Mtu asiyejulikana agawa fedha jijini Dar

Mtu asiyejulikana agawa fedha jijini Dar

Tusiulize pesa yake imetoka wapi. Tusiulize dhamira yake ni nini? Tusihoji anachotarajia kupata toka kwetu kwani hatumjui na yeye hatujui. Sijanufaika na huo mgao, lakini walionufaika wamshukuru Mungu.

Pamoja na majanga yote yaliyopo duniani, anapotokea mtu wa ajabu kama huyu, hatuna budi kumshukuru Mungu, kwani haya ni matendo yake.

Labda mtu huyu alichuma sana duniani. Labda ameambiwa amebakiza muda mfupi wa kuishi duniani. Kauza mali zake alizochuma, kahakikisha ndugu zake wanaotamani mali zake (alizochuma kwa shida) ili wafaidi atakapoaga dunia. Wako matajiri wangapi ambapo katika siku zao za mwisho waliteseka sana, kisha wakaaga dunia pasipo kujisafishia njia yao huko waendako?

Kama ulichuma, halafu hutoi sadaka kwa Mungu, unatarajia utakapoondoka duniani, utakuwa mgeni wa nani? Nyumba yako ya baadaye itakuwaje? Hata huko kaburini, utahitaji vitu vya kuishibisha roho yako. Kuna chakula cha roho - nenda ukasali. Kuna mwanga wa roho - hujawanunulia watu mishumaa. Fedha hazina matumizi huko, ila katoe sadaka kwa yatima, wajane, maskini, wagonjwa.

Huyu kaenda kuwalipia wagonjwa bili zao. Hakujali kama wana uwezo wa kulipa ama la. Kalipa.

Kawalipia watu nauli. Hakuwauliza kama wanaweza kulipa au hawawezi.

Kawajazia wajasiriamali wa bajaj mafuta. Kawapunguzia gharama za kuendesha biashara yao hiyo ngumu.

TUNAMTAKIA UBAYA MTU MWEMA HUYU WA MUNGU ILI IWEJE?

Badala ya kumwunga mkono, nye wengine mnasema "Watanzania mjihadhari..." Tujihadhari na mtu anayetuletea sinia la dhahabu limesheheni kila aina ya vito vya thamani kisha yu aenda zake bila kusema neno lolote?

Wahenga walisema: Hakuna cha bure.

Lakini huyu ni Mtoa Sadaka. Alijisahau, sasa kaamua kumrudia Mungu. Wewe unayeona boriti machoni mwake, hujaona vibanzi vilivyopo machoni mwako?

Mrudie Mungu, muda bado unao. Hujui utaondoka lini. Hata mimi sina mkataba na Mungu! Sijui nitaondoka lini. Lakini kila fursa ninayoipata ya kumtumikia Mungu, NAITUMIA!
 

CHANZO: JAMBO TZ

My take:
Sina shida na huyo mgawa fedha ila nani anawapangia hili lindo hao askari polisi? Jeshi letu la polisi linatakiwa lifanyiwe ukarabati upya.

Kisheria mtu yoyote anaweza kwenda kituoni na kuomba ulinzi wa polisi akiwa na sababu za kuleweka kupewa huo ulinzi na sio lindo kama unavyosema wewe. Polisi wapo kulinda usalama wa raia.

Hata wewe MTENGETI ukitaka kupewa ulinzi wa polisi utapewa kama ukiwa na sababu inayoileweka na kujielezea kwako sababu za kuutaka huo ulinzi wa polisi. MTENGETI ijue haki yako na ulinzi wa polisi ni haki yako kama mtanzania na raia wa nchi hii au sio raia wa nchii hii pia una haki ya kulindwa na polisi

 
Kwa kuliangalia kwenye "dimension" nyingine inawezekana kuna Mtu anatoa sadaka. Kimsingi ugawaji bure wa "economic resource" yoyote siyo jambo endelevu!
 
Hela za bure!!!! Hakika waliozipokea imekula kwao!!!! Ni lini tutaachana na vitu vya bure kutoka kwa watu tusiowafahamu? Ingekuwa ni za utajiri basi matajiri tulio nao wangegawa!!! Tena tajiri siku zote ni mchoyo!!! Hizo imekula kwao!!! Subiri matokea watakuja hapa hapa kutoa ushuhuda wa yatakayowapata.

People should be careful. This is another babu of Loliondo. Hata hivyo anatakiwa achunguzwe vizuri kama anafanya kazi gani na kama amewekeza kwenye nini.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Askari wako makini kuhakikisha huyo jamaa hasogelewi na majambazi! Ila kuna swali la kujiuliza, "ni nani anawagangia kazi hao askari?" manake nijuavyo, maaskari wanapangiwa lindo hasa kwenye taasisi za fedha!

Mnasema mtu huyu asiyejulikana anagawa hela ; halafu mnasema huyu mtu analindwa na maaskari wawili!!! Kama asingejulikana angelindwa na askari?
 
Back
Top Bottom