Mtoto alipoharibu

Mtoto alipoharibu

Habari za leo wapendwa,

Jamani leo shost mwingine amepata majanga, huyu niliwahi kufanya nae kazi sehemu flani lakini bado tunamawasiliano.

Kisa chenyewe ni kuwa, shost alipokuwa 30+ aligundulika na fibroids, kwakuwa hakuwa na mume wala mtoto, alikuwa desperate kupata angalau mtoto akihofia baada ya matatibabu anaweza akose kabisa.

Sijui makubaliano yalivyokuwa lakini alikutana na kijana Peter ambae ni engineer, Peter ana mke na mabinti wawili. Shost amebahatika kupata mtoto wa kiume, Peter amechanganyikiwa kwa furaha. Peter aliahidi kumtunza mama na mtoto, aliwapangishia nyumba nzima lakini mbali kabisa na nyumbani kwake, mfano iwe Gongo la Mboto na Mbweni.

Peter alihakikisha mara mbili kwa wiki alikuwa kwa shost akimuogesha mtoto, kumsomea bedtime stories mpaka mtoto akilala ndiyo anaondoka kwenda kwake. Mtoto alimfahamu baba yake na mara nyingi aliuliza kwanini baba hakai na sisi, si fahamu ni jibu gani wazazi walimpatia.

Mke wa Peter hakuwa na fahamu yeyote kwa haya yote yanayotekea. Kasheshe imekuja kipindi hiki cha sikukuu, shost alikwenda kumnunulia mtoto mahitaji ya sikukuu Mlimani City na kugongana uso kwa uso na Peter akiwa na mkewe na watoto wao.

Katoto ka shost masikini kamemkimbilia Peter daddy, jamani Peter aliishiwa nguvu, mke amekuja juu, inakuwaje mtoto apite watu wote aje akuite wewe daddy?
Khaaa wewe dada wa mie nawe hupungukiwi na vistori vya kuturusha roho sisi wananume,daaah what a coincidence?,yaani jiji looote hilo la Makonda jamani?,eti nakutana na katoto kangu ka mchepuko? daah nakosa pumzi aisee,na sasa hivi Venossa kaninywesha mbege ndo kabisaa siamini,tena Venossa kasema ati umetunga story au?
 
We espy, naona umeamua kuwa SPY. 🙂
Kui hebu njoo pm,maana umekaa mkao wa hasara kabisaaa au vipi?,nafikiri nikikupa ile inaitwa sakayosa au magoma moto ndio itakuwa heshima humu jukwaani baby au?,nataka ukirudi jukwaaani uhadithie jinsi gani nanihii ilikuwa taamu.
 
Habari za leo wapendwa,

Mke wa Peter hakuwa na fahamu yeyote kwa haya yote yanayotekea. Kasheshe imekuja kipindi hiki cha sikukuu, shost alikwenda kumnunulia mtoto mahitaji ya sikukuu Mlimani City na kugongana uso kwa uso na Peter akiwa na mkewe na watoto wao.

Katoto ka shost masikini kamemkimbilia Peter daddy, jamani Peter aliishiwa nguvu, mke amekuja juu, inakuwaje mtoto apite watu wote aje akuite wewe daddy?

Mimi ningejifanya na presha nakuzimia, nikija kuzinduka najifanya sikumbuki chochote
 
Mchepukaji ni mchepukaji tu, kama alikudharau mwanzo akachepuka na kukuletea mtoto, ukimchukua huyo ataenda kwa mwingine utaletewa mwingine.

Mwanamke kama uko hai walaa usikubali mwanao kulelewa na mama wa kambo.
Wala kulelewa na bibi au ndugu wa upande wa mwanaume.
 
Kabisaaaa,tatizo watu wana rahisisha sana.
Si kurahisisha ninadhani dhana kubwa ni kuhimiza waliathirika kuzingatia matibabu ili kuepusha maambukizi mapya, na pia walioathirika wakitumia dawa kikamilifu wanaweza kuishi maisha ya kawaida.
 
Ningekuwa mke wa Peter ningesema dogo aletwe nyumbani, mama yake atakuwa anakuja kumsalimia.
utawapa nafasi yakufyatua wengine!
Huyo rafiki yako amweke huyo dogo mbali na mke wa Peter kwani reaction yake kwa mtoto inaweza isiwe nzuri.

Hongera [HASHTAG]#sky eclat[/HASHTAG] kwa sababu hii story imekuwa short and clear sio zile za mwaka jana zilikuwa ndefu kama CV ya professor mwenye noble prize. Au ndio mwaka mpya mambo mapya. Ila collection ya threads zako za hii topic zinaweza kufanya a very good comic book with important underlying messages.
ningependa kuzichapisha kama short stories!
 
Si kurahisisha ninadhani dhana kubwa ni kuhimiza waliathirika kuzingatia matibabu ili kuepusha maambukizi mapya, na pia walioathirika wakitumia dawa kikamilifu wanaweza kuishi maisha ya kawaida.
Kweli lakini bado huwezi kuwa na amani uliyokua nayo mwanzo.
 
Kabisa, mpaka ukazaa it means yo ready to be a mom, kuwa responsible,lea mwanao mwenyewe.
Kwelii sababu mtoto inatakiwa alelewe na mama na baba lakini inapotokea hali kama hiyo mtoto alelewe na mama tu sababu sikuzote uchungu wa mwana aujue mama.
 
duh hapo mwanaume ajishushe akiri kosa maisha yaendelee.. ila walikosea walitakiwa wawe na mawasiliano in advance wasijekugongana duh.. mke halali anawakati mgumu
Lakin mchepuko unarlax shida iko kwa mtoto

Kwel dam nzito kuliko maji
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom