Preta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 24,320
- 18,886
We are finished!
Me am not finished oooooh.........hebu nielekezeni nampataje huyo mahbubah........
We are finished!
Me am not finished oooooh.........hebu nielekezeni nampataje huyo mahbubah........
Njoo nikugawie laki nkamu ghwangu..
Sidhani kama jamaa angetaka akumbukwe angeficha jina lake watu wasimjue, ana mishe nyingine tu huwezi jua so usimjudge fasterfaster, huezi jua mtu anafikiria nini kichwani,Anatafuta sifa si akajenge zahanati vijijin au shule au vituo vya polisi akumbukwe daima
Kidogo nishangae, Preta hutaki hela?
Yaani mie inabidi ninunue kifaa cha kum-locate kila alipo
Mtu huyo ana lake jambo. Nchi nyingi ni makosa kugawa hela kwa mtindo huo ila hapa tz poa tu.Yaani ukiwa mtu makini huwezi ukapokea pesa yeyote kama hii.
Lazima ujie chanzo cha hizo pesa na sababu za mgao wa bure.
hahaaa umenichekeshaje,Me am not finished oooooh.........hebu nielekezeni nampataje huyo mahbubah........
Hii inshu ingekua Arusha sijui angeitwaje huyo mgawa VYEEEZA.
Usipende kulipiwa lipiwa matumizi yako na mwanaume mwenzako, ipo siku mtaombwa Mombasa halafu manze kutafutana. Hapa mjini bwana.
Bajaji wakiwa kwenye foleni kuwekewa mafuta na mtu ambaye hakutaka kujitambulisha
Mwanaume mmoja, ambaye amekuwa akiongozana na maaskari polisi wawili, amekuwa akigawa fedha za bure kwa watu mbalimbali jijini Dar.
Kijana huyo wa makamo, ambaye kwa wiki hii nzima amekuwa akitajwa kwenye radio mbalimbali, aliwalipia bili wagonjwa wote waliokuwa wamelazwa hospitali ya Mwanyamala na Muhimbili, wodi ya wanawake.
Akizungumza na mwandishi wetu,mmoja wagonjwa wa hospitali ya Muhimbili, Subira Juma alisema kijana huyo alikuja hospitali na kuuliza wangapi wanadaiwa halafu akawalipia bili zao na kisha kuondoka zake bila kujitambulisha.
Kwa kweli hata mimi sifahamu kijana huyu katokea wapi, lakini sijwahi kuona mtu akitoa hela bila kujuana, na kisha kuondoka bila kusema lolote alisema Subira.
Wakati huo huo, wasafiri wa daladala nao, hasa ziendazo Mbagala nao wametajwa kunufaika na mgao huo, ambapo wamekuwa wakilipiwa nauli mara kadhaa na mtu huyo.
Mbali na kulipia watu usafiri, kijana huyo pia anatajwa kuwanufaisha madereva boda boda na bajaji kwa kuwawekea mafuta kwenye vyombo vyao vya usafiri.
CHANZO JAMBO TZ
Mwenyeezi Mungu amlipe Pepo huyo Kijana inshallah Wanachama Wenzangu Semeni Ameen.