Mtu asiyejulikana agawa fedha jijini Dar

Mtu asiyejulikana agawa fedha jijini Dar

Kwanini atembee na polisi je hao polisi wanajua source ya hizo pesa na vyombo vya usalama na wizara ya mambo ya ndani inafahamu hilo, kwanini hajakamatwa na kujitambulisha kwa wizara ya fedha, hayo mabilioni anabeba kws gari gani au ipo kwenye mifuko ya rambo, hizi habari ni utata tu, kuna aliepokea kitita cha huyo msela hapa JF atwambie!?
 
​

Bajaji wakiwa kwenye foleni kuwekewa mafuta na mtu ambaye hakutaka kujitambulisha

Mwanaume mmoja, ambaye amekuwa akiongozana na maaskari polisi wawili, amekuwa akigawa fedha za bure kwa watu mbalimbali jijini Dar.

Kijana huyo wa makamo, ambaye kwa wiki hii nzima amekuwa akitajwa kwenye radio mbalimbali, aliwalipia bili wagonjwa wote waliokuwa wamelazwa hospitali ya Mwanyamala na Muhimbili, wodi ya wanawake.

Akizungumza na mwandishi wetu,mmoja wagonjwa wa hospitali ya Muhimbili, Subira Juma alisema kijana huyo alikuja hospitali na kuuliza wangapi wanadaiwa halafu akawalipia bili zao na kisha kuondoka zake bila kujitambulisha.

‘Kwa kweli hata mimi sifahamu kijana huyu katokea wapi, lakini sijwahi kuona mtu akitoa hela bila kujuana, na kisha kuondoka bila kusema lolote
’ alisema Subira.

Wakati huo huo, wasafiri wa daladala nao, hasa ziendazo Mbagala nao wametajwa kunufaika na mgao huo, ambapo wamekuwa wakilipiwa nauli mara kadhaa na mtu huyo.

Mbali na kulipia watu usafiri, kijana huyo pia anatajwa kuwanufaisha madereva boda boda na bajaji kwa kuwawekea mafuta kwenye vyombo vyao vya usafiri.

CHANZO JAMBO TZ

Mwenyeezi Mungu amlipe Pepo huyo Kijana inshallah Wanachama Wenzangu Semeni Ameen.


Nyie endeleeni kushabikia vitu msivovijua....huyo anafanya ibada hapo ngojeni matokeo atapomaliza kiasi alichoambiwa kukitoa ...
 
Wajameenii HIYO ni Sadaka kuna mambo mengi katika zoezi hili:- Kuna KAFARA hutozwa kwa njia ya mgao na kuna Sadaka kwa njia ya magao, kuna Dhimaa, kuna Zawadi hutozwa kwa njia ya magao nk.
Hilo siyo jambo geni pokeeni na mtumie "'NO WORRY wandugu"
 
[/B]
Really? Are they poor to such extent?
Mkuu Honestly ukiwanazo na umejaaliwa full pochi kuwa KIND to others Especially to your countrymen !! "Charity starts at home" kweli tunao watu nchini humu hata hajui ml wa leo ataupata wapi ? haswa kuna familiya hazipendi kunyosha na kunyanywa mkono wa kuomba. " Tuwafikirie hao masikini ili nasiye tuiishi na tuengezwe zaidi " Good luck.
 
Kwel majanga... kama kwel hizo anazo gawa ni pesa halali kwanin asizigawe kwenye vituo vya watoto ya tima? Kusaidia shule zakata zipate vitabu? kuwa saidia watu wasio jiweze? n.k. namashaka sana na hizo pesa.. watanzania mnakubalishwa kuingia mikata msio ijua kipumbavu sana. Endeleeni kuwa part 2 the contract and later you wl hav 2 fulfill your parties too though mnaingia kichwa kichwa kwenye contracts msizojua terms zake zita wataka mfanye nini?????. Nothing goes for free as well as making money money... money making money. Kuweni makini navitu vyakupewa hata jackpot bingo hawatoi pesa kihivyo.
 
pesa za mashetani hizo
shauri zenu
mtakapoambiwa toeni sadaka kwa kula vya watu
mie sipo.
 
Dar sio sehemu sahihi pa kuanzia kutoa misaada ya kweli...hata viongozi wetu wanachemsha hivyohivyo!!!
tunajua mnataka media coverage na misukule!!
 
Yaani ukiwa mtu makini huwezi ukapokea pesa yeyote kama hii.
Lazima ujie chanzo cha hizo pesa na sababu za mgao wa bure.

Sawa kabisa mkuu, ila wabongo kwa kupenda vya bure utaonekana mbaya, mi ndo maana nikaamua kunyamaza kimya. ki msingi ndio hivo huwezi pokea pesa usiyo jua malengo yako au ilko tokea.
 
Back
Top Bottom