Mungu amemjalia maisha marefu mzee wetu huyu, mpaka sasa anaikaribia miaka 100.
Pamoja na kuwa tunasema ni kwa neema na kudra za mwenyezi Mungu lakini nina uhakika kuna mambo huwa anaepuka kuyafanya ama huyafanya kwa kiasi mpaka kuufikia umri huu.
Basi ni muda umefika mzee wetu aulizwe ili atupe mwangaza wa namna yeye anaishi. Atutajie kinagaubaga vitu anavyopendelea kuvifanya, chakula anachopendelea kula, na atuambie ni mambo gani hapendelei kuyafanya.
Badala ya kutegemea mambo ya vitabuni ambayo wakati mwingi huwa hayaendani na uhalisia ni vema tukachota maarifa kutoka kwenye kisima kinachotembea.
Wafuasi wa Prof. Janabi mpo?