Renegade Asante kwa ufafanuzi mzuri. Wakati mwingine hizi mada za JF tunazijibu kwa utani kumbe mwenzetu ana tatizo kweli. Kwa kuongezea kwenye ufafanuzi huo, wakati mwingine tabia mbaya ya mtoto ni matokeo ya yale maneno yaliyotamkwa na baba au mama wakati wa mimba huska. Ilimtokea rafiki yangu, yeye na mke wake walikuwa wameamua watazaa watoto watatu tu, na waliamua kufuata kalenda. wakiwa ndani ya mkakati wao wa kufuata kalenda mwanamke kapata mimba. yule jamaa alimfokea sana mke wake kwa nini karuhusu ile hali. Mimba miezi tisa wiki 40, mtoto hatoki. Wiki 42, mama kafanyiwa maombi ndo mtoto kazaliwa.
Mtoto kakua lakn kila akishikwa na baba lazima aliye sana. Hadi miaka miwili hali hiyo hiyo. Miaka minne, baba hawezi hata mkumtuma kitu. Fimbo haikusaidia. Baba akaanza kuhisi mtoto si wake.
Kama bahati akahudhuria semina ya maisha ya kiroho, bahati nzuri akafundishwa somo la toba. Ile semina ikampa mwanga. Baada ya semina jamaa alienda moja kwa moja hadi nyumbani. Kafika kamnyanyua mtoto na kumbeba kifuani kwake. Mtoto anakawa anajitahidi kujinasua mikononi mwake ila jamaa kamung'ang'ania, huku akitamka maneno ya kuomba msamaha kama alivyoelekezwa kwenye semina. Ilikuwa jioni, wakalala ikawa asubuhi. Mtoto alikuwa wa kwanza kumuamsha na kumsalimia: 'Baba shikamoo'. Hicho ni kitu alikuwa hajawahi kupata kutoka kwa huyo mtoto. Tokea hapo, mtoto akabadilika baba yake ndo akawa kipenzi chake kuliko hata mama. Kwa hiyo basi huenda tatizo likawa kwenye meneno yaliyotamkwa juu ya ile mimba. Wazazi waulizwe vizuri circumstances za hiyo mimba.