Mtoto wa Waziri Simbachawene kuburuzwa mahakamani

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Siku moja baada ya kusambaa video inayomuonyesha mtoto wa Waziri wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene akitoa lugha chafu mbele ya askari wa usalama barabarani, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema sheria itafuata mkondo wake.

Juzi ilisambaa video hiyo ikionyesha watu wanaolalamikia magari yao kugongwa na kijana huyo aitwaye James Simbachawene aliyekuwa akijitapa hawezi kufanywa chochote kwa kuwa ni mtoto wa waziri.

Kulingana na watu hao, kijana huyo alidaiwa kuzidiwa na ulevi na ndio maana aligonga gari zaidi ya moja na kuendelea na safari yake bila kujali.

Kipande kingine kilimuonyesha James akiwa kituo cha polisi na akibishana na askari waliokuwa kituoni hapo na kuwatolea lugha chafu huku naye akilalamikia kutaka kupigwa.

Kamanda Muliro alilieleza Mwananchi kuwa hakuna uhusiano wa kosa alilofanya kijana huyo na kuwa mtoto wa waziri, hivyo atawajibishwa kulingana na sheria.

“Katiba yetu ipo wazi. Ipo ibara inayosisitiza usawa mbele ya sheria.” Watu wote wapo sawa mbele ya sheria. Atashughulikiwa kama yeye. Kwenye kosa alilolitenda, kalitenda yeye. Hakuna uhusiano wa makosa aliyoyatenda na kumhusisha baba yake. Atawajibika kisheria kama yeye,” alisema Muliro ambaye kwa sasa yupo likizo.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi kanda maalumu, William Mkonda alisema upelelezi unaendelea na muda wowote atafikishwa mahakamani.

“Ni tukio la uvunjaji wa sheria za usalama barabarani lilitokea maeneo ya Oysterbay na alifikishwa kituo cha polisi Oysterbay. Tunakusanya ushahidi wote tukikamilisha atafikishwa mahakamani kesho au Jumatano,” alisema Mkonda.

Juzi jioni muda mfupi baada ya kusambaa kwa video hiyo, Waziri Simbachawene alitoa taarifa kukemea tukio hilo kwa kuandika, “Nimeiona clip inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii , nakiri kuwa huyo ni kijana wangu ambaye ni mtu mzima anajitegemea na anafamilia yake.

“Nimemwagiza mkuu wa kituo kwa sababu amekosa adabu kwa Jeshi la Polisi na ametenda kosa la usalama barabarani ashughulikiwe bila huruma kwa mujibu wa sheria. Binafsi naomba radhi sana kwa walioathirika na mkasa huo, lakini pia kwa jeshi la polisi na Watanzania wote. Poleni kwa usumbufu wowote mlioupata.”

Tukio hilo linaloendana na lililotokea mwaka 2016 ambapo askari wa usalama barabarani, Deogratius Mbango alijikuta katika vute nikuvute na mke wa aliyekuwa waziri Agustino Mahiga baada ya kumuandikia faini dereva wake kwa kosa la kutosimama kwenye kivuko cha watembea kwa miguu.

Taarifa zilieleza mwanamke huyo alimshambulia kwa maneno Mbango akieleza yeye ni mke wa waziri na hakubaliani na adhabu hiyo iliyotolewa kwa dereva wake.

Baada ya taarifa hiyo kusambaa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli alimpongeza askari huyo na kuelekeza apandishwe cheo kwa uthubutu aliofanya kusimamia misingi ya kazi yake.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha kazi cha makamanda wa polisi wa mikoa, mawakili wafawidhi wa Serikali, na wakuu wa upelelezi wa mikoa na vikosi, kilichofanyika mjini Dodoma, hayati Rais Magufuli alisema, “Ebo! Yule trafiki anajua kazi, mpandishe cheo. Na huyo waziri na mke wake nimeshamwambia.”
 
Ulitaka asemeje??? Ulitaka awaambie waandishi wa habari kwamba hakuna matata huyu ataendelea kula bata mtaani?

Angalia kuna clip inasambaa mtandaoni polisi hao hao wanampa kichapo mwananchi licha ya mtuhumiwa kuomba asiadhibiwe yeye ni mgonjwa wa pumu ma bwa yale yanaendelea kumpa kipigo Mtanzania mwenzetu wakati polisi wale wale walinywea kwa huyo mliye danganywa atapelekwa lupango.

Inaumiza na kukasirisha sana kuona jinsi gani jeshi letu la polisi linavunja sheria. Unampiga mtu miguuni kwa rungu huku umemfunga pingu dah enewei sawa. Tuwatakie kazi njema ya kumpeleka mahakamani mtoto wa walamba asali.
 
Nimeiona Hiyo clip ya mtu anaye pigwa na polisi! Jamani hatujui kosa alilofanya yule jamaa kwa hiyo tuache ushabiki wa kijinga!
Yule jamaa kama ni jambazi au muuaji je?
Foolish
 
Nimeiona Hiyo clip ya mtu anaye pigwa na polisi! Jamani hatujui kosa alilofanya yule jamaa kwa hiyo tuache ushabiki wa kijinga!
Yule jamaa kama ni jambazi au muuaji je?
Foolish
Bila kujari kosa analotuhumiwa nalo mkosaji,hairuhusiwi kumpiga,maana kumpiga tayari ni kumhukumu.

Uandishi na ushabiki wa namna hii uliofanya, ndiyo unaofanya wakenya wale wanatutukana matusi ya hovyo
 
Nimeiona Hiyo clip ya mtu anaye pigwa na polisi! Jamani hatujui kosa alilofanya yule jamaa kwa hiyo tuache ushabiki wa kijinga!
Yule jamaa kama ni jambazi au muuaji je?
Foolish
Wewe ndo foolish ever seen!!

Unafahamu PGO na sheria za nchi zinasemaje? Waulize wametumia sheria gani kumuadhibu mtuhumiwa????

Hata kama angekuwa amemuua baba yako sheria za nchi haziruhusu polisi au mtu yoyote kumuadhibu mhalifu. Take time uache uzwazwa na upopoma!!

Kama unasubri teuzi sisi wenyewe tushasubiri saaaa hadi tumechoka.. Endelea kusubiri kulamba asali.
 
tabia kama hizi zilipotea sasa naona majuha wameanza kuchipuka.

Nashauri adhabu kali ichukiliwe dhidi yake kwa kutumia cheo cha baba yake vibaya ili iwe fundisho kwa majuha/malimbukine wengine kuwa hakuna aliye juu ya sheria, sheria ni msumeno hivyo tunataka kuona unamkata huyu mtoto wa waziri kama unavyo kata watoto wa wanyonge.

kwa nchi za wenzetu wanao fahamu maana ya uwajibikaji, ilipaswa Baba awajibike ajiuzulu kwa matendo aliyo yafanya mtoto wake ili kulinda heshima yake, kwasababu ametumia/ameringia cheo cha Baba yake kuvunja sheria.
 
Back
Top Bottom