Mungu kwenye Quran kusema kwamba Jua hutuama kwenye kisima cha matope mazito alikuwa na maana gani?

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,320
Quran inasema kwamba jua hutuama kwenye kisima ama dimbwi la matope kazito na asubuhi huamka.

Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Ta'ala kwenye Quran kupitia Sura al-Kahf (18: 83-86), inaeleza kwamba Jua huchwea katika chemchemu ya matope meusi mazito(dark Muddy spring):

“83-Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake.84 -Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu.85 - Basi akaifuata njia. 86 - Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.”

Nimeuliza hivyo kwasababu Sayansi ya Dunia inatuambia kwamba Jua liko mahapa pamoja ila Dunia ndio hulizunguka hivyo halina kuzama wala kuibuka.

Je, mwenyezi Mungu SWT alikua na maana gani kusema hivyo?

Ahsante.
 
Huyo Dhur Qarnain,ndio aliona jua,soma vizuri aya.
Kwanini na unadhani na "Mungu" amliipokea hivo hivo information ya huyo bwana,je si kusema naye "Mungu" anaamini jua huzama matopeni?
Hiki ni kisa,kinasimuliwa,kwa msimuliaji,ndio anaelezea kuhusu huyu aliyeona jua likizama. Hiki kisa kimekuja katika lugha ya kiarabu, kila lugha huja na utamaduni wa wenye hiyo lugha, ukitafsiri kuleta lugha nyingine,inatakiwa anayetafsiriwa kwa hiyo lugha, ajuwe utamaduni wa lugha husika, kwa mfano wazungu, kuna KUOA, hakuna kuolewa, mwanamke anaoa na mwanamme, anaoa, Mwanamme atamuuliza mwanamke "Will you marry me"(je utanioa?), kwenye kiswahili kuna kuolewa na kuoa,mwanamme haolewi, anaoa.
 
Aliyeona jua linazama kwenye matope ni huyo dhul Qarnain na si MUNGU.

hapo MUNGU anamsimulia muhammad ambaye hakuwepo wakati tukio linatokezea.

Yalaumiwe macho ya DHUL QARNAIN

Mwisho wa uelewa wangu
DHUL QARNAIN ni nani?! hadi Mwenyezi Mungu aliyeumba mbigu na dunia na vyote vilivyomo amsimulie Muhamad uongo wake?? Au kulikuwa na maana nyingine?! maana ni kituko.
 
Hakuna cha kutuama , Mungu sijui nini, ni mastory ya watu tu! Muulize Einstein atakwambia ukweli wa ulimengu ukoje. Haya mengine achana nayo!
Kila lugha huja na utamaduni wa lugha husika.Huyo anayesimuliwa kisa chake,anaitwa Dhur Qarnain,ndio yeye aliyeona jua.Lugha zote duniani,zinaambatana na utamaduni wa lugha husika, kwa mfano katika kiarabu,hakuna baba mkubwa,awe mkubwa wa baba ako,kila baba,hata awe mkubwa wa baba anakuwa ni baba mdogo.Mama vile vile,hata awe ni mkubwa wa Mama aliyekuzaa ni mama mdogo.

Upande wa wazungu,hakuna kuoa,kuna kuolewa,mwanamke anaolewa na mwanamme anaolewa.Mwanamme atamuuliza mwanamke,"Will you marry me?"(utanioa?).Kwa wazungu mwanamme,anaolewa na mwanamke anaolewa.Ukitafsiria kutoka lugha nyingine,mpaka ujuwe utamaduni wa lugha husika.
 
DHUL QARNAIN ni nani?! hadi Mwenyezi Mungu aliyeumba mbigu na dunia na vyote vilivyomo amsimulie Muhamad uongo wake?? Au kulikuwa na maana nyingine?! maana ni kituko.
Muhammad aliulizwa na hao wageni waliomtembelea juu ya huyo bwana dhul qarnain

Muhammad hamfahamu dhul qarnain kwa sababu waliishi nyakati tofauti ndipo akasimuliwa kupitia aya

Mbona hizo aya ipo wazi

83-Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake.
 
Kwanini na unadhani na "Mungu" amliipokea hivo hivo information ya huyo bwana,je si kusema naye "Mungu" anaamini jua huzama matopeni ?
Hiki ni kisa kinasimuliwa,ukisimulia kisa chochote,utaeleza vile kilivyotokea.Kwa mfano mtu asiyeona vizuri,atakapo ona kitu,itakuwa tofauti na mwenye macho mazima,kikiwa kitu hicho kiko mbali,na alipo.

Msimuliaji,wa maelezo ya asiyeona mbali,atasimulia vile,yule alivyoona,hata kama aliona kimakosa.
 
D5B801C5-FC3F-446F-9CE6-5A3784C04A74.jpeg


Watu huko kwenye science world wametuma chombo kwa jina (Parker Solar Probe) kimenasa kwenye orbit ya jua kinalizinguka kulisoma. Kumbuka jua alipo stationary na lenyewe linatembea kwa hivyo wanaenda nalo chezea mzungu.

Moja ya vitu wanavyotaka kuvielewa ni solar flares zina impact kubwa sana (uharibifu) kwenye miundombinu ya umeme ambayo inaweza kuleta athari kubwa sana ya power cuts.

Sasa watu hilo jua lenyewe wanalizunguka, wanaelewa elements zinazofanya liwe moto, halafu bado tu kuna mtu anasikiliza hadithi kutoka vitabu vya dini kuhusu how the universe work that is beyond me.

Copernicus mtu wa kwanza kubaini dunia ndio inalizunguka jua, not vice versa kama church ilivyokuwa inahubiri; alikuwa priest. George Lemaitre alieleta theory ya ‘Big Bang’ was a priest.

Ifike mahala as human beings common sense has to prevail, and not sticking to religious ideologies wakati the facts are out there.
 
Kila lugha huja na utamaduni wa lugha husika.Huyo anayesimuliwa kisa chake,anaitwa Dhur Qarnain,ndio yeye aliyeona jua.Lugha zote duniani,...
Umeandika vema kabisa, very very true.....I am sorry Nashindwa kupata connection! Issue ni ulweli wa kilichoandikwa na mleta thread/post!
 
View attachment 2488686

Watu huko kwenye science works wametuma chombo kwa jina (Parker Solar Probe) kimenasa kwenye orbit ya jua kinalizinguka kulisoma. Kumbuka jua alipo stationary na lenyewe linatembea chezea mzungu...
Tatizo ni kutafsiri kutoka lugha ya kiarabu kuja kiswahili.Kisa kinasimuliwa kuhusu huyo aliyeona jua kuzama.Yeye huyo anayesimuliwa kisa chake, ndio yeye aliona jua kuzama.Kila lugha ina uandishi wake, kutegemea na lugha husika.

Ukisoma, tafsiri kutoka lugha moja kwenda nyingine,inatakiwa ujuwe utamaduni wa lugha husika,katika kiswahili, mtu aliyekuzidi umri, huwezi kumwamkia kwa kumwambia habari yako, lakini kwa wazungu na lugha nyingi duniani, hazitofautishi katika kuamkiana,akiwa ni baba yako,mama yako,mkubwa wako, wote ni "How are you".

Kujuwa utamaduni wa lugha iliyotafsiriwa ni muhimu.
 
Back
Top Bottom