Mtu akifa anaenda wapi?

Mtu akifa anaenda wapi?

Hakuna ajuaye mtu akifa huwa anaenda wapi, ni fumbo lililokosa majibu
Sasa mkuu wangu kwa kufikiria TU kidogo ukifa mifumo yako yote ya mwili imekufa kuanzia ubongo,jicho mpaka moyo Ina maanisha hauna unachokijua wewe ni zero labda kwenye decomposition viumbe wengine waibuke kula hivo virutubisho vyako
Sasa jibu liko wazi BIASHARA ITAKUA IMEISHA
 
Ukweli mtupu huu mkuu.
Binadamu Akifa ni sawa na amekufa mbuzi tu, sema sisi kifo tumekiongezea sifuri tumekipatia uzito🤣
Ila ukweli mchungu ukifa unaenda kuoza na kurutubisha ardhi
Ndio uhalisia ni vile tu tunaheshimu ubinadam ndio maana mambo yanakuwa mengi.
 
Kulala ni kupoteza fahamu kwa Muda kwasababu unapolala, huwezi kufahamu kinachoendelea duniani. Ukipitiwa na usingizi mzito, huwezi kujua mtu akiingia chumbani, hata sauti nyingine zinaweza usizisikie. Hali hii inafanana na kifo kwa sababu mtu aliyekufa pia hana tena fahamu ya kinachoendelea duniani. Hivyo basi, kwa macho ya kawaida, mtu aliyelala anaonekana kana kwamba amekufa, tofauti ikiwa ni kwamba bado atamka.

Kila Usingizi ni "Mazoezi" ya Kifo
Wanafalsafa na wahenga wengi huona usingizi kama kumbusho la udhaifu wa mwanadamu. Unapolala, ni kama unakabidhi maisha yako mikononi mwa Mungu; huwezi kujilinda wala kujitambua. Kila kuamka ni kama kupewa nafasi mpya ya kuendelea kuishi. Ndiyo maana wengine huomba kabla ya kulala na wanaposhukuru wanapoamka wakihisi wamepewa “maisha mapya.”

Lakini wakati mwili umechoka hauwezi kufanya kazi mara unaota unatembea na kufanya mambo mbalimbali. Ndoto ni kama kivuli cha ulimwengu mwingine. Ndoto hutazamwa kama safari ya nafsi katika ulimwengu wa roho au wa ndani. Kwa hiyo, baadhi ya falsafa husema usingizi ni kama “kutembelea” ulimwengu wa kifo bila kuondoka kabisa duniani. Ndiyo maana mtu akipata ndoto nzito, anaweza kusema “ilikuwa kama kweli, nilihisi nipo sehemu nyingine.”

Daah! Ila wewe Mdau. Nimekubali kwamba upo vizuri. Ahsante kwa shule nzuri. 🙏🏽
 
Acha vitisho mkuu visivyo na msingi! Tenda wema nenda zako, malipo Yako hapa hapa Duniani. Kama haujapata malipo hapa Duniani basi usitarajie kwamba Kuna malipo huko kwenye mawingu.
Unawachukuliaje wale watu waliotesa watu hapa duniani na Wala hawakupata malipo yao hapa je mambo yao yamepita Bure Bure?
 
BINADAMU ana vitu vitatu vikuu 3
1)MWILI HUU WA NYAMA
asili yake ni mavumbi ya udongo,kuharibika,mauti ,akifa mwili huu huharibika.

2)Nafsi ..utashi..akili..memory kumbukumbu data..hizi hazifutiki,maarifa,ufahamu

3)ROHO..hii ni pumzi ya Mungu ya uhai aliyotupulizia wanadamu wote,na hii Roho pumzi ya uhai..haifi,isipokuwa Mungu pekee anaweza kuua Roho na mwili,mara nyingi Roho haifi...milele.

BAADA YA MTU KUFA/KUFARIKI
ROHO huacha mwili dakika hiyohiyo na kuvaa mwili mpya ambao hauharibiki na KUSHUKA KUZIMU

KUZIMU ni njiapanda ya kwenda either NJIA YA KUZIMU YA MATESO au kwenda njia ya MBINGUNI
Kuna tofauti kati ya Kuzimu ya mateso na JEHANAMU .
Utakatifu wako ukiwa duniani/matendo yako ukiwa hai duniani ndio yatakayo amua roho yako itakapokwenda baada ya kufa.
UTAVUNA ULICHOPANDA.

YESU alieleze hatima baada ya kufa kwa kutumia mfano wa TAJIRI NA MASIKINI LAZARO..baada ya hawa watu wawilli kufa TAJIRI ALIKWENDA KUZIMU YA MOTO kutokana na matendo yake mabaya ya uchoyo n.k akiwa duniani,na masikini Lazaro alikwenda mbinguni.

TAJIRI NA LAZARO
Luka 16:19-31 “Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu. Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.”
YESU NI KWELI MFANO HUU SIO MFANO WA KUFIKIRIKA KINADHARIA TU BALI NI HALI HALISI.

KUZIMU NI HALISI UNAWEZA KWENDA NA UKARUDI ,HATA SASA WAPO WATU WANAENDA KUZIMU NA KURUDI ,HASA WASHIRIKINA ,WACHAWI WAGANGA WA KIENYEJI,WATU MAARUFU,IKIWEMO FREEMANSORY,MITUME NA MANABII WA UONGO,WASANII,WANASIASA N.K

NB Kuzimu umegawanyika vipengele zaidi ya vitatu ,ile sehemu ya mateso wanaenda kuzimu wengi hawafiki hapo ,wanafikia mapokezi na kusaini mikataba na kupewa mahitaji nguvu,mafanikio mvuto n.k

illa kuna enzi za kuzimu au maeneo zaidi ya moja.


View: https://youtu.be/35jly4iZ5ns?si=baGYbXbXkpiJgF08


View: https://www.youtube.com/live/_tI94qsZM_g?si=ZzBrgJTSj1C9BJ15


View: https://youtube.com/playlist?list=PLXTmPgeqbJ0kKsxAotPQkrszE6Qt_Y0qk&si=F-wiPlDs89ptqmyv
 
Unawachukuliaje wale watu waliotesa watu hapa duniani na Wala hawakupata malipo yao hapa je mambo yao yamepita Bure Bure?
Imeisha hiyo mkuu, kama hawajapata malipo hapa Duniani hasi habari Yao imeisha
 
Swali lako linatakiwa lijibiwe na mtu aliyekufa kiukweli kweli kwa kukatwa shingo na kiwiliwili kisha akafufuka.Kama hakuna mtu aliyewai kufa kifo cha namna biyo na akarudi basi jua ukifa hakuna unakoenda na ndoo imeisha hivyo.Mengine ni imani tu ambazo hakuna nwenye uhakika zaidi ya kuaminishana nando maana ata anayekuaminisha naye anaogopa kufa.
 
Na kabla ya kuzaliwa ulikuwepo wapi?

Na kwanini sisi na wanyama tonatofautiana ufahamu?

Na kwanini ufe kama vile ulivyozaliwa bila ya utashi wako? Unajikuta tu umezaliwa.

Na kwanini wengine wapitie mateso hapa duniani na angalia wengine wanaishi vizuri?

Kama vile ilivyokuwa huwezi kujibu maswali hayo basi aliyekuumba alishakwambia kuwa ukifa unakwenda wapi na utalipwa kwa Yale uliyotatenda.

Kila hatua utakayo idiriki katika maisha yako iwe njema au iwe mbaya wewe ndio utakaye i experience.

Jiandae usiishi kwa mazoea hukuumbwa Bure Bure ufanye yako vyovyote ujiskiavyo alafu useme hakuna malipo.
Binadamu amewazidi viumbe wengine ufahamu gani?.Au unazungumzia kusoma shule nakutengeneza magari.Huo sio ufahamu ni madhaifu yetu yakimaumbike ndiyo umetufanya tujifikishe uko..Kitu pekee ambacho binadamu ni tofauti na viumbe wengine ni kutemea wima(upright).Mengine yote tuko sawa.kwasababu mambo ya msingi ni kuzaana,kuishi na kufa ambayo tuko sawa viumbe hai vyote duniani.
 
Ukweli gani? Kuna mahali popote sayansi inajihusisha na vitu vya imani visivyo na empirical evidence?
Naongelea sayansi kujaribu kusema ukweli ushaleta Imani Kati.

Narudia Tena, haijawahi kusema itabakia kujaribu kusema ukweli.
 
Story za vitabu vya apokrifa vya wayahudi na wakristo waasi

Unajua kwanini biblia ya canon hawakuviweka ?
 
1. Sehemu ya Wenye Haki

Roho za wenye haki hupumzika kwenye sehemu yenye chemchemi ya maji angavu.

Ni alama ya faraja, pumziko na tumaini la ufufuo wa uzima.


2. Sehemu ya Wenye Dhambi Wasiohukumiwa Duniani

Hawa ni wale waliotenda maovu lakini hawakupata hukumu wakati wa maisha yao.

Roho zao zinawekwa kwenye mateso makubwa, zikitazamia hukumu ya mwisho.


3. Sehemu ya Waliouliwa kwa Dhuluma

Roho hizi zinawekwa sehemu ya kutoa malalamiko na ushuhuda juu ya mateso yao.


4. Sehemu ya Wenye Dhambi Waliojaa Makosa

Hawa walikamilika katika uovu, waliishi maisha ya uasi wa kudumu.

Roho zao hazitafufuliwa tena, bali zitafungwa milele kwenye giza lisilo na tumaini.

Tunaokolewa kwa imani na sio kwa kufuata sheria.

Tunapewa bure tunatoa bure
 
Back
Top Bottom