Mtukufu Rais bora tu angeandika R.I.P

Mtukufu Rais bora tu angeandika R.I.P

Mbona marais wa nchi nyingi duniani tena nchizilizoendelea hawajui iyo lugha. alafu sisi uku mtu asipo ongea iyo lugha anaonekana hamna kitu. Ama kwahakika mleta mada unanishangaza, tena unawezakuta una elimu ya shahada au zaidi. Warusi, Wachina, Wajerumani wafaransa wakuuwao hawaongei iyo lugha. sasa uki kwetu ikikosewa sentensi basi ni mjadala mwaka mzima.

Apa ndipo ninapo pata picha waajiri wanaposema wasomiwetu hawakidhi vigezo vya ajira. Unaweza kuta mleta mada ni mtumzima na ana familia lakini analo waza nikutafuta fulani kukosea wapi ili nipate kiki. Ebu tufanye kazi majungu hayajengi.
kinacho shangaza zaidi ngazi ya elimu aliyonayo na huko darasani ndio ilikuwa lugha ya kujifunzia
 
unakosoa halafu huweki wazi ingekuwaje sababu unajua kwa wengi hiyo sentensi inakwenda na inakubalika na amejiweka yeye pia kuonyesha uzito wake etc

Sasa naona mnatafuta tu kitu cha kupupua akili zenu, wewe unajua english iliyo vipande pande kabisa hata ukisoma haupati kujua mtu alitaka ongelea nini.

Naweza kubet na wewe ktk english haupo kivileeeeeeeeeee.

uatfikiri mnapata pesa, wavivu wakubwa, eti unakosoa lugha kabisaaaaaaa kama vile alizaliwa nayo hata kama hakuzaliwa nayo yupo vizuri. Msipende mtu aandike kufata mnayotaka, hajui kimondo ok SO!!!!?????

mtanyooka tu
Mkuu, niliwaji kuanzisha mjadala humumkuwa ikiwa Rais Magufuli ataamua kuwa bubu sijui hawa CHADEMA watakiwa na ajenda gani. Utafikiri hapa tunapimana uwezo wa kuandika kiingereza fasaha
 
Kwa tuliosoma science tunaona yupo sawa kwa sababu lugha zetu ni let x=tanzania
Assume jpm =tanzania
So tumwache afanye kazi
 
Bachellor tu ukikosea tu kuandika hiyo lugha watakuita kila jina, ki.la.za. mara division five sembuse Phd holder
Sio bure kunatatizo mahali

Na jeska, ndio ivyo tena kaonyesha uwezo wake. Gpa 1.6....

Naanza kupata mashaka na iq ya mfalme... Kukariri sio akili!

Bwana Yule wa kuita watu v.i.l.a.z.a kazi anayo, kweli hii mitandao inabidi malaika waifunge.

Ukweli utabaki kuwa ukweli ht watu wakifungwa midomo..
 
Maraisi wote wanajua Kiingereza?
Hapana. Ndio maana wengine wanatumia lugha za kwao kama wachina, wajapani nk. Sasa kwani ni lazima yeye atumie Kiingereza? Kuna shida hapa, huenda hajui kwamba hajui, na mbaya zaidi huenda pia hajui kwamba watz wengi wameshajua kwamba hajui!!! Nchi nyingi duniani zinajifunza kiswahili, sio dhambi akitumia kiswahili!
 
Mkuu angekuwa ameshawatumbua, mzee hayuko busy kama unavyofikilia, juzi alivyopiga simu live kwenye mkutano wa makonda nikajiuliza kumbe mheshimiwa naye anafuatilia ziala za makonda live.
Kama anapata muda wa kuangalia kipindi cha 360 clouds TV kila siku asubuhi kama alivyosema akipopiga simu atakuwaje busy mtu huyo?
Tukubaliane tuu ushamba umevamia Ofisi yetu tukufu na hatujielewi
 
AIBU HII TUNAIFICHAJE, KWA MFANO???

Kuna ubishi mwingine haufai, lazima tuambizane ukweli.. Wakati wa kumpongeza Rais-mchaguliwa wa marekani, Rais Magufuli aliandika 'broken English' kwenye ukurasa wake wa Twitter kwa nia njema tu ya kupongeza, nikashauri kuwa Ikulu waandaliwe watu wa kuandika kwenye mitandao ya kijamii kwa niaba ya Rais Magufuli, ili yasijirudie tena yale yale, kwasababu ni kuiaibisha taasisi ya Urais, na nchi kwa ujumla.

Kufumba na kufumbua, sijui tatizo ni uelewa au misimamo isiyokuwa na tija, bado 'broken English' imeonekana katika post ya Rais Magufuli alipotoa pole kwa kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Cuba, hayati Fidel Castro.

Wakati ule wa mwanzo kuna watu walisema kwa kumtetea kuwa kiingereza sio 'issue' sana, na kumficha Rais Magufuli kwa mwamvuli wa uzalendo kwamba kiingereza sio lugha yetu.. Lakini niliwaambia, katika moja ya hotuba ya Mwl. Nyerere wakati wa uhai wake aliwahi kusisitiza juu ya matumizi ya lugha ya kiingereza kuwa; kama Ghana wanajifunza, Kenya wanajifunza, Uganda wanajifunza, Mozambique, Malawi, etc. iweje Tanzania tuwe nyuma tusijifunze kiingereza? Mwl. Nyerere akasisitiza kwa kusema kuwa; Kiingereza ndiyo kiswahili cha dunia, ni lazima tukipe mkazo tujifunze na tukitumie, pamoja na kuwa lugha yetu ni kiswahili.

Sasa hili la Rais Magufuli kuandika 'broken English' kwenye ukurasa wake wa Twitter unaosomeka dunia nzima, ni aibu, na mbaya zaidi Rais Magufuli anatambulika kama Dr. Magufuli J.P. kwa maana mtu mwenye shahada zaidi ya moja, na shahafa hizo amezisoma kwa lugha ya kiingereza, na moja wapo ni kwenye chuo kikuu chenye hadhi ya kimataifa, chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM.

Ninashauri tena, Ikulu iandae watu kwa kazi hii, yeye kama Rais awape mawazo yake, wao wajue wanaandikaje, lakini kwa utaratibu huu, kwenye nchi ambayo watoto wa darasa la sita kwenye international schools wanazungumza kiingereza kumzidi mhitimu wa chuo kikuu, ni aibu kubwa, kwa taasisi ya Urais na taifa kwa ujumla.

Wako katika demokrasia na maendeleo
View attachment 440130
Wewe mwenyewe mbona umeandika kiswahili ambacho sio fasaha?
 
"unaishi nchini au ughaibuni mkuu?....tu nataka tuone kama tunaweza kuja kukumata ili tukufungulie mashtaka ya udhalilishaji maana umetutukana sana sisi wafanyakazi wa ikulu". kwa sauti ya mfanyakazi kilaza wa ikulu.
Na mimi nakuja na wanafunzi wote wale wa UDOM aliowaita jina hilo hilo. Patakuwa hapatoshi.
 
Mfuraishe Mfalme siku ya mwisho utaenda kunywa nae mvinyo

Kuna siku nilikua naangalia kipindi fulani, nadhani ilikua ile shughuli ya Waziri mkuu katika kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera. Kuna baadhi ya mabalozi waliongea kiswahili ingawa hakikua kimenyooka na bado tulielewa, vivyo hivyo wapo walioongea kiingereza cha ajabu na bado tuliwaelewa. Hatuko darasani kufundishana vitenzi, tunachoangalia ujumbe uliomaanishwa umefika.

Kuna vitu vingi vizuri vya kumshauri mkuu, vitavyoleta tija kwake na mwananchi wake ukiwemo wewe, mshauri afanyeje uchumi ustawi, mshauri afanyeje ajira ziongezeke, mshauri atapata wapi mapato ya kuendesha nchi, mshauri afanyeje wanavyuo wapate mikopo na hao wanaomaliza wapate kazi waweze kurejesha mikopo...leo hii tunapoteza muda kuongelea kitu kidogo sana (japo huu ni mtazamo wangu tu, na niweke wazi kuwa sifungamani na chama chochote cha siasa)
 
Huo n ujinga kutwa mnataka kumsema rais tu uyo n mwanasayansi na wengi tulio soma pcb na pcm tuna matatizo ya lugha
 
On behalf of myself and the country,

ni sawa kabisa. What are you complaing of?

Nadhani ingekuwa bora kulalamika kuhusu mantiki ya rais,kuliko kulalamika kuhusu mambo petty.

Kwani yule mtu alipojifunza chemistry,ilikuwa inafundishwa kwa lugha gani?

Ni kama katika BBC utamsikia Alan Kasuja anasema 'fast' badala ya 'first' and such errors. Lakini inaeleweka katika context ilivyotumika.
Wewe nawe walewale, kwa dizaini hii kweli elimu yetu dhaifu sana
 
Magufuli hajui Kiingereza na hilo halina ubishi ila nina wasiwasi kama hii akaunti ya Twitter huwa yeye ndiye mwandishi. Hii itakuwa inaandikwa na Msigwa au pimbi mwingine sababu simuoni Magufuli akikaa na kuanza kutupia mambo humo kwa sababu ya wingi wa hekaheka za kazi yake.
Lakini vyovyote vile iwavyo ni kweli kuna ushamba mwingi sana Ikulu sababu ya kujaza v-i-l-a-z-a.
Kila anachofanya huwa unamuona mkuu?

Au ukute aliyeandika niwewe ndiyo maana ukaja kutetea[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Rais wetu au mtu yeyote, asikosolewe kwa dhihaka bali kwa heshima na hekima. Ujumbe wa maneno aliyoandika unaeleweka kwa kila mtu anayejua kiingereza. Mbona watu wengi wanaoandika "Brocken Swahili" hawambiwi kwa maneno yenye ukakasi kama ya kwako? Tafadhali mkosoeni rais pale amavunja katiba ya nchi, sio vinginevyo. Rais hakuapishwa kuongea kiingereza unachotaka wewe.
 
Kuna siku nilikua naangalia kipindi fulani, nadhani ilikua ile shughuli ya Waziri mkuu katika kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera. Kuna baadhi ya mabalozi waliongea kiswahili ingawa hakikua kimenyooka na bado tulielewa, vivyo hivyo wapo walioongea kiingereza cha ajabu na bado tuliwaelewa. Hatuko darasani kufundishana vitenzi, tunachoangalia ujumbe uliomaanishwa umefika.

Kuna vitu vingi vizuri vya kumshauri mkuu, vitavyoleta tija kwake na mwananchi wake ukiwemo wewe, mshauri afanyeje uchumi ustawi, mshauri afanyeje ajira ziongezeke, mshauri atapata wapi mapato ya kuendesha nchi, mshauri afanyeje wanavyuo wapate mikopo na hao wanaomaliza wapate kazi waweze kurejesha mikopo...leo hii tunapoteza muda kuongelea kitu kidogo sana (japo huu ni mtazamo wangu tu, na niweke wazi kuwa sifungamani na chama chochote cha siasa)
some thread vzri
 
Maendeleo ni kubomoa Nyumba hovyo hovyo kwa kigezo cha kuwa na excavator za kubomolea.
Jengo la makao makuu ya tanesco lililojengwa na serikali hiyo hiyo ya cc em leo linavunjwa na serikali hiyo hiyo!!!!
Hawajali thamani ya hela zetu.

Hiv kiingereza ndo maendeleo? Hapo angeandika kiswahili tu ingetosha mbona wachina hawajui kiingereza na wanasonga? Wabongo kwa utumwa.
 
Back
Top Bottom