Mtoto alipoharibu

Mtoto alipoharibu

Mbona hapo kama yule kimada angekuwa na akili ya fasta ilikuwa ni ishu ndogo tu,

Wakati dogo anamkimbilia dady, yule bibie alitakiwa aende, kuanzisha story, shem vip? Mtoto kawamisi baba zake jamani, hamji kumtelembelea , so ingepata pa kumaliziwa.
Usanii kipaji mkuu, ukichanganya na panic usishangae mchepuko kujieleza pasipo kuulizwa swali.
 
Huruma kwa katoto .... Engineer kachemsha. He made his bed, now he must lie in it! Akimkana hapo mbele ya wife to save his skin, atamwelezaje tena akimtembelea?
Hakumkana ila alimchukua wife wakarudi nyumbani, shopping trip ilikwenda break.
 
Nlikuepo siku hiyo.

Ilivyokuwa;

Anatoka mwanamke mmoja aliyevalia suruali nyeusi isiyombana Sana na kiblauzi cha maua maua, kichwani akiwa amesuka kwa mtindo wa kisasa.
Anafungua mlango wa nyuma wa gari anatoka mtoto wa kiume wa miaka Kama minne Kama sio mitano.

Mwanamke anachukua simu yake na kupiga;
"Shosti"
Sauti kutoka upande wa pili kwenye simu inasikika.
"Shosti, ndio nimefika. We upo wapi?"
Mwanamke akajibu huku mkono mwingine ukishusha blauz kutokana na ufupi wake.
Anamaliza kuongea na simu akashangaa kutokumwona Mtoto wake.

Akiwa katika kuangaza macho yake Mara kwa nyuma mbali kidogo na alipo anashtushwa na sauti ya mwanae ikiita "daddyyyy!!!!!!"

Anageuka haamini macho yake kwa kile anachokiona. Anamwona mwanae akimkimbilia mwanaume mmoja ambaye yeye mwenyewe anaonekana kumfahamu vizuri.

Mwanaume huyo alikuwa na mwanamke ambaye ni dhahiri alikuwa mke wake na watoto wawili wakike ambao wote walionekana kumshangaa Mtoto huyu aliyekuja kumrukia Baba yao.

Nini kitafuata;;
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom