Mtume Mwamposa na jaribu la imani

Mtume Mwamposa na jaribu la imani

Pole ww unaeamini kila anaelitaja jina la Mungu.Nabii wa kweli hawezi kimbia maiti. Na Mungu hawezi ruhusu watu wafe kwenye madhabahu yake wakati walienda kumuomba. Huyo Mwamposa ni Devil worshiper hana uhusiano wowote na Mungu wa kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
unaongea na mimi au anaongea na simu??

Mwamposa ni tapeli full stop.
 
Nyenyere,

Uwanja unabeba watu 10,000 na una mageti 8 unaweza kuniambia sababu zilizomfanya afungue geti moja pekee

Kwa hali why tusilifananishe na tukio la kibwetere la Uganda

Then umezungumzia kuhusu theology unajua elimu hii inasema nini kuhusu huu uongo wa hawa wanajiita mitume na manabii?

Unapozungumzia mafuta mafuta kile kitu ni sacred ni kitakatifu kama kitu ni kitakatifu unaweza kukimwaga chini chini ili watu wakanyage?.....unajua tafsiri ya kukanyaga kitu ni ishara ya dharau na kukikosea kitu thamani

Alafu unatuaminisha mafuta ya upako kitu kitakatifu kinatunzwa na kama wangekuwa kweli wanaelewa wasingekikosea heshima hivi.....sababu hii ilitosha kabisa kuona huyu ni MUONGO na TAPELI

Kwa kanisa katoliki mafuta matakatifu ya Krisma yanatumika mwaka mzima yanayobaki HUZIKWA kwa heshima maana ni kitu kitakatifu

Tusitetee uongo elimu haitoshi tu kutuondolea ujinga pia itongezee maarifa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hamtaki kusema tu lakini Mwamposa ni tapeli Wa kidini hawamubili Yesu wanahubili mafuta

Sent using Jamii Forums mobile app
Sikatai wala sikubali. Imani ya mtu ni kitu tofauti sana kwa sababu huyo Yesu unayemhubiri wewe ukijiona sahih wengine watakuita kanjanja na tapeli pia. Ndio maana huwa nasisitiza imani sio kitu cha kundi, ni mahusiano binafsi na muumba. Sasa unamchuuliaje muumba wako, hapo ndipo utakuta wazee wa leso, sabuni za upako, asali ya upako, udi na ubani, maji ya baraka, rozali, scapulali, kuheshimu msalaba, mkao wa ubwabwa, sigda n.k. Katika hayo kosa la Blldozer ni lipi?

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Uwanja unabeba watu 10,000 na una mageti 8 unaweza kuniambia sababu zilizomfanya afungue geti moja pekee

Yaweza kuwa vyombo vya mafuta na pia walitarajia utaratibu wa kupanga mstari lakini watu wakavamia kila mmoja anataka awe wa kwanza. Tuliza kichwa mkuu.

Kwa hali why tusilifananishe na tukio la kibwetere la Uganda

Kibwetere alikuwa na mahubiri na mafundisho tofauti sana mkuu, ndio maana nikahoji, kuna tatizo gani kwenye hayo mafundisho ya Mwamposa in relation to the incidence? Hoja iko hapo, mihemko pembeni. Ya kibwetere hata teolojia yake haikuwa salama kwa wanadamu, sasa teolojia ya Mwamposa ina tatizo gani kiusalama? Tuache chuki binafsi.

Then umezungumzia kuhusu theology unajua elimu hii inasema nini kuhusu huu uongo wa hawa wanajiita mitume na manabii?

Mimi ni mpingaji namba moja wa teolojia. Hii ni elimu ya kum-define Mungu kwa mtazamo wa mtu ama kikundi cha watu. Huko ndiko huzaliwa viu kama statement of faith. Ni mambo haya yabteolojia yaliyoingiza imani potofu kwenye kanisa, ibada ambazo hazina sapoti ya biblia. Kumbe basi natazama Neno la Mungu zaidi kuliko kusikiliza mwana teolojia amesema nini.

Unapozungumzia mafuta mafuta kile kitu ni sacred ni kitakatifu kama kitu ni kitakatifu unaweza kukimwaga chini chini ili watu wakanyage?.....unajua tafsiri ya kukanyaga kitu ni ishara ya dharau na kukikosea kitu thamani

Ni wapi imeandikwa mafuta ni matakatifu? Mafuta yatabaki mafuta tu, ila kwa imani watu huamini kilichonenwa juu ya mafuta hayo kitawapa matokeo. Kumwaga chini? Hapa sijakuelewa mkuu, mafuta huwekwa kwenye vyombo ili watu wakanyage, miguu ikiwa sehemu ya mwili.

Nachelea kuongea sana kwa sababu mimi pia siamini katika mafuta ila najenga tu hoja kwamba watu wanamhukumu Mwamposa kwa kufuata hisia binafsi juu ya huduma yake. Hakuna sehemu kwenye biblia inaposema ukimwaga mafuta mwenye vyombo watu wakanyage ni dharau.

Alafu unatuaminisha mafuta ya upako kitu kitakatifu kinatunzwa na kama wangekuwa kweli wanaelewa wasingekikosea heshima hivi.....sababu hii ilitosha kabisa kuona huyu ni MUONGO na TAPELI

Yesu aliponya kwa mate, nadhani ungekuwepo enzi hizo ungempiga mawe. Tatizo lako unadhani Mungu anaangalia heshima za nje ambazo kimsingi ni unafiki mkubwa, Mungu anaangalia ROHO YAKO. Hili ndilo lilipelekea Mungu kuwekwa kwenye vyombo makanisani pia, akatunzwa sakaristia. Matokeo yake wengine kama kina Bulldozer wamemweka kwenye mafuta, kwa nini basi uwanyooshee kidole?

Kwa kanisa katoliki mafuta matakatifu ya Krisma yanatumika mwaka mzima yanayobaki HUZIKWA kwa heshima maana ni kitu kitakatifu

Tusitetee uongo elimu haitoshi tu kutuondolea ujinga pia itongezee maarifa


Sent from my iPhone using JamiiForums

Elimu itakupa maarifa ni kweli, lakaini maarifa ya dunia hii. Elimu ya Mungu itakupa ujuzi wa ufalme wa mbinguni. Hakuna chuo cha teolojia kina uwezo wa kufundisha hili zaidi ya mashindano ya doctrines kwamba kwa nini sisi tunaamini hivi na wao wanaamini vile.

Kumbuka tangu kale na HATA SASA Mungu alivichagua vitu vinyonge na vidhaifu ili kuviaibisha vikubwa na vyenye nguvu. Unaielewa hiyo?

Kama maprofesa wanakwenda kunywa kikombe cha babu, ama kukanyaga mafuta ya upako, yako wapi maarifa hayo unayosema? Elimu ya Mungu itabaki kuwa hivyo na ya dunia kadhalika.

Kuhusu kuzika vitu vitakatifu, Mungu wa leo hakai kwenye vitu bali akaa kwenye roho zao wamtafutao kwa bidii. Habari za ukigusa hostia utapatwa kichaa sio biblical bali ni mafundisho ya kibinadamu. Tusimshushe Mungu wetu hivyo, tumheshimu kama alivyotaka. Ndio maana leo hii hatuendi kuhiji Israeli kwa sababu hakuna tena ya kuabudu mlima huu wa ule.

Tusome biblia.


Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Ni makosa makubwa kuwaaminisha wau kuwa tukio la mwamposa inashabihiana na lile la Kibwetee wa Uganda. Hii ni namna ya kutafuta kushambulia imani nyingine kwa mgongo wa nyuma na ndipo hoja za wenye imani tofauti zilipojikita. Mpaka sasa sielewi ni kwa vipi tukio la Moshi limefanana na lile la Kibwetere. Ni uongo na uzushi mkubwa

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk

Mkuu umedadavua vizuri ila kuna wakati unajichanganya. Unasema ni makosa kumfananisha mwamposa na kibwetere. Mi sioni tofauti zao. Wa mwamposa wanaona wa kibwetere potofu na wa kibwetere wanaona wa mwamposa potofu. Wote wameruhusiwa na mamlaka za nchi zao kueneza neno. Mimi naona wote wawili ni potofu.

Kibwetere alifunga milango ya kanisa waumini wakateketea. Mwamposa kuweka mafuta kwenye mlango wa geti moja maelfu ya waumini wapite wakikanyaga, wakafa. Kwangu mimi sioni tofauti. Yote ni makosa yatokanayo na kukosa busara ya kimungu.

Wewe mwenyewe umeweka swali "Mwenye jukumu la kupima usahihi wa mafundisho ni nani hasa linapokuja suala la imani?". Sasa kama unaona ni ngumu kupima usahihi wa mafundisho ya kiimani, ni kwa nini unabeza imani ya kina kibwetere? Kubali kila mtu abaki na imani yake. We unaona ya mwamposa sawa, kibwetere anaona yake sawa, mi naona ya wamposa na kibwetere si sawa ni utapeli, bali imani yangu ndio sawa.

Kwa kifupi hautafanikiwa kutetea usahihi wa imani ya mwamposa, achilia mbali kumuondoa kwenye hatia ya vifo vilivyotokana na aliyofanya.

Na ni bora baada ya hii kesi ashauriwe aachane na jina "bulldozer". Ame bulldoze watu to death!!!
 
Nyenyere,
Umejibu vizuri ila swali la mwanzo kuhusu kuweka mafuta mlango moja kati ya milango nane hujalijibu vizuri. Vipi tuendelee kusubiria majibu au tuomboleze kwanza?
 
Mimi naona chanzo Cha vifo Ni mafuta yaliyomwagwa.
Yawezekana hakukusudia watu wafe lakini chanzo Ni hicho brother.

Halafu baada ya Hilo tukio kwanini aliondoka?
Kwanini akimbie na wakati tukio limetokea katika kongamano lake?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msijifanamishe na Yesu ninyi ni binadamu wa kawaida zaidi ya ukawaida wenyewe,KASOMENI,tafuteni ELIMU,mshikeni sana ELIMU,
unvyosema Yesu hakuanzisha chuo mbona hausemi Yesu hakuanzisha kukanyagisha watu mafuta,
Afu skieni bana acheni kujitutumua kwa kujidai mnafanya aliyofanya Masihi,km ndo mnavyofnya mbona mmekimbilia kuwazika marehemu na hamkuwafufua km Yesu alivyomfufua Lazaro ama Paulo alivyofnya?
Jifunzeni kujinyenyekeza siyo kunyenyekewa,utumishi wa kujipa mbaya
Nimekuwa nikitafakari kile kinachoendelea kufuatia tukio la vifo vya watu 20 vilivyotokea huko Moshi kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa "Bulldozer." Baada ya tukio hilo kumekuwa na maoni mengi na mitazamo tofauti kwa ujumla kutokana na jinsi ukio hilo lilivyotokea, nami nimeona nitoe mtazamo wangu juu ya jambo hili.

Chanzo cha vifo ni kipi hasa?

Hapa nimeona nichambue kwa kina tatizo hasa ni nini. Kumekuwa na mitazamo hasi kuhusiana na chanzo hasa cha vifo kiasi kwamba kumekuww na hasira kali juu ya imani ya baadhi ya watu.

1. Je vifo vimetokana na mafuta?
Ukitafakari kwa kina utaona hili si kweli. Mafuta hayakusababisha hivyo vifo kwa sababu hayuko hata mmoja aliyetumia mafuta hayo na kufariki. Mafuta hayo yamekuwa yakikanyagwa mara nyingi, kwa miaka mingi pasipo kuwa na madhara kwa watumiaji.

2. Je vifo vimesababishwa na mafundisho?
Ni muhimu kupima mafundisho kama ndio chanzo hasa cha vifo hivi. Kwamba kile kilichohubiriwa siku hiyo ndicho kilichopelekea watu kukanyagana hata vifo kutokea. Kama siku hiyo waliambiwa watakuokuwa wa kwanza kukanyaga mafuta watapokea upako kiasi cha kuwalazimu waamini kugombania nafasi ya kwanza basi hilo ni tatizo. Lakini kama fundisho lilikuwa ni kwamba kukanyaga mafuta tu ni kupokea baraka, basi haijalishi kama ni wa kwanza ama ni wa mwisho.

3. Je vifo vimesababishwa na mafundisho potofu?
Hili ni suala pana kwa sababu limelenga mambo ya kiimani. Nilishangaa jana pale nilipomsikiliza waziri Simbachawene akielezea jinsi ambavyo huwa anaangalia baadhi ya mafundisho na kujiuliza kama kuna Mungu pale. Siamini kama ni jukumu la waziri kupima wapi pana Mungu wa kweli na wapi hapana Mungu.

Mwenye jukumu la kupima usahihi wa mafundisho ni nani hasa linapokuja suala la imani? Nimesikia hoja yabkuwa na wahubiri wenye digrii ya teolojia. Je, ni sehemu gani kwenye Biblia ambapo Yesu alianzisha chuo cha teolojia ama kuagiza kianzishwe? Teolojia ni elimu ya kimfafanua Mungu KWA MTAZAMO WA ANAYEFUNDISHA. Hili ni tatizo. Tukifika hapo itabidi waprotestanti, wasabato, wakatoliki, moraviani, waanglikana na walutheri wakalishwe chini kuamua mafundisho yapi ni ya Mungu wa kweli. Itabidi tuamue teolojia ipi ni ya kweli na ndiyo hasa anayoikubali Mwenyezi Mungu.

Labda tujiulize mafundisho potofu ni nini? Hapo ndipo penye mgogoro na si vinginevyo. Sisemi haya kutetea mambo ya mafuta na maji ya upako, hasha. Nasema kwa sababu naona suala hili linachukua mkondo wa kidunia zaidi, kumpima Mungu kwa elimu ya kidunia wakati kumbe elimi ya Mungu wala haichangamani na hiyo.

4. Je, vifo vimesababishwa na usimamizi mbovu?
Nadhani hapa ndipo penye tatizo. Kilichotokea ni wazi kuwa ni usimamizi mbovu, ama uzembe kwenye kusimamia uendeshaji wa tukio la kukanyaga mafuta. Habari ya kwa nini watu wanaamini katika mafuta haina uhusiano hata kidogo na vifo hivyo. Ni sawa na kuhoji kwa nini watu wanaamini katika mkate na divai, ama katika kuchoma udi n.k. Tatizo liko kwenye utaratibu wa waamini kukipata kile wanachokiaminia.

Mambo ya kiimani yanabaki kuwa juu ya mhusika mwenyewe, hivyo ni ujinga kumwona anayeamininhayo kuwa mjinga. Nikutafuta kuwaingizia wengine imani yako kwa lazima, hivyo kuondoa maana ya uhuru wa kuabudu bila kuvunja sheria. Kama sheria imevunjwa, sio sheria ya kukanyaga mafuta bali sheria ya kushindwa kusimamia kusanyiko kwa usalama.

Hivyo basi hoja yangu imelenga kuonyesha kuwa sio sahihi kuanza kushambulia imani ya watu kwa vigezo vya nini sisi wengine tunakiamini, bali yatupasa kuwafundisha uzuri wa imani zetu na ubaya wa imani yao ili waamini habari zetu waachane na hayo yao.

Ni makosa makubwa kuwaaminisha wau kuwa tukio la mwamposa inashabihiana na lile la Kibwetee wa Uganda. Hii ni namna ya kutafuta kushambulia imani nyingine kwa mgongo wa nyuma na ndipo hoja za wenye imani tofauti zilipojikita. Mpaka sasa sielewi ni kwa vipi tukio la Moshi limefanana na lile la Kibwetere. Ni uongo na uzushi mkubwa wa wenye kuishambulia imani.

Nawasihi utafakari kwa kina tatizo lilipo, tuachane na mihemkoa bali tuwe wakweli kwani kweli itatuweka huru.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati huo huo huwa wanaaminisha watu kuwa wanaongozwa na kulindwa na mahali walipo pana nguvu na ulinzi wa Mungu,
Waache kulitaja burebure jina la mtakatifu azidiye utakatifu
Prophet -a person regarded as an inspired teacher or proclaimer of the will of God.

awali ya yote ; imekuwaje Nabii Mwamposya asipewe ishara na Mwenyezi Mungu kwamba haya yatatokea...?



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali jingine,
Ni kweli uwepo wa Mungu ulikuwepo pale km wanavyojidai?
Mkutano kwa yaliyotokea unaonesha ulikuwa na kibali cha nani,muuaji ama mponyaji,
Mungu ama shetani?,
Utaskia oooo katika ulimwengu wa roho!!!
Ndio maana nimemjibu pia kuwa ni sawa na kumtuhumu Mwenyezi Mungu kutotoa ishara.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom