Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,965
Hivi karibuni kwenye mitandao mbalimbali kumeenea video kadhaa zikionesha raia wa Afrika kusini wakiwapiga na kuwafukuza raia kutoka maifa mengine barani Afrika kwa madai kwamba wamechukua kazi zao, pia ni sababu huduma nyingi za kijamii haziwafikii raia wa Afrika Kusini pamoja na hali ngumu kwa wakazi hao.
Baadi ya rai wa Afrika Kusini wameanzisha vikundi vya kuwataka raia hao warudi nchini kwao huku wengine wakivamia biashara na makazi ya raia wa kigeni. Lakini Serikali ya Afrika Kusini ilikaa kimya na sasa wamejitokea kufafanua hali halisi.....
--------------------------

Serikali ya Afrika Kusini imetangaza mpango wa kutuma wajumbe katika mataifa mbalimbali barani Afrika na sehemu nyingine duniani kufuatia kuongezeka kwa mashambulizi yanayowalenga raia wa kigeni wanaoishi nchini humo.
Akizungumza katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na Rais wa Kenya, William Ruto, uliofanyika Pretoria Juni 4, Rais Cyril Ramaphosa amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kushughulikia changamoto za uhamiaji.
Kauli hiyo imekuja wakati ambapo baadhi ya raia wa kigeni, wakiwemo wawekezaji, wamekuwa wakikumbwa na mashambulizi na kulazimishwa kuondoka katika maeneo mbalimbali ya Afrika Kusini.
Rais Ramaphosa amesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mfumo ulioratibiwa zaidi wa kusimamia uhamiaji, huku akizitaka nchi husika pamoja na wadau muhimu kushirikiana kwa karibu ili kutafuta suluhisho la kudumu na lenye ufanisi kwa tatizo hilo.