Waziri Simbachawene aitaka TAKUKURU kuwadhibiti wachezeaji rasilimali za nchi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU kudhibiti mianya ya rushwa katika fedha za miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na serikali nchini ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana.

Ametoa kauli hiyo leo alipotembelea na kukagua ujenzi wa jengo la ofisi za TAKUKURU mkoani Iringa ambapo amemtaka Mkandarasi kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ifikapo mwezi Juni mwaka huu kama ilivyopangwa ili watumishi wa taasisi hiyo waweze kufanya kazi zao katika mazingira mazuri.

“Tukawe watu wa kupekenyua pekenyua kwenye miradi hii inayotekelezwa na serikali kwani kuna watu wanatumia vibaya fedha za serikali, penyeni huko kuwadhibiti ili miradi ya maendeleo ikamilike kwa wakati na kwa viwango kama ilivyokusudiwa,” amesisitiza Mhe. Simbachwene

Amefafanua kuwa TAKUKURU inatakiwa kuhakikisha inasimamia na kudhibiti fedha zisipotee lakini bila kuathiri maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa nchini.

"Palipo na shilingi ya Mama Samia waambieni TAKUKURU tupo ila katika kufanya haya tusikwamishe maendeleo" amesisitiza Mhe. Simbachawene.

Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Simbachawene ameitaka Taasisi hiyo kuwachukulia hatua wale wote wanaokwamisha shughuli za maendeleo na hivyo kukwamisha utendaji wa Rais Mhe. Dkt. Samia suluhu Hassan.

"Dhibitini mianya ya kuchezea rasilimali za nchi ikiwemo fedha zinazotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, sehemu ambako fedha imesimamiwa vizuri matokeo mazuri yameonekana, naomba niwasihi kuendelea kuwadhibiti ipasavyo wachezea fedha za maendeleo" amesema Mhe. Simbachawene.

Ameongeza kuwa anataka kuona TAKUKURU ikichukua hatua kwa wale wote wanaokwamisha nia nzuri ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kama hatua hizo hazichukuliwi basi miradi mizuri iliyotekelezwa ionekane ili wananchi wazidi kuwa na imani na serikali yao.

50849abf5d8ca9e7a5dcc6945d955e02.jpeg
WhatsApp Image 2024-02-22 at 12.22.47.jpeg
WhatsApp Image 2024-02-22 at 12.22.46.jpeg
WhatsApp Image 2024-02-22 at 12.22.46(1).jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-02-22 at 12.22.45.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-22 at 12.22.45.jpeg
    70.1 KB · Views: 2
Kiukweli hao jamaa sijaona Impact yao kabisa. Sijui namna wanvyofanya kazi nisilaumu sana.

Kuna hao na Zimamoto.
 
Hiyo nguvu wanayo au wabaki ti kuwavizia watendaji kata,waalimu wakuu na mahakimu wa mahakama za kata.
 
Takukuru wangefumuliwa tu wana kesi za ajabu ajabu sana huku wakiacha Mali za Nchi zikitafunwa na wahuni wachache...
 
Back
Top Bottom