Mtu akifa anaenda wapi?

Mtu akifa anaenda wapi?

Na vyote wanakuambia unavyo wewe ila kuvielewa mpaka wakusimulie wao waliosimuliwa😅
Fwatisha sara ya toba hii kama unataka kuokoka, MUNGU BABA Mimi ni mwenye ni mwenye dhambi naomba unisamehe dhambi zangu zote natubu kwa kumaanisha kuziacha kabisa, naomba liandike jina langu kwenye kitabu Cha uzima wa milele, ameni. Baada ya hapa itabidi ubatizwe. Upo mkoa gani?
 
Fwatisha sara ya toba hii kama unataka kuokoka, MUNGU BABA Mimi ni mwenye ni mwenye dhambi naomba unisamehe dhambi zangu zote natubu kwa kumaanisha kuziacha kabisa, naomba liandike jina langu kwenye kitabu Cha uzima wa milele, ameni. Baada ya hapa itabidi ubatizwe. Upo mkoa gani?
Mwombe huyo Mungu akufundishe kuandika kwanza

Fwatisha , sara ni kitu gan🚮
 
Kitabu cha Henoko naonaga hakina hata mashiko.
By the way tupe ka summary akiii 😁
 
Kwenye Imani yetu,tukifa tunaenda peponi na kugawiwa mademu wenye macho makubwa 72 wote bikra.Pembeni ya vijito tunajilaza huku tunabugia mvinyo bardiiiii na kusikiliza kaswida mwororooo!
Bikra ni kwa watu wema washenzi washenzi watakula kuni za moto
 
Swali hili limekuwa ni kitendawili kwa wanadamu wote: Mtu akifa, anaenda wapi?

Maandiko ya kale ya Henoko 22:18–26 yanatupa picha nzito ya safari ya roho baada ya kifo. Hebu tusome kwa pamoja:

18 Kutoka hapo nikaenda mahali pengine, mlima wa mwamba mgumu.

19 Na ndani yake palikuwa na mashimo manne, makubwa na mapana na laini sana. Mashimo hayo yalikuwa laini mno, makubwa na yenye giza kuonekana.

20 Ndipo Rafael, mmoja wa malaika watakatifu aliyekuwa pamoja nami, akaniambia:
“Mashimo haya yameumbwa kwa kusudi hili, kwamba roho za nafsi za waliokufa zikusanyike humu, naam, kwamba roho zote za watoto wa wanadamu zikusanyike hapa. Na mashimo haya yamefanywa kuyapokea hadi siku ya hukumu yao na muda wao uliowekwa, mpaka hukumu kuu juu yao itakapofika.”

21 Nikaona roho ya mtu aliyekufa ikileta malalamiko, na sauti yake ikaenda mbinguni ikiwasilisha kesi. Nikamuuliza Rafael malaika aliyekuwa pamoja nami:
“Hii roho inayowasilisha malalamiko, ni ya nani? Ni nani ambaye sauti yake inapaza kesi mbele ya mbingu?”

22 Akanijibu akasema:
“Hii ni roho iliyotoka kwa Habili, ambaye aliuawa na ndugu yake Kaini. Yeye anawasilisha kesi dhidi yake hadi uzao wake utakapofutwa kabisa juu ya uso wa dunia, na uzao wake uondolewe kati ya uzao wa wanadamu.”

23 Kisha nikauliza kuhusu hilo, na kuhusu mashimo yale yote:
“Kwa nini shimo moja limetengwa na lingine?”

24 Akanijibu akasema:
“Mashimo haya matatu yamefanywa ili roho za waliokufa zitenganishwe. Na mgawanyiko umewekwa kwa ajili ya roho za wenye haki, ambamo kuna chemchemi yenye maji angavu.

Na mgawanyiko umewekwa kwa ajili ya wenye dhambi wanapokufa na kuzikwa duniani, na hukumu haijatendeka juu yao wakati wa maisha yao.

25 Hapa roho zao zitawekwa kando katika mateso makubwa mpaka siku kuu ya hukumu na adhabu na mateso ya wale wanaolaani milele na malipo ya roho zao. Hapa watafungwa milele.

Na mgawanyiko umewekwa kwa ajili ya roho za wale wanaowasilisha malalamiko, wanaotoa ushuhuda kuhusu maangamizi yao, walipouawa katika siku za wenye dhambi.

26 Mgawanyiko pia umewekwa kwa ajili ya roho za watu ambao hawakuwa wenye haki bali ni wenye dhambi, waliokamilika katika makosa. Hao watakuwa marafiki wa wakosaji, lakini roho zao hazitauawa siku ya hukumu, wala hazitafufuliwa kutoka humo.”

Ufunuo wa Safari ya Roho Baada ya Kifo

Kulingana na Henoko, malaika Rafael alimwonyesha kwamba baada ya kifo, roho za wanadamu haziishi ovyo, bali zinakusanywa na kutenganishwa kulingana na matendo yao. Kuna mashimo manne makuu:

(a) Shimo la Wenye Haki

Roho za wenye haki hupumzika kwenye sehemu yenye chemchemi ya maji angavu.

Ni alama ya faraja, pumziko na tumaini la ufufuo wa uzima.

Yesu alisema: “Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.” (Yohana 17:3).

(b) Shimo la Wenye Dhambi Wasiohukumiwa Duniani

Hawa ni wale waliotenda maovu lakini hawakupata hukumu wakati wa maisha yao.

Roho zao zinawekwa kwenye mateso makubwa, zikitazamia hukumu ya mwisho.

Waebrania 9:27: “Na kama vile wanadamu wamewekwa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu.”

(c) Shimo la Waliouliwa kwa Dhuluma

Roho hizi zinatoa malalamiko na ushuhuda juu ya mateso yao.

Mfano ni Habili, ambaye damu yake ilililia haki mbele za Mungu (Mwanzo 4:10).
"Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi."

Hii inatufundisha kuwa Mungu husikia kilio cha wanyonge.

(d) Shimo la Wenye Dhambi Waliojaa Makosa

Hawa walikamilika katika uovu, waliishi maisha ya uasi wa kudumu.

Roho zao hazitafufuliwa tena, bali zitafungwa milele kwenye giza lisilo na tumaini.

Ufunuo 20:15: “Na mtu yeyote asiyepatikana ameandikwa katika kitabu cha uzima alitupwa katika ziwa la moto.”

Mafunzo Makuu kwa Maisha Yetu

1. Kifo si mwisho, bali ni mwanzo wa safari ya milele.

2. Mungu ni wa haki, kila dhuluma huangaliwa na hukumu yake huja.

3. Wenye haki na waovu hutenganishwa.

4. Yesu Kristo ndiye tumaini la uzima wa milele. Yohana 11:25: “Mimi ndimi huo ufufuo na uzima; yeye aniaminiye mimi ajapokufa ataishi.”

Kwa hiyo, mtu akifa haendi mahali pamoja kwa wote. Kuna mgawanyiko:

Wenye haki → pumziko na faraja.

Wenye dhambi → mateso na giza la milele.
Mungu aiweke roho ya marehemu panapostahili
 
Sio story ni kweli mkuu. Jaribuni kujifunza vitu msiishie kusoma elimu za Biology, Physics na Chemistry pekee. Hiyo elimu haitoshi kwa mwadamu kuwa na maarifa.
Hizo elimu za Biology, physics n.k zinaundwa kwa nadharia zinazothibitishika na hivyo kuwa na mantiki.
Hizo elimu nyingine ni za kiungaunga, uongo na vitisho..
Mfano; Tukiuliza ututhibitishie uwepo wa nafasi na roho, utaanza kujiumauma na kuleta ubishi.
 
Hizo elimu za Biology, physics n.k zinaundwa kwa nadharia zinazothibitishika na hivyo kuwa na mantiki.
Hizo elimu nyingine ni za kiungaunga, uongo na vitisho..
Mfano; Tukiuliza ututhibitishie uwepo wa nafasi na roho, utaanza kujiumauma na kuleta ubishi.
Mtu anauliza akifa ataenda wapi ? Wakati hata alipo toka hajui ? Na wala hakua anajitambua kwa chochote
 
Nakazia, jinsi mnyama akifa akazikwa ardhini na kuoza ndivyo ilivyo pia kwa binadam sema ni vile hizi imani zinatuaminisha vitu ambavyo atuna ushahidi navyo.
Na kabla ya kuzaliwa ulikuwepo wapi?

Na kwanini sisi na wanyama tonatofautiana ufahamu?

Na kwanini ufe kama vile ulivyozaliwa bila ya utashi wako? Unajikuta tu umezaliwa.

Na kwanini wengine wapitie mateso hapa duniani na angalia wengine wanaishi vizuri?

Kama vile ilivyokuwa huwezi kujibu maswali hayo basi aliyekuumba alishakwambia kuwa ukifa unakwenda wapi na utalipwa kwa Yale uliyotatenda.

Kila hatua utakayo idiriki katika maisha yako iwe njema au iwe mbaya wewe ndio utakaye i experience.

Jiandae usiishi kwa mazoea hukuumbwa Bure Bure ufanye yako vyovyote ujiskiavyo alafu useme hakuna malipo.
 
Bikra ni kwa watu wema washenzi washenzi watakula kuni za moto
😡 hakuna moto/jehanam, hizo verse zimetengenezwa ili kuleta utulivu duniani, na kudhibiti tabia za watu, Mungu hana vitisho na kama alituumba hawezi tutupa motoni tuungue for endless time, akiwa anatuona na kufurahia maumivu tunayopata
I believe if there is any kind of god, he cannot be a sadist, If he really is all-powerful and all-knowing, why does he let his own creation go through so much shit?

View: https://youtu.be/TpawdjeH-8w?t=31
 
Hizo zote ni story za kutungwa mtu akifa haendi popote zaidi ya kuoza na kirutubisha ardhi na kufanya maisha yaendelee duniani
Hata ulivyokuwa kiunoni mwa wazazi wako ulikuwa hujui kama utakaa kwenye uterus, ukakaa na hapo pia ulikuwa hujui kama utakuja duniani na ukaja

Sasa unapata wapi jeuri ya kuwa na confidence ya kujibu hivyo?
 
Mambo ya ngumu kumeza haya
Ila bora kifo kimeumbiwa kwa
Mwanadam,maana hakuna kiumbe jeuri,mjuaji,roho mbaya kama mwanadam

Ova
 
Hata ulivyokuwa kiunoni mwa wazazi wako ulikuwa hujui kama utakaa kwenye uterus, ukakaa na hapo pia ulikuwa hujui kama utakuja duniani na ukaja

Sasa unapata wapi jeuri ya kuwa na confidence ya kujibu hivyo?
Wewe ukifa utakua na confidence au jeuri ya kujua unaenda wapi?
 
Hapana mkuu mtu anapokufa mwili na roho ya nafsi vinatengana. Mwili unabaki duniani. Roho ya nafsi inachukuliwa na malaika mtoa roho inapelekwa ulimwengu mwingine.
Kwanza thibitisha uwepo wa hiyo roho.

Sio kuleta hadithi za kwenye hekaya za Biblia
 
Back
Top Bottom