mgen
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 22,631
- 8,417
Msimamo wa Yehova kuhusu ibada za watu wa mataifa (wapagani)
Kulingana na mafundisho ya Biblia tukufu, msimamo wa Yehova au Allah (s.w.) kuhusu ibada za watu wa mataifa au wapagani, ni "ubatili", ni "chukizo" na ni "najisi" tupu. Msimamo wake huu unathibitishwa na maandiko yafuatayo ya Biblia tukufu kama yalivyomkariri Yeye mwenyewe (Yehova au Allah s.w.) akisema:
"BWANA anasema hivi, Msijifunze njia ya mataifa, wala msishangae kwa sababu ya ishara za mbinguni, maana mataifa hushangaa kwa sababu ya ishara hizo. Maana desturi za watu hao ni ubatili; maana mtu mmoja hukata mti mwituni, kazi ya mikono ya fundi na shoka". (Yeremia 10:2-3).
"Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo, kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote; na hiyo nchi imekuwa najisi, kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa. Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu; kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi... kwani mtu awaye yote atakayefanya machukizo hayo mojawapo, nafsi hizo zitakazofanya zitakatiliwa mbali na watu wao. Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili kwamba msifanye kabisa desturi hizi zichukizazo mojawapo zilizotangulia kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo, mimi ndimi BWANA, Mungu wenu". (Mambo ya Walawi 18:24-30 ).
"Na wa mataifa BWANA aiwaambia wana wa Israeili, msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao..." (1 Wafalme 11:3)
"Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua". (Mathayo 7:6).
Kwa uchache, huu ndio msimamo halisi wa Yehova kuhusu ibada za watu wa mataifa au wapagani; kwamba ni chukizo, najisi na ni ubatili mtupu kwake (Yehova).
Mnatia aibu kwenda kula denda jiwe kila mwaka mnakufa