Mtizamo wangu wa 'Kiufundi' kwa Simba SC iliyocheza na Geita Gold FC na inayoenda Kucheza na Yanga SC 11 Disemba, 2021

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
44,032
2,000
1. Timu inacheza kwa Kasi kipindi cha Kwanza ila kipindi cha Pili inapungua. Na tatizo hili linaonekana pale tu Simba SC ikicheza Dar es Salaam ila kwa Mikoani Timu huwa inakuwa 'active' katika dakika zote 90.

2. Ugonjwa sugu wa Mabeki kutoicheza vyema Mipira ya Juu bado haujapatiwa Tiba ya Kudumu na kuna Uwezekano Washambuliaji makini wa Yanga SC wakaiadhibu Simba SC kwa huu huu Udhaifu na baadae ikaanza kutafuta Mchawi au kusema Mwamuzi ameionea na Kuwabeba Yanga SC.

3. Kipa Manula ana Mizaha isiyo na Faida kwa Timu, Kajiamini kupitiliza na kuna muda hupoteza Umakini ambao asipoonywa kuna Siku ataigharimu Klabu.

4. Wachezaji akina John Boko na Erasto Nyoni wasipewe sana Vipaumbele katika Mechi zenye Umuhimu kwani Wameshachoka ila wanalazimisha tu Kucheza Soka la sasa ambalo kwa Kasi yake hawaliwezi na matokeo yake Wanavurunda Uwanjani.

5. Beki Joash Onyango asipangwe dhidi ya Yanga SC kwani ana Mapungufu ya Kimsingi hasa ya Kuchoka haraka, Uzito mkubwa na Umakini Hafifu katika Kukaba hivyo kwa Mafowadi wazuri wa Yanga SC kama Mayele na Makambo anaweza Kuigharimu Simba SC.

6. Mchezaji Bernard Morrison aache kutaka Kujiona ndiyo Mfalme ndani ya Simba SC na acheze Kitimu zaidi kuliko kutaka kufanya Mwenyewe kila Kitu na akiharibu hakabi hivyo kutokuwa na Msaada kwa Timu pale ikianza Kushambuliwa.

7. Kuelekea Mechi na Yanga SC naishauri Simba SC kuanzia sasa ijiandae ama Kuchezesha Viungo Watatu ama Wanne ili waweze Kupunguza Nguvu Kubwa ya Yanga SC iliyopo na inayoanzia katika Kiungo chao.

8. Kuelekea Mechi na Yanga SC nashauri Wachezaji hawa akina Mohamed Hussein Tshabalala, Meddie Kagere, Jonas Mkude, Kibu Denis, Bernard Morrison na Larry Bwalya wasikosekane kwani kwa sasa ndani ya Ligi Kuu yetu hii ya NBC wameonyesha ndiyo Mhimili na Msaada mkubwa kwa Ushindi na Mafanikio ya Simba SC.

9. Kiungo 'Punda' Muzamir Yasin ana Msaada mkubwa katika Kuimarisha nafasi ya Kiungo ya Simba SC ila Makocha wa Simba SC na hata Watu wa Saikolojia wamsaidie kwani kuna muda huwa anacheza hovyo na ukimtizama vyema utahisi Mwili wake tu ndiyo huwa unakuwa Uwanjani lakini Akili (Fikra) zake huwa zinakuwa ama Kwake Dar es Salaam au Kwao kabisa Morogoro.

10. Kama kuna Zoezi muhimu ambalo Wachezaji wa Simba SC wanatakiwa kulifanya na ikiwezekana hata kupelekwa 'Tuition' ili waliweze ni la Kukaba Kiuhakika, Kutoridhika na Kubweteka na Ushindi wa Goli Moja au Mawili na Kutopunguza Umakini wao wa Kimchezo hasa dakika 30 za mwisho (Kipindi cha Pili)

11. Timu (Simba SC) ikicheza 'Kitimu' zaidi katika Mechi ya Yanga SC na Kukazia katika Mfumo wa 'Total Football' itashinda mapema tu ila ikicheza kwa kila Mchezaji kucheza Kivyake ili Kumfurahisha Mwekezaji Mo Dewji, CEO Barbara Gonzalez na Mashabiki Uwanjani Yanga SC inaenda Kuiadhibu tena na Simba SC sasa kuwa ni Mteja rasmi na wa Kudumu wa Yanga SC ambayo naisifu ikiwa inaenda Kucheza na Simba SC huwa inacheza 'Kimkakati' hasa ( zaidi ) na hufanikiwa na Kushinda.

Kwa Yanga SC hii Simba SC ikajidhatiti.
 

Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
14,224
2,000
Hakuna kitu kinaniuma kama mchezaji kuacha kukaba na kutembea uwanjani, wakati timu inashambuliwa, Jana nimeona KIBU ,BANDA MORISON, BWALYA, KAPOMBE wakipoteza wao Wana fanya Tu jogging

Nimewaona Geita Walikua wanakabia juu, ili Simba wasianze kucheza mpira nyuma, alafu Simba Walikua wanawaacha GEITA waanze wanakotaka wao
 

CARDLESS

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
3,620
2,000
Sijamaliza kusoma nimecheka hapo uliposema SIMBA waweke VIUNGO WANNE. Hiyo timu itakuwa inakaba balaa
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
58,616
2,000
Kwani Simba si huwa inashinda kipindi cha mvua, siku hiyo mvua itanyesha...
 

changaule

JF-Expert Member
Jan 10, 2020
1,779
2,000
Hili namba moja hukulifanyia uchunguzi vizuri. Kwanzia ujio wa kocha pablo na kocha mpya wa viungo, Simba kipindi cha pili wanakata moto. Simba imecheza mechi ya biashara na dodoma jiji ni mechi iliyochezwa mkoani lakini simba hawakukata moto kipindi cha pili. Tatizo la kukafa moto limeanza kwenye mechi dhidi ya ruvu uliochezwa mwanza. Ruvu waliisakama lango la Simba muda wote katika kipindi cha pili.
 

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,202
2,000
Umeona vizuri.
Simba hawajui kukaba hasa mabeki. Mpira wanaucheza kwa macho badala ya mwili. Hata Manula ana hill tatizo baadhi ya wakati.

Kosa LA Jana LA goli LA kwanza na LA pili LA Geita ni mwendelezo wa makosa ya magoli ya Galaxy Jwaneng na Yale ya Kaizer Chief.

Bado hakuna dawa. Mabeki wanakiuka principle. Katika 18 unacheza MTU na sio nafasi. Unarushwa mpira mmoja, unatua mguuni mwa mpinzani, anageuza kiulaini na kufunga. Mbele ya mabeki kibao.

Timu makini zinatumia huo udhaifu.

Wakati ni sasa.
 

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,202
2,000
Kuna lengine LA jicho LA tatu. Kocha inaonekana anaasisi mfumo was kupress na kuachia. Wachezaji wanakariri badala ya kuangalia mazingira.

Kama mmeona, wachezaji wanafanya makosa ya kutoa Pasi kwa kulazimisha na hatimae kunaswa au kupotea. Ndio ukaona mipira haikai katikati.

Sasa mfumo huo was kocha unahitaji total football kupanda wote na kushuka. Kwa nature ya wachezaji wa simba was kujisikia, ufadha na kujiamini Fulani hivi, kocha ana kazi kubwa.

Timu iko kwenye mpito wa mfumo. Wachezaji wengi sio wanyumbulifu na hawajitumi ipasavyo. Hebu tazama kwa mfano, kuna muda mchezaji Morrison ana moira, anapapatua kupunguza wapinzani, wachezaji wenzake wamejificha huwaoni kuhaha kutafuta nafasi na mbinu za kujitoa. Mpaka anaamua kupiga fyongo au kutwaliwa na mpinzani.
 

NAJYUZ

JF-Expert Member
May 10, 2021
475
500
Hili namba moja hukulifanyia uchunguzi vizuri. Kwanzia ujio wa kocha pablo na kocha mpya wa viungo, Simba kipindi cha pili wanakata moto. Simba imecheza mechi ya biashara na dodoma jiji ni mechi iliyochezwa mkoani lakini simba hawakukata moto kipindi cha pili. Tatizo la kukafa moto limeanza kwenye mechi dhidi ya ruvu uliochezwa mwanza. Ruvu waliisakama lango la Simba muda wote katika kipindi cha pili.
Mwanangu changaule una capacity kubwa sana ya kufanya analysis.

Bravo..
 

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
15,547
2,000
... Kwanzia ujio wa kocha pablo na kocha mpya wa viungo, Simba kipindi cha pili wanakata moto. Simba imecheza mechi ya biashara na dodoma jiji ni mechi iliyochezwa mkoani lakini simba hawakukata moto kipindi cha pili. Tatizo la kukafa moto limeanza kwenye mechi dhidi ya ruvu uliochezwa mwanza. Ruvu waliisakama lango la Simba muda wote katika kipindi cha pili.
Sio kukata moto, ni kuridhika. Mechi ulizoziona kama Simba haikukata moto ni zile ambazo Simba ilikuwa inapambana kutafuta goli (Biashara, Dodoma FC na Coastal Union). Mechi ambazo umeona kama Simba ilikata moto ni zile ambazo Simba ilikuwa na ushindi kipindi cha kwanza tayari (Ruvu, Red Arrows na Geita)
 

Huja

Member
Aug 7, 2021
37
125
Beki INONGA ni muhimu kuongeza sharpness ktk backline.
Ni wakati sasa wa kumuamuni beki Kennedy Juma...ili kumjengea confidence...kwa height yake ni msaada kwa cross ball

.Simba Full back right bado hazibadiliki namna zinavyoweza kusaidia...wakipata nafasi wao ni kupiga tu cross ya gombania goli.

Mkude ameonyesha utulivu, anavyopokonya na kutawanya mpira.

lakini bado quality ya Bwalya hachezi kwa kasi , nadhani pia bado ana mawazo ya uzito wa kuibeba timu....si mbaya akianzia bench kama sub ili kuisoma mechi na kupunguza pressure kichwani mwake.

Kibu Dennis aendelee kufundishwa utulivu, lakini ana kasi na nguvu kitu ambacho ni muhimu kwa soka la sasa

Boko amepoteza confidence....inayoondoa umakini wa kucheza kwa malengo.

Natamani kuona combinations ya MORRIS kushoto na BANDA kulia ...naamini kwa kasi na ujanja wao basi kwa beki pinzani hawezi kupanda ..


Muhimu kuliko yote SIMBA gym ni muhimu...soka la sasa pamoja na maarifa inahitaji nguvu pia
 

This is...

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
3,139
2,000
We jamaa una machale sana, kuna mda uwa unashtukia jambo fulani lakini umeshachelewa, yanga itawaonyesha simba kiwango chenu halisi mlichonacho Siku iyo kwa vitendo zaidi
mkuu hiyo Ni dabi haina Simba mbovu wala Yanga mbovu.Hakuna anayeenda akijiamini kushinda mechi,Ni DK 90 zinaamua.

Labda umeanza kuzifahamu simba na Yanga Jana.
 

Mtanzanias

JF-Expert Member
Jul 30, 2021
329
1,000
mkuu hiyo Ni dabi haina Simba mbovu wala Yanga mbovu.Hakuna anayeenda akijiamini kushinda mechi,Ni DK 90 zinaamua.

Labda umeanza kuzifahamu simba na Yanga Jana.
Tunaangalia timu zinavyocheza kiufundi ayo mambo mengine ya nje ya uwanja yanabaki kama yalivyo tunachoangalia kwa sasa ni mambo ya kiufundi zaidi ndani ya uwanja
 

Satan

JF-Expert Member
Aug 9, 2017
607
1,000
Kuzidiwa kupo.

Kuzidiwa kunafanya uone mapungufu mengi lakini haizii ubora na kiwango cha mchezaji.

Simba ilionekana bora kwasababu iliwazidi wengine. Na yenyewe ilizidiwa sana. Geita walikuwa bora sana. Kongole kwao.

Usijisifu una mbio, msifu anayekukimbiza pia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom