Mtu aliye intelligent, mwenye exposure na street-oriented anipe ushauri

Mtu aliye intelligent, mwenye exposure na street-oriented anipe ushauri

Leverage

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2021
Posts
2,125
Reaction score
3,169
Mimi ni graduate niliyeajiriwa ila sioni future kwenye ajira kila nikiangalia mbele naona giza tu. Nilijaribu vibiashara lakini sioni mafanikio yeyote mpaka sasa nimeona labda nyota yangu haipo kwenye biashara. Nimejichanga kwa sasa Nina milioni 7.5

Katika kutafakari nitachomokaje kwenye maisha nimepata mawazo matatu:

1. Nitumie milioni 6 kusoma masters kisha nitafute kadi ya chama CCM ili nibahatishe uteuzi.
2. Niende Veta nikasome ufundi wa magari niingie mtaani kutafuta shilingi
3. Nizamie Ulaya nikabebe box.

Mtu matured na mwenye uzoefu wa maisha karibu kwa mchango wako.

Ahsante.
 
Japo Mimi ni kama wewe ila nakuomba utulize akili kwanza, soma mazingira then anzisha kitu ambacho unakipenda moyoni mwako. Usiangalie faida kubwa sana na utajiri wa haraka haraka, kusanya nguvu, na kubuni kitu ambacho kitakusaidia baadae.

Na kama unaekeza hakikisha unatumia robo au nusu ya hela uliyonayo maana biashara ni risk.
 
Kama umeshindwa na maisha jaribu dili zingine.
 
Dunia inaendeshwa kwa kanuni.Kama kulivyo na kanuni za physics pia kila kitu kina kanuni zake.Ukifanya jambo nje ya kanuni zilizopo hutafanikiwa kamwe.

Ili binadamu afanikiwe kwa urahisi na bila kutumia nguvu kubwa anapaswa kufanya shughuli yenye sifa moja au zaidi kati ya hizi:

1.Kipaji

2.Passion

3.Enthusiasm

Tafuta shughuli yoyote ambayo inaangukia kati ya nilivyotaja hapo juu kisha utafanikiwa kirahisi sana,bila kutumia nguvu kubwa na kwa ufanisi wa hali ya juu sana.Nimekupa kanuni ya bure,ni wewe tu ushindwe mwenyewe.
 
Hauna uvumilivu kwene kutafuta, biashara uloianzisha nafikiri ulikuwa ushajiekea malengo ya faida tu! Kaza buti kama unaamini katika Biashara utatoka tu cha muhimu uvumilivu na kusoma mazingira ya Biashara na aina ya biashara unayofungua
 
Huwezi kupata uteuzi wakati huna connection..Yan your father was no body and he knew somebody. Unaweza nunua vifaa automatic vya kuziba pancha na wheel alignment, Ukaondoka jijini ukaenda mikoani kwenye barabara kubwa za highway. Ukafungua goli lako hapo. Huwezi kosa kulaza 50 yako hapo kwa kuanzia
 
Japo Mimi ni kama wewe ila nakuomba utulize akili kwanza, soma mazingira then anzisha kitu ambacho unakipenda moyoni mwako. Usiangalie faida kubwa sana na utajiri wa haraka haraka, kusanya nguvu, na kubuni kitu ambacho kitakusaidia baadae.

Na kama unaekeza hakikisha unatumia robo au nusu ya hela uliyonayo maana biashara ni risk.
Well said...
 
Sina sifa ulizotaja Ila jaribu kwenda VETA. Mtu intelligent kwako ni masters kwenda juu au vipi!
 
Mkuu wakati mwingine ili mkono uende kinywani yakubidi ufanye hata jambo usilopenda
Ok,ushauri wangu angalia kitaa/mtaani kwako au mitaa mingine jirani kuna changamoto gani ya bidhaa au huduma then uitatue,au kama kuna mdau ameshafanya hilo wazo/biashara angalia number ya customers,kama wapo wengi pambana muwagawane,au uwachukue wote..hapa ushindani wa biashara utakuwepo so factors zngne km bei,ubora wa bidhaa,customer caring vitakuhusu...
 
Hauna uvumilivu kwene kutafuta, biashara uloianzisha nafikiri ulikuwa ushajiekea malengo ya faida tu! Kaza buti kama unaamini katika Biashara utatoka tu cha muhimu uvumilivu na kusoma mazingira ya Biashara na aina ya biashara unayofungua
Shida ni kwamba biashara ikifa nachukua muda mrefu sana kupata mtaji mwingine huku nikiugulia makato ya benki
 
Back
Top Bottom