Mtoto wa wiki mbili aliyechomwa kisu afariki dunia

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
kichanga-pic.jpg

Mtoto mchanga wa wiki mbili aliyechomwa kisu na kisha utumbo kutoka nje na mama yake kuuawa akiwa amelala, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC).

Februari 22, mwaka huu Mwanamke huyo ajulikanaye kwa jina la Fausta Tesha (26) mkazi wa Mero, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro alichomwa kisu sehemu za mwili wake na kisha kufariki dunia huku mwanaye huyo akijeruhiwa tumboni hali ambayo iliyosababisha utumbo kutoka nje.

Akizungumza na Mwananchi digital leo Februari 25, 2023, Mama mzazi wa binti huyo, Ezra Tesha amesema mjukuu wake amefariki dunia leo wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya KCMC.

"Kwa kweli tuna huzunika sana, maana na hata mjukuu wetu aliyejeruhiwa na huyu mhalifu tumepewa taarifa naye amefariki, tunamwachia Mungu zaidi hatuna la kufanya," amesema bibi huyo.

Amesema kwa sasa wanaendelea na taratibu za mazishi ambapo mama na mwanaye huyo watazikwa kwa pamoja siku ya Jumanne, Februari 28 katika kijiji cha Mero, kata ya Kirua Vunjo Mashariki.

Mpaka sasa mwanaume aliyetekeleza mauaji hayo anatafutwa na Polisi, Mkoani Kilimanjaro ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma hizo za mauaji.

Awali Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alisema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi baina ya wanandoa hao.

Pia soma: Kilimanjaro: Mume adaiwa kumuua mkewe na kumjeruhi mtoto mchanga

MWANANCHI
 
Mnhh mnh mnhh..😭
Dunia hii!
 
Hapana, hapo umemkufuru muumba!

Ungelisema ni heri kubakia single kwa kisa kama hiki.

Maana dharau zingine waweza kuletewa na mwanamke, ukamwadhibu kwa libolo na heshima ikarudi.

Je kama haujiwezi, umpige kwa makofi ukafungwe udhalilike?

Nyege zikimrudia kiburi kipo pale pale
 
Back
Top Bottom