Mtukufu Rais bora tu angeandika R.I.P

Mtukufu Rais bora tu angeandika R.I.P

Ninaposema elimu yako aikusaidii siongopi apa tanzania tunajifunza kwakutumia kiswaili masomo karibuyote na bado kunawanafunzi wanapata F ya Kiswahili. Akija Mwingereza apa akikosea Kiswahili hamshangai!!!
Ila mswahili akikosea neno mmoja la Kiingereza mnamshangaa. Sasa apo kweli tuna akili?
 
Magufuli yuko sahihi kabisa sababu kaandika Tanzanian English...siyo lazima english ya tz iwe kama ya america au england,mbona nigeria wana english yao hata uganda pia..
 
Jpm yupo bise na kusoma MIKATABA yenu mlioingiza Hasara taifa letu,

Hizo ngeli zenu za kiingereza kwa sasa so kipaumbele chake bora ujumbe umewafikia hao watu wa CUBA kwanza hata wao wenyentewe kiingereza kinawasubua yann kutuumiza kichwa kwa sentensi ndogo Kama hiyo?
 
Anatutia aibu tuu, mbona hotuba zake hua anatoa kwa kiswahili sasa anashindwa vipi kutweet kwa kiswahili.
 
Kwa mbali naweza kukubali kuwa mheshimiwa kidogo lugha ni tatizo kweli, lakini hii ya kuandika broken English kwenye page najiuliza kweli ni yeye au kuna mchezo unachezwa, na kama kweli ni yeye kwani hana wasaidizi jamani....
 
Mungu wangu.......siyo kweli kabisa.Mimi siamini na tuache kumzushia Rais
 
Kwanza naamini umeelewa alichoandika,lakini pili unashindwaje kuonea aibu ufisadi,rushwa na uvivu uje uonee aibu lugha,tena lugha yenyewe sio yetu.
Tatu kiswahili chenyewe watu hukosea sana wengi husema kwa niaba yangu mwenyewe. Kitu ambacho kisarufi ni makosa.
Sasa alichofanya rais ni kutohoa kutoka kiswahili kwenda kiingereza.
Ni bahati mbaya sana mnatazama vitu visivyo na maana wala faida kwenye maendeleo
Tena usivyojitambua unaandika aibu.
 
Hiyo account angemuachia Mahiga aiendeshe yeye awe anampa input tu.....Mahiga anatema mayai barabara na shughuli hizo ndio zake haswaaa.
 
unakosoa halafu huweki wazi ingekuwaje sababu unajua kwa wengi hiyo sentensi inakwenda na inakubalika na amejiweka yeye pia kuonyesha uzito wake etc

Sasa naona mnatafuta tu kitu cha kupupua akili zenu, wewe unajua english iliyo vipande pande kabisa hata ukisoma haupati kujua mtu alitaka ongelea nini.

Naweza kubet na wewe ktk english haupo kivileeeeeeeeeee.

uatfikiri mnapata pesa, wavivu wakubwa, eti unakosoa lugha kabisaaaaaaa kama vile alizaliwa nayo hata kama hakuzaliwa nayo yupo vizuri. Msipende mtu aandike kufata mnayotaka, hajui kimondo ok SO!!!!?????

mtanyooka tu

Sikiliza mama yangu yule ni PhD holder wa udsm, sawa lugha hajaziwa nayo angeandika aliyozaliwa nayo basi kuliko kutia aibu namna hii kwani lazima aandike kikristo???
Hatujamuomba rais aandike tunavyotaka kapost kwenye social network broken english na tumeona halafu tupige makofi
Haya we endelea kuunga mkono hoja sisi ngoja tunyooke
 
Mkuu, niliwaji kuanzisha mjadala humumkuwa ikiwa Rais Magufuli ataamua kuwa bubu sijui hawa CHADEMA watakiwa na ajenda gani. Utafikiri hapa tunapimana uwezo wa kuandika kiingereza fasaha

Ha ha haaa watatunga

Halafu ameandika gazeti kwa kiswahili, sasa sijui kiingereza kashindwaje kukitumia

Ni kituko ha ha haaaa
 
AIBU HII TUNAIFICHAJE, KWA MFANO???

Kuna ubishi mwingine haufai, lazima tuambizane ukweli.. Wakati wa kumpongeza Rais-mchaguliwa wa marekani, Rais Magufuli aliandika 'broken English' kwenye ukurasa wake wa Twitter kwa nia njema tu ya kupongeza, nikashauri kuwa Ikulu waandaliwe watu wa kuandika kwenye mitandao ya kijamii kwa niaba ya Rais Magufuli, ili yasijirudie tena yale yale, kwasababu ni kuiaibisha taasisi ya Urais, na nchi kwa ujumla.

Kufumba na kufumbua, sijui tatizo ni uelewa au misimamo isiyokuwa na tija, bado 'broken English' imeonekana katika post ya Rais Magufuli alipotoa pole kwa kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Cuba, hayati Fidel Castro.

Wakati ule wa mwanzo kuna watu walisema kwa kumtetea kuwa kiingereza sio 'issue' sana, na kumficha Rais Magufuli kwa mwamvuli wa uzalendo kwamba kiingereza sio lugha yetu.. Lakini niliwaambia, katika moja ya hotuba ya Mwl. Nyerere wakati wa uhai wake aliwahi kusisitiza juu ya matumizi ya lugha ya kiingereza kuwa; kama Ghana wanajifunza, Kenya wanajifunza, Uganda wanajifunza, Mozambique, Malawi, etc. iweje Tanzania tuwe nyuma tusijifunze kiingereza? Mwl. Nyerere akasisitiza kwa kusema kuwa; Kiingereza ndiyo kiswahili cha dunia, ni lazima tukipe mkazo tujifunze na tukitumie, pamoja na kuwa lugha yetu ni kiswahili.

Sasa hili la Rais Magufuli kuandika 'broken English' kwenye ukurasa wake wa Twitter unaosomeka dunia nzima, ni aibu, na mbaya zaidi Rais Magufuli anatambulika kama Dr. Magufuli J.P. kwa maana mtu mwenye shahada zaidi ya moja, na shahafa hizo amezisoma kwa lugha ya kiingereza, na moja wapo ni kwenye chuo kikuu chenye hadhi ya kimataifa, chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM.

Ninashauri tena, Ikulu iandae watu kwa kazi hii, yeye kama Rais awape mawazo yake, wao wajue wanaandikaje, lakini kwa utaratibu huu, kwenye nchi ambayo watoto wa darasa la sita kwenye international schools wanazungumza kiingereza kumzidi mhitimu wa chuo kikuu, ni aibu kubwa, kwa taasisi ya Urais na taifa kwa ujumla.

Wako katika demokrasia na maendeleo
View attachment 440130
On my behalf..
 
Back
Top Bottom