GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,571
- 108,922
1. Timu inacheza kwa Kasi kipindi cha Kwanza ila kipindi cha Pili inapungua. Na tatizo hili linaonekana pale tu Simba SC ikicheza Dar es Salaam ila kwa Mikoani Timu huwa inakuwa 'active' katika dakika zote 90.
2. Ugonjwa sugu wa Mabeki kutoicheza vyema Mipira ya Juu bado haujapatiwa Tiba ya Kudumu na kuna Uwezekano Washambuliaji makini wa Yanga SC wakaiadhibu Simba SC kwa huu huu Udhaifu na baadae ikaanza kutafuta Mchawi au kusema Mwamuzi ameionea na Kuwabeba Yanga SC.
3. Kipa Manula ana Mizaha isiyo na Faida kwa Timu, Kajiamini kupitiliza na kuna muda hupoteza Umakini ambao asipoonywa kuna Siku ataigharimu Klabu.
4. Wachezaji akina John Boko na Erasto Nyoni wasipewe sana Vipaumbele katika Mechi zenye Umuhimu kwani Wameshachoka ila wanalazimisha tu Kucheza Soka la sasa ambalo kwa Kasi yake hawaliwezi na matokeo yake Wanavurunda Uwanjani.
5. Beki Joash Onyango asipangwe dhidi ya Yanga SC kwani ana Mapungufu ya Kimsingi hasa ya Kuchoka haraka, Uzito mkubwa na Umakini Hafifu katika Kukaba hivyo kwa Mafowadi wazuri wa Yanga SC kama Mayele na Makambo anaweza Kuigharimu Simba SC.
6. Mchezaji Bernard Morrison aache kutaka Kujiona ndiyo Mfalme ndani ya Simba SC na acheze Kitimu zaidi kuliko kutaka kufanya Mwenyewe kila Kitu na akiharibu hakabi hivyo kutokuwa na Msaada kwa Timu pale ikianza Kushambuliwa.
7. Kuelekea Mechi na Yanga SC naishauri Simba SC kuanzia sasa ijiandae ama Kuchezesha Viungo Watatu ama Wanne ili waweze Kupunguza Nguvu Kubwa ya Yanga SC iliyopo na inayoanzia katika Kiungo chao.
8. Kuelekea Mechi na Yanga SC nashauri Wachezaji hawa akina Mohamed Hussein Tshabalala, Meddie Kagere, Jonas Mkude, Kibu Denis, Bernard Morrison na Larry Bwalya wasikosekane kwani kwa sasa ndani ya Ligi Kuu yetu hii ya NBC wameonyesha ndiyo Mhimili na Msaada mkubwa kwa Ushindi na Mafanikio ya Simba SC.
9. Kiungo 'Punda' Muzamir Yasin ana Msaada mkubwa katika Kuimarisha nafasi ya Kiungo ya Simba SC ila Makocha wa Simba SC na hata Watu wa Saikolojia wamsaidie kwani kuna muda huwa anacheza hovyo na ukimtizama vyema utahisi Mwili wake tu ndiyo huwa unakuwa Uwanjani lakini Akili (Fikra) zake huwa zinakuwa ama Kwake Dar es Salaam au Kwao kabisa Morogoro.
10. Kama kuna Zoezi muhimu ambalo Wachezaji wa Simba SC wanatakiwa kulifanya na ikiwezekana hata kupelekwa 'Tuition' ili waliweze ni la Kukaba Kiuhakika, Kutoridhika na Kubweteka na Ushindi wa Goli Moja au Mawili na Kutopunguza Umakini wao wa Kimchezo hasa dakika 30 za mwisho (Kipindi cha Pili)
11. Timu (Simba SC) ikicheza 'Kitimu' zaidi katika Mechi ya Yanga SC na Kukazia katika Mfumo wa 'Total Football' itashinda mapema tu ila ikicheza kwa kila Mchezaji kucheza Kivyake ili Kumfurahisha Mwekezaji Mo Dewji, CEO Barbara Gonzalez na Mashabiki Uwanjani Yanga SC inaenda Kuiadhibu tena na Simba SC sasa kuwa ni Mteja rasmi na wa Kudumu wa Yanga SC ambayo naisifu ikiwa inaenda Kucheza na Simba SC huwa inacheza 'Kimkakati' hasa ( zaidi ) na hufanikiwa na Kushinda.
Kwa Yanga SC hii Simba SC ikajidhatiti.