Tuwe wakweli, kwanza Mzee Pinda(our PM) ni binadam kama alivyo yeyote. Katika mazingira ambayo kamati ya Maadili haikumfikisha Kamati Kuu( kama ni kweli) basi lazima alalame akiwa kama human being( hapa kama mtu binafsi)!
Si kweli kabisa kwamba Mzee Pinda hana maadili kuliko anaowaongoza kama Makamba Jr, Magufuli(Dr), Migiro(Dr) et al!
Kama kalalamika hata kama siyo hadharani, nami namuunga mkono! Mtu kama Jaji Ramadhan, Mzee Bilal(V Pres) nae eti kamati ya maadili inatajwa ilimtosa. Labda kamati pia ilishauri na suala la umri, ila kuhusu maadili akili ya kawaida inagoma kuamini kuwa Dr Bilal, Jaji Ramadhan, Mzee Pinda na wengine wanaoheshimika katika jamii wamsshindwa kupenya kwenye kamati ya maadili.
Kwa anaefahamu atutajie wajumbe wa Kamati ya Maadili halafu kila mjumbe alinganishwe na wazee hawa watatu waliokatwa. Mzee Kingunge ameinyooshea kidole kamati kwayo pia kutokuwa na maadili kwa kuvunja kanuni!
Aliye leta hii mada ni muongo. Jina la pinda halikukatwa. Liliondolewa kwenye mchakato baada ya maridhiano.
Hawezi kulalamika kwa sababu hakuondolewa kwa vigezo bali kwa maridhiano kutokana na mazingira halusi.
Ukiwa kama kiongozi wa serikali bungeni ulikuwa na kila fursa ya kuhakikisha hoja ya mgombea binafsi iliyoafikiwa baina ya vyama vya upinzani na CCM inafikishwa bungeni na kujadiliwa hata kwa hati ya dharula ili kupanua wigo wa demokrasia nchini!
Badala yake ukalazimisha kuingiza miswada ya gesi na mafuta ambayo haikushirikisha wadau na ambayo wa-Tanzania wana mashaka nayo kwa hati ya dharula!
Sasa ona mambo yalivyokugeuka! CCM imekupiga teke eti huna maadili!
Hoja ya mgombea binafsi ingepitishwa na bunge saa hizi ungekuwa unapeta na wala usingebabaishwa na akina Nape!
Nadhani hili limekuwa funzo kwa viongozi wengine wanaodharau hoja zenye maslahi mapana kwa Taifa na si maslahi binafsi au chama fulani!
Wewe jamaa uwa muongo muongo kama Yericko juzi ulituambia leo Lowasssa anatoa waraka.Habari za uhakika nilizofikishiwa ni kwamba, waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akubaliani na yaliyotoka Dodoma katika harakati zilizofanywa kumpata mgombea urais wa CCM.
Pinda amedai kutokuridhishwa kwake na jina lake kaondolewa na kamati ya maadili huku watu aliokuwa akiwaongoza na kuwatetea kila kukicha bungeni wakipenya kwa kile alichokiita kuwa kwa utaratibu 'mbovu'
Pinda akionekana akilia kwa uchungu wakati ambapo John Magufuli alikuwa akitangazwa kama mgombea urais wa CCM mwaka 2015.
Aidha Pinda amedai kusikitishwa na jinsi ambavyo January Makamba alivyobebwa na mbeleko ya Kikwete kuingia tano bora huku akiwa na muda mfupi sana katika siasa.
Tutasikia mengi ila fukuto lililopo ndani ya CCM ni zaidi ya ujuavyo.
Habari za uhakika nilizofikishiwa ni kwamba, waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akubaliani na yaliyotoka Dodoma katika harakati zilizofanywa kumpata mgombea urais wa CCM.
Pinda amedai kutokuridhishwa kwake na jina lake kaondolewa na kamati ya maadili huku watu aliokuwa akiwaongoza na kuwatetea kila kukicha bungeni wakipenya kwa kile alichokiita kuwa kwa utaratibu 'mbovu'
Pinda akionekana akilia kwa uchungu wakati ambapo John Magufuli alikuwa akitangazwa kama mgombea urais wa CCM mwaka 2015.
Aidha Pinda amedai kusikitishwa na jinsi ambavyo January Makamba alivyobebwa na mbeleko ya Kikwete kuingia tano bora huku akiwa na muda mfupi sana katika siasa.
Tutasikia mengi ila fukuto lililopo ndani ya CCM ni zaidi ya ujuavyo.
Ukiwa kama kiongozi wa serikali bungeni ulikuwa na kila fursa ya kuhakikisha hoja ya mgombea binafsi iliyoafikiwa baina ya vyama vya upinzani na CCM inafikishwa bungeni na kujadiliwa hata kwa hati ya dharula ili kupanua wigo wa demokrasia nchini!
Badala yake ukalazimisha kuingiza miswada ya gesi na mafuta ambayo haikushirikisha wadau na ambayo wa-Tanzania wana mashaka nayo kwa hati ya dharula!
Sasa ona mambo yalivyokugeuka! CCM imekupiga teke eti huna maadili!
Hoja ya mgombea binafsi ingepitishwa na bunge saa hizi ungekuwa unapeta na wala usingebabaishwa na akina Nape!
Nadhani hili limekuwa funzo kwa viongozi wengine wanaodharau hoja zenye maslahi mapana kwa Taifa na si maslahi binafsi au chama fulani!
KANU ilipotea kwenye ramani kwa kumbeba Kenyatta ambaye hakuwa chaguo la wengi na Mwai Kibaki akaibukia upinzani na kushinda