Mtu binafsi anaweza kumiliki soko?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,886
Kwa jina la jamhuri,

Wakuu hivi kama nina kiwanja naona kimekaa sehemu nzuri naweza kukifanya kiwe soko? Yaani hapo kati nijenge au niwape watu wajenge meza za kuweka mambo ya mbogamboga, nafaka na vyakula vingine halafu pembeni nijenge furemu kuzunguka. Kama tu yalivyo masoko mengi.

Hapo nakuwa nachukua miatatu miatatu za wenye vibanda, miambilimiambili za chooni na kodi za maduka kwenye frem zinazozunguka.

Inawwzekana hii kitu, ishu za mipango miji zikoje?
 
Ndio ila likishakuwa na manufaa watu wakawa wengi utakumbushwa kuwa ardhi yote ni mali ya JMT.

Kabla hujafanya biashara ambayo ipo wazi ila haifanyiki maswali ya msingi ya kujiuliza ni haya:

Kwann hii biashara haifanyiki na wengine?

Mm nina akili sana kuliko wengine wasioifanya?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom