Mtoto wa Mugabe afukuzwa Afrika Kusini

Mtoto wa Mugabe afukuzwa Afrika Kusini

Mawele

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
941
Reaction score
3,288
Mahakama Nchini Afrika Kusini imeamuru Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, Bellarmine Mugabe, kufukuzwa Nchini humo baada ya kukiri kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria pamoja na ukiukwaji wa taratibu za uhamiaji.

Katika hukumu hiyo, Mahakama imeeleza kuwa Mugabe mwenye umri wa miaka 28 atatakiwa kulipa faini ya dola za Kimarekani 36,000 sawa na takriban shilingi milioni 93.6 za Kitanzania na kuagiza kurejeshwa Zimbabwe mara moja baada ya kukamilika kwa taratibu za kisheria.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa za kesi hiyo, Mugabe amekamatwa Februari 19, 2026 kufuatia tukio la kumpiga risasi Mlinzi wa Nyumbani kwake Mjini Johannesburg na kumjeruhi vibaya.

Pamoja na hayo, katika shauri hilo, Mshitakiwa mwenza Tobias Matonhodze amekiri makosa ya kujaribu kuua, kuishi Nchini humo kinyume cha sheria pamoja na kumiliki silaha isivyo halali na Mahakama imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia.
 
Mtoto pendwa anapolindwa kwa nguvu zote, ila angekuwa wa kajamba nani! hata huyo aliyechukua lawama, babea tu, dogo alishoot mwenyewe. Watoto wa waasisi wa uhuru ni spoiled sana kama hizi mbegu za CCM tu.
 
Back
Top Bottom