kwa mujibu wa Ukristo.
 
Najua neno moja tu; Kwa jina la YESU, pepo wanatoka, vilema wanatembea, vipofu wanaona etc.......Yote yamethibitishwa na neno la MUNGU. Sio kwa jina lingine liwalo lolote. Hebu fuatilia mahubiri ya watumishi wa Mungu wakati wa uzinduzi wa jukwaa la JKK pale BCC Mbezi kwa Askofu Gwamanya
Naijua JKK kabla yako nadhani, from day one. Mimi sina tatizo na hicho wanachokihubiri. Labda nikuulize tu, ni kwa nini wanatofautiana doctrine kila mtu na lake? Lengo la jukwa ni kurekebisha mapungufu na kukosoa upotoshaji, kwa nini wasianzie kwenye tofauti zao kwanza?

Halafu lengo la mada hii sio kutetea mafuta, mimi sio mwamini wa mafuta wala maji. Lengo la mada ni kuweka wazi kilichotokea mbali na kile wengi walikuwa wakiaminishana. Kuondoa upotoshaji na kuisema kwelinya tukio, lakini inapokuja kweli ya Mungu, mimi nami nina imani yangu

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Mungu ni Boss wa maboss wote; haulizwi kwanini, huo ni utovu wa nidhamu. Chukua neno hili la Biblia;;;.WATU WANGU HUANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA''. Maarifa ni kulifahamu neno sahihi la Mungu
Ndivyo lilivyokuwa swali nililojibu. Soma biblia

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Wewe unaandika hivi sababu hujafiwa. unatetea imani yako na mwamposa tu.

Kibwetere na mwamposa hawana tofauti. kesi yao ni ileile KUDANGANYA kwa kutumia imani na KUTENGENEZA MAZINGIRA yaliyosababisha vifo.

Kibwetere alitumia bible kuona mwisho wa dunia, mwamposa anatumia bible kutibu HIV, mimba, kuwapa wa2 utajiri, nk.

Hivi unafahamu sehemu kubwa ya waliokufa kwa mwamposa ni WATOTO na KINAMANA? Mwanamme mtu mzima aliekufa ni mmoja tu. Utawekaje WATOTO na WAGONJWA wakanyage mafuta katika mazingira yale?

Hivi unafahamu mwamposa kaua WATOTO na KINAMAMA au unatetea tu? Kwa nini WATOTO na KINAMAMA ambao kati yao ni WAGONJWA wasingepewa mafuta kwa njia nyingine?

Kuanzia sasa usiseme mwamposa kaua WATU, sema kaua KINAMANA, WATOTO, WAGONJWA. Nadhani ukisema hivi itakusaidia kujua kosa lake. Ile ni stampede ya wanaume wenye nguvu kuua KINAMAMA na WATOTO kati yao WAGONJWA. Mwanamme mtu mzima kafa mmoja tu!!!
Sijui hata umeandika kitu gani. Kudanganya kwa kutumia imani, weka ushahidi hapa tuone.

Kutumia imani kutengeneza..... sijaona hoja ya maana mpaka sasa. Weka vigezo vya tuhuma hizo

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
"Mungu" wakati anamuumba "Shetani" alikosa ishara kuwa "Shetani" atakuja kuleta "matatizo"?
Vipi wakati anaumba ulimwengu, hakupata ishara kuwa kutakuwa na " natural calamities" kama matetemeko ya ardhi na milipuko ya volcano?
Kama "Mungu" alishindwa kupata ishara hakuna ajabu lolote Mwamposa akishindwa kupata ishara.
[emoji2297]
maelezo yatakua mengi.
Mwamposa...Tufanye umeshinda basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui hata umeandika kitu gani. Kudanganya kwa kutumia imani, weka ushahidi hapa tuone.

Kutumia imani kutengeneza..... sijaona hoja ya maana mpaka sasa. Weka vigezo vya tuhuma hizo

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Mkuu kama UNAAMINI hayo mwamposa anayosema kuhusu mafuta yake na keki zake basi niachane nawe kiupole kabisa maana hatutafikia muafaka.

We ubaki na imani yako na mm nibaki na yangu. Ila kumbuka roho za wale wanawake, watoto na wagonjwa waliopambana kukanyaga mafuta hadi umauti!!!
 
Back
Top Bottom