Mtoto sio baraka, ni wajibu wa maisha yako yote

Mtoto sio baraka, ni wajibu wa maisha yako yote

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
19,288
Reaction score
39,974
Kabla ya kuwa na mtoto hakikisha una mikakati na mipango thabiti kifedha kuweza kumhudumia mtoto. Kumbuka mtoto toka anazaliwa unawajibika kwake maishani mwake. Hata ukitangulia kufa atakutumia kama mzimu wake umsaidie. Kumleta mtoto duniani na kushindwa kumhudumia ni kinyume na haki za binadamu.

Inakera sana kuona mtoto wa miezi kadhaa kashaanza kuvishwa mitumba. Kuweni serious ndugu. Wengine vipato vidogo ila analazimisha kuwa na watoto wengi. Sio sawa hiyo. Hakikisha kabla hujamwagia ndani umejiridhisha utaweza kumudu mahitaji yake.
 
Mkuu kuna watu wamepambana lakini anafika 35 bado ramani hazisomi,
Tuje kwa wanawake wengi wao wakifika 35+ wanapata changamoto sana kujifungua salama,
Sasa watu wote wakisubiri wawe vizuri financially kuna uwezekano mpaka wanafika 50 wakawa hawana financial freedom

Acha watu waishi maisha yao
 
Kwani kuzaa ni lazima kama kula??
 
Kuzaa ni nature
Hata wakimbizi makambizi wamekimbia nchi zao wanazaa.

Congo, Iran, Sudan Kuna vita ila watu wanazaa

Kuzaa ni zaidi ya uweZo wako
Ni zaidi ya maandalizi na Mali

Hakuna mtu anaweza kumtunza binadamu mwenzake

Uzazi ni zaidi ya uelewa wako
 
Ukiwaza hivyo hutazaa, kuna watoto walivalishwa mitumba lakini leo hii ni matajiri wana mali na fedha nyingi hata hawakumbuki kama waliwahi kuvalishwa mitumba na wazazi wao
 
Back
Top Bottom