Kidzogolae,
Yaelekea wewe umeshatoa adhabu kabisa maana unavyoonekana ni ungempa talaka mkeo tu akaanze maisha mapya, hayo unayoyasema.
wanaume mnajifanya mna mahasira sana, na ndio maana hamuambiwi jambo. Busara zenu tuzione katika vitendo na maneno yenu na sio MANGUMI na KUCHINJANA. Mbona sisi wanawake tunawafumania na bado tunawaandalia chakula na kuwatunzia siri? Hapa sitafuti sympathy, nataka tu kuonyesha kuwa mko tofauti.
Sijui kama umesoma alivyosema Abunuwasi - yeye ana wake baba mkubwa sasa na anamtunza. Labda "kifua" chako kidogo tu.
Nataka kujaribu kumpa mume wangu mtihani kumpima pressure kabla sijampa ishu, any idea how?.
Dadangu, ninachosema mimi ni cha kweli, sio nakuhukumu. ila nakupa tahadhari. kitu cha muhimu ni kwamba, kama utaendelea kukaa kimya, ndo jipu linaendelea kutunga kwa ndani.bora ulitumbue mapema ili kama litaleta kidonda, ukipeleke kwa daktari mapema upone na uanze kutembea vizuri. inauma sana kudanganywa,kulea mtoto ukijua ni wako kumbe sio. inauma sana, kwa hiyo ni lazima uwe tayari kwa lolote. Inavyoonyesha ni kwamba, wewe sio mtu mwaminifu. na sio mtu wa dini, mtu wa kawaida hawezi kudanganyika kirahisi hivyo.
Hiyo ilikuwa ni tabia yako, ndo maana nasema lazima ule pilipili uloiunga mwenyewe. nanilazima iishe, ndo upakue mboga ingine isokuwa na pilipili. jitahidi kufumba macho, to face this prob, na hakuna wa kumlaumu.ila Mungu ni wenye rehema, anaweza akakusaidia jambo hili likawa rahisi, lakini ni kwa miujiza ya Mungu, sio hivihivi.
Unavyoonekana ni kwamba, wewe sio mwanake layman. unaonyesha umesoma kidogo, hivyo hata mwili wako unaujua. ulijua kabisa siku zako za hatari ni zipi, na ambazo sio za hatari ni zipi. uliamua tu kuzaa na huyo mtu.mtu msomi kama wewe hawazi kuwa reckless kama hivi. ulifanya makusudi kabisa,na huyo mtoto ulitarajia iwe hivyo,ndo maana hata ulipopata mimba ulienda kumwambia jamaa hata kabla hajazaliwa, kwasababu ulijua kuwa umeamua kufanya ngono wakati wa siku za hatari ili umzalie jamaa huyo mtoto. siajabu huyojamaa alikuwa mtu wako wa zamani, au pengine jamaa ni handsome hivyo ulipenda tu upata photocopy yake kwenye tumbo lako.
the only remedy hapa kwako dada, piga magoti,mwombe Mungu, Okoka, ubadilishe maisha yako ili Mungu akusaidie uwe makini katika nyendo zako. katika maisha siku zote, kuwa nje ya Mungu ni hasara kama hizo. ona sasa shetani alikushauri ufanye ngono na huyojamaa, lakini sasa hivi ukiwa na matatizo amekuacha peke yako. shetani amekutelekeze? ndo maana nasema, jibu lako lipo kwa Mungu tu sasa hivi. kama ukifanya moyo wako kuwa mgumu, I tell you, this issue sio rahisi, itakugarimu sana. bora utafute msaada wa Mungu ndo pona yako, na ndo utaweza kufikia solution ya heri. Nenda kanisani, mara moja haraka sana, kaokoka na uanze kuwa mtaua.asante.