Mimi naungana na Shishi kukwambia kwamba ni bora usiseme chochote maana mumewe wako atachanganyikiwa sana na kujiuliza maswali mengi ambayo wewe huwezi kuyajibu. Atakuuliza maswali kama yafuatayo: Umetembea na huyo jamaa kwa miaka mingapi wakati wa ndoa yenu? Kama mna watoto wengine anaweza kuuliza je na hawa watoto kuna uwezekano kuwa si wangu? Ni wakati gani ambapo mlikuwa mnakutana na mlikutana mara ngapi labda kwa wiki au kwa mwezi? Kama mumeo huwa anasafiri kikazi au kibiashara atakuuliza uliwahi kumleta nyumbani kwenu na mkafanya naye mapenzi labda kitandani kwenu? Na mengine mengi tu.
Kwa kifupi ukimwambia ndio itakuwa mwisho wa ndoa yenu. Najua hiki kitu kinakutesa sana na kukukosesha raha katika maisha yako ya kila siku, lakini siafikiani na wewe kumwambia mumeo. Unajua kwa sababu halinihusu mimi ni rahisi mno kusema mwambie atakusamehe, lakini ukweli mkuki kwa nguruwe kwa mwanadamu ni mchungu. Wanaume tulivyo katika maswala haya hasa kunapokuwa na mtoto aliyemlea miaka yote hiyo akijua kwamba ni mwanae halafu anakuja kuambiwa si mwanae basi inakuwa ni kasheshe ya hali ya juu. Ndio wako wanaume wachache wanaweza kusamehe lakini zaidi ya asilimia 80 ya wanaume hawawezi kusamehe na ndoa inakuwa imeingia dosari kubwa na itadorora na hatimaye huvunjika. Kila la heri lakini kumwambia mumeo IS A NO NO maana ndio itakuwa mwisho wa ndoa yenu. Na huyo taahira fanya juu chini ukate mawasiliano naye kabisa kama mnafanya kazi pamoja basi aanza kutafuta kazi nyingine kwa juhudi zako zote.
Kidzogolae,
Yaelekea wewe umeshatoa adhabu kabisa maana unavyoonekana ni ungempa talaka mkeo tu akaanze maisha mapya, hayo unayoyasema.
wanaume mnajifanya mna mahasira sana, na ndio maana hamuambiwi jambo. Busara zenu tuzione katika vitendo na maneno yenu na sio MANGUMI na KUCHINJANA. Mbona sisi wanawake tunawafumania na bado tunawaandalia chakula na kuwatunzia siri? Hapa sitafuti sympathy, nataka tu kuonyesha kuwa mko tofauti.
Sijui kama umesoma alivyosema Abunuwasi - yeye ana wake baba mkubwa sasa na anamtunza. Labda "kifua" chako kidogo tu.
Nataka kujaribu kumpa mume wangu mtihani kumpima pressure kabla sijampa ishu, any idea how?.
"You have no right to call me father and I got no right to call you son" aliwahi kuimba Lucky Dube akielezea tukio kama la Da'Maindainda!
Japo nimechelewa pls let me share a live example related to this one:
Nina rafiki yangu wa karibu mno ambaye alililewa katika mazingara kama haya, yeye ni mzaliwa wa kwanza kwa wazazi wake, akifuatiwa na wadogo zake watatu wawili wa kike na mmoja wa kiume kwenye familia yao ya watoto wanne! Kimaisha wazazi wake hawa hawakuwa na maisha mazuri sana na huyu rafiki yangu alijitahidi mno kujaribu kuweka mambo sawa ikiwa ni pamoja kuwahudumia wadogo zake pamoja na wazazi wake.
Huyu rafiki yangu pia alijitahidi kufungua biashara ndogo ndogo kijijini kwao pamoja na kununua mashamba na BABA zake wadogo walikuwa ndio wasimamizi. Maisha yalisonga mbele kwa staili hii hadi mwaka 2005 alipougua baba yake mzazi, Rafiki yangu alifanya juhudi zote za kumpatia matibabu baba yake kwa muda mrefu bila mafaniakio na bahati mbaya baba yake alifariki mwaka huo huo. Alifanya taratibu zote za mazishi na baada ya kumaliza mambo yaliendelea kama kawaida!
KASHESHE! iliibuka mwaka 2007, ikiwa ni miaka miwili baada ya kumzika baba yake! Aliibuka baba mwingine na kudai kuwa ni mwanae! (HUYU rafiki yangu keshaoa tangu mwaka 1998 na ana watoto wawili!) Huyu baba kila kitu anafanana naye! Hiii ilimuweka huyu rafiki yangu katika hali ya kuchanganyikiwa na kutoamini na hadi leo hii hataki hata kumuona huyo baba yake mzazi (japokuwa ni mtu anayejiweza kiuchumi na rafiki yangu mambo yake sio mazuri) huyu baba kamuahidi mambo kibao lakini jamaa kagoma kabisa
KIBAYA ZAIDI baada ya huyu baba kujitokeza jamaa ilibidi amvae mama yake ambaye yuko kijijini na kumuuliza, mama alishindwa kumjibu akamuelekeza kwa wajomba zake ambao walimwambia kuwa ni kweli na hata BABA aliyemzika alikuwa anafahamu kuwa hakuwa mwanae! Baba zake wadogo nao pia walikuwa wanalifahamu hilo na walipoona kuwa ameshafahamu wakaanza kumuwekea mipaka, biashara na mashamba wamechukia na imekuwa kama wamemtenga! Jamaa amekuwa mpweke sasa kwani ndugu wa upande wa baba aliyemlea hawamtaki na wa upande wa bilogical father hawafahamu na wala hataki kuwasikia!
Honestly hii hali imemuathiri sana kisaikolojia na hata kiutendaji ameshuka sana pamoja na ushauri anaoupata mara kwa mara!
Tofauti kwa huyu rafiki yangu ni kuwa watu wengi katika familia walikuwa wanalifahamu hili baada ya mama kuamua kumueleza ukweli baba'ke kuwa wakati anaolewa alikuwa na mimba ya mtu mwingine, na huyu bwana (mwenye mimba) hakuwahi hata mara moja kujitokeza kwa mtoto.
Da'Mainda hili jambo ni gumu na lahitaji busara za ziada, ila kama ulivyoamua mueleze mumeo na pia mtoto kuepusha mabalaa ya uzeeni!
Pole dada, Mimi binafsi nina jambo linalofanana na lako,miaka sita iliyopita nilikuwa na uhusiano na dada mmoja ambaye kwa wakati ule alikuwa na mchumba wake, ambaye walikuwa wakiishi sehemu tofauti tofauti,kazi ya huyu dada ilikuwa inamfanya awe asafiri mara kwa mara na hivyo kuwa anakutana na mwenza wake .Lakini katika mahusiano yetu huyu dada alipata uja uzito,kilichotokea ni kwamba alikuwa ajasafiri katika kipindi cha miezi mitatu hivi, hiyo ilifanya ajue wazi muhusika ni nani, na wakati huo maandalizi ya Ndoa yao yalikuwa yamekamilika.Baada ya miezi minne wakafunga ndoa wakati yule dada akiwa mja mzito,tulipojadiliano juu ya huo huja uzito alikubali kutotoa ,lolote na liwe.Kweli akajifungua mtoto wa kiume copyright na baba mimi,na akawa anataka niendelee kuwa baba wa mtoto wakati yeye ni mke wa mtu?Nilikataa katakata.
Na jambo baya zaidi nilipoamia kwenye makazi yangu mapya nikagundua kuwa tunaishi wote mtaa mmoja kwa tofauti ya nyumba kama 10 hivi.
Nime-avoid sana mawasiliano naye.Japo yeye analazimisha.Sipendi mke wangu ajue wala mume wake.
Hivyo kumueleza au kutomueleza mume wako kunategemeana na jinsi yeye alivyo kitabia, kama high tempered utalimwa talaka ya haraka.Kumueleza kunategemeana na tabia ya mtu.kumueleza kutamfanya akose imani kwako.
Kwanza pole sana Mainda,
Katika vitu ambavyo sitokushauri kama unaipenda ndoa yako basi UMWAMBIE huyu baba...
KASHESHE! iliibuka mwaka 2007, ikiwa ni miaka miwili baada ya kumzika baba yake! Aliibuka baba mwingine na kudai kuwa ni mwanae! (HUYU rafiki yangu keshaoa tangu mwaka 1998 na ana watoto wawili!) Huyu baba kila kitu anafanana naye! Hiii ilimuweka huyu rafiki yangu katika hali ya kuchanganyikiwa na kutoamini na hadi leo hii hataki hata kumuona huyo baba yake mzazi (japokuwa ni mtu anayejiweza kiuchumi na rafiki yangu mambo yake sio mazuri) huyu baba kamuahidi mambo kibao lakini jamaa kagoma kabisa
KIBAYA ZAIDI baada ya huyu baba kujitokeza jamaa ilibidi amvae mama yake ambaye yuko kijijini na kumuuliza, mama alishindwa kumjibu akamuelekeza kwa wajomba zake ambao walimwambia kuwa ni kweli na hata BABA aliyemzika alikuwa anafahamu kuwa hakuwa mwanae! Baba zake wadogo nao pia walikuwa wanalifahamu hilo na walipoona kuwa ameshafahamu wakaanza kumuwekea mipaka, biashara na mashamba wamechukia na imekuwa kama wamemtenga! Jamaa amekuwa mpweke sasa kwani ndugu wa upande wa baba aliyemlea hawamtaki na wa upande wa bilogical father hawafahamu na wala hataki kuwasikia!
Mnh, Renegade, pole bro. Naomba kukuuliza maswali matatu...
...1; kwanini unakataa kuwa baba wa huyo mtoto?
...2: Kwanini hupendi mumewe ajue, wala mkeo ajue huyo mtoto ni wako?
...3; unaonaje ukipata vipimo vya kitaalamu zaidi, i.e DNA test kuhakikisha ukweli wa paternity?
Eeka Mangi na wote mnaokataa 'asimwambie',... hapo nyuma umesoma mkasa aliotuletea ndugu yetu KILAMBI? niwakumbushe;
...sumu hii haifichiki, utaficha leo, lakini ipo siku tu itakuja toka hadharani! Mw'Mungu atakuumbua tu, hata kama sio kwenye mambo ya mirathi, huenda hata pale wanandugu watapokuomba umchangie damu, au magonjwa ya kurithi, nk... Siku hizi safari za Uingereza zinahusisha sana DNA testing iwapo watoto wanahusishwa...
Kuna mengi tu yakuumbua...! siri hiyo isipomdhuru mume, itakuja wadhuru watoto huko maishani mwao iwapo litatokea jambo ambalo litawataka wathibitishe undugu wao...
Naomba kukujibu kama ifuatavyo,
1.Sikatai kuwa baba wa mtoto, lakini hakuna mtoto anayeweza kuwa na baba wawili,pia kukubali kwangu akuwezi kumsaidia huyo dada na hasa ukizingatia kuwa tulipokuwa na uhusiano kila mmoja alikuwa na mtu wake.Na isitoshe itahadhiri ndoa yake.
2.Kwa upande wa mke wangu ,nitaazaje kumueleza?Mume wake akijua nini itakuwa hatima ya ndo yao, lengo hasa ni nini?
3.Kuhusu DNA sawa unaweza kufanya hivyo kama una mashaka hivi,kwa upande wangu sina mashaka, maana sura ya mtoto ni yangu na pia anafanana sana na watoto wangu.
Mama pole sana kwani napenda kukutia moyo uwe tu mkweli kwa mumeo. Mimi haya yalikuta miaka 18 iliyopita baada ya mamsapu wangu kufanya tendo kama lako na akazaa mtoto ambaye kwa kweli ni kijana mzuri sana na mwenye akili sana> Nimemsomesha na hata sasa yuko USA kwenye chuo kikuu huko. Hili pendo lilitokea baada ya mke wangu kunieleza ukweli na kunisihi sana nimfichie hii siri kama mwenzanke kwenye ndoa inayotambulika tulifanya hivyo and now the boy is 21 yrs old. Baadaye nilizunguza na Bilogical father wake kuhusu hili jambo na kuwa kijana anatumia sir yangu. Huyu bwana naye kanishukuru sana na kuniomba hata mtoto asiambiwe yaliyopita yasije yakamfanya akaumia roho. Hivyo kama mumeo ni mtu aliyekomaa kindoa naona hili halitakuwa jambo la ajaabu kwake na bila shaka atalipokea kwa moyo wa kutaka kukusaidia pia maana ni kitu ambacho uanakijutia hadi leo.