Kana-Ka-Nsungu
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,257
- 362
Naukumbuka msiba wa babu,wakati wa kula ulipowadia,
Sinia la ugali mkubwa, bakuli la mboga pembeni
Wanaume kumi wamelizungunguka,mtoto mimi peke yangu,
Bakuli la maji ya kunawa lawadia.Ile nataka nawa tu,"Mtoto wa nani huyu asiye na adabu? subiri wakubwa wanawe" aling'aka mmoja wa wazee.Hadi bakuli lanifikia,maji yalishakua meusiiii!! Kama hiyo haitoshi,nataka kuokota nyama zee jingine lanidaka mkono-"subiri wakubwa waokote kwanza", mtumee-hadi zamu yangu inawadia,mifupa mitupu!
Vichapo, vichapo, vichapo, si nyumbani si shuleni.
Wazazi wananichapa eti kwa kuwa nacheza mpira,wangenisupport enzi zile saa hizi si ningekua Madrid?
Hawataki nicheze, wanataka nisome,nioshe vyombo, nifue na kudeki, jumamosi na jumapili twende shamba tukalime-si ndio child labour hii wazungu wanaita?
Walimu nao -nikikosa namba asubuhi- viboko.Mbona hawaniulizi sababu, jana usiku nimekaa hadi saa 6, wazazi hawajasema kitu!Nikiwa mchafu kwenye ukaguzi-viboko, ntakuaje msafi wakati dingi hela ya soap hakuacha?.7 X 7 nikijibu 40- viboko, kwani ndo vitanipa majibu?labda nilikua dyslexic? halafu wakati wa brake saa 4 wenzangu wacheza ,mwalimu nanihii bila haya, aniomba nimuuzie mandazi na vitumbua vyake!
Jirani naye yumo, kampira kangu ka matambara na vipande vya godoro, nimekasuka kwa kamba ya manila na kukavisha sox-kanadunda kwelikweli,masaa karibu mawili metumia. Shuti la kwanza tu, boom-kametua bustanini kwake, mamaaa-bila huruma kakatia moto!Siku ingine basi hata siri asinifanyie, viboko vya bure kanisababishia -ndio nini kumuambia mama kuwa nimekula kwake wakati nilimuambia kuwa nimekatazwa na asiseme?
Serekali nayo haikuwa nyuma. Nanusurika kugongwa na gari kwa kucheza mpira barabarani, eneo langu lililotengwa kwa kuchezea wameliuza kwa mwarabu. Naumwa malaria, hospitali dawa hakuna, thanks to mkwinini lakini shubiri yake unaijua? Tofali ndio dawati langu, chini ya mwembe darasa langu- baba si aliniambia kodi analipa na hii ndo kazi yake?
Maskini mimi mtoto wa kiafrika, nina mengi ya kulalama, natamani ningezaliwa ng'ambo ambapo kero zote hizi waziita Child Abuse.