Mtu binafsi anaweza kumiliki soko?

Itafaidika kwà kupata fedha za leseni ya biashara ya kuendesha na kumiliki soko.
Ndo kuandika barua kuomba kufanya hivyo Kisha uieleze jinsi itakavyo faidika .
ANGALIZO:
ANGALIA BAADA YA MIAKA KADHAA KUPITA ENEO HILO LIKAMILIKIWA NA HALMASHAURI YAKO KWANI MASOKO YOTE NI MALI YA HALMASHAURI.
 
Kwa jina la jamhuri.

Wakuu hivi kama nina kiwanja naona kimekaa sehemu nzuri naweza kukifanya kiwe soko? Yaani hapo kati nijenge au niwape watu wajenge meza za kuweka mambo ya mbogamboga, nafaka na vyakula vingine halafu pembeni nijenge furemu kuzunguka. Kama tu yalivyo masoko mengi.
Hapo nakuwa nachukua miatatu miatatu za wenye vibanda, miambilimiambili za chooni na kodi za maduka kwenye frem zinazozunguka.

Inawwzekana hii kitu, ishu za mipango miji zikoje?
Inawezekana kabisa. Jenga fremu kuzunguka kama uwanja, hapo katikati ndio wamama watakuwa wanaweka mazagazaga n.k

Usisahau milango mikubwa miwili ya kuingilia na kutokea pamoja na choo cha kulipia, choo 200, kuoga 500.
 
Soko ni mali ya umma. Kutaka kumiliki private ni kuvunja sheria( zipo sheria ) ni kam stendi au bus terminal! Labda uwauzie halmashaur walifany wao kuw soko
Mbona CCM huwa wanamiliki masoko. Halafu soko ni mkusanyiko tu wa magenge na fremu, mbona vikiwa kimojakimoja siyo kosa kuwa navyo, inamaana vikiwa vingi sehemu moja ndiyo kosa?. Hili la masoko kuwa mali ya umma ni sababu ya sera za kijamaa, bado zinafanya kazi?
 
Tengeneza frem au kodisha kishikaji, soko, stand, open space na vinavyo fanania na hivyo hizi ni Mali ya umma...

Umma ni pamoja na wewe... Soko likiwa karibu yako au eneo lako lina tazama soko basi nawe utapata fursa kupitia hapo lakini sio uanzishe...

Ukianzisha kuna kuja kuamisha soko au upewe fidia au wakupige marufuku kufanya soko
 
Baba yangu ni mfanyabiashara wakati soko linaanza wao ndo walikuwa waanzilishi miaka zaidi ya 25 iliyopita. Wao waliuziwa viwanja Yani kisehemu unajenga fremu mwenyewe, Wakawa wanalipa Kodi ya biashara halmashauri.
Magufuli alipoingia kawanyang'anya kasema eneo ni la CCM, wakapigiwa hesabu Kodi ya kulipa kila fremu kwa mwaka wanalipa hela inaenda CCM na fremu walizijenga wenyewe.
Hii nchi
 
Tengeneza frem au kodisha kishikaji, soko, stand, open space na vinavyo fanania na hivyo hizi ni Mali ya umma...

Umma ni pamoja na wewe... Soko likiwa karibu yako au eneo lako lina tazama soko basi nawe utapata fursa kupitia hapo lakini sio uanzishe...

Ukianzisha kuna kuja kuamisha soko au upewe fidia au wakupige marufuku kufanya soko
Mkuu mbona CCM huwa inamiliki open space kisha inawakodishia watu wanaoweka vibanda na kuwa soko, hujawahi ona hilo?
 
Baba yangu ni mfanyabiashara wakati soko linaanza wao ndo walikuwa waanzilishi miaka zaidi ya 25 iliyopita. Wao waliuziwa viwanja Yani kisehemu unajenga fremu mwenyewe, Wao walikuwa wanalipa Kodi ya biashara halmashauri.
Magufuli alipoingia kawanyang'anya kasema eneo ni la CCM, wakapigiwa hesabu Kodi ya kulipa kila fremu kwa mwaka wanalipa hela inaenda CCM na fremu walizijenga wenyewe.
Hii nchi
Poleni sana mkuu. Umeona kuwa CCM ni taasisi binafsi lakini inamiliki soko.
 
Mkuu mbona CCM huwa inamiliki open space kisha inawakodishia watu wanaoweka vibanda na kuwa soko, hujawahi ona hilo?
Mkuu kuna sheria zinafunga kumiliki hiyo kitu labda ufanye kama kamkusanyiko flan ka watu kujikwamua n u.skini siy mmilki kuwa mmoja.ashum kam hayo mabanda ya waliounda hilo kundi na mmeandika lengo la umoja huo kibiashara then, mmeamua kukodisha wat wengine kuendesha kwa malipo kwen. Nilion temeke pale sido kuna kama kiwanda kina jina moja lakin kila mtu ana biashar yake ndani ila wanalipa ushuru
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom