Ilikuwaje Waziri mkuu Pinda aulilie Urais

JET SALLI

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2014
Posts
2,995
Reaction score
2,047
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, alimwaga chozi ndani ya mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kulilia urais.Anaandika Saed Kubenea… (endelea).Taarifa zinasema, Pinda alimwaga kilio hicho wakati John Pombe Magufuli, akitangazwa mshindi.Majina matano ya wasaka urais kupitia CCM, yaliyowasilishwa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, ni January Makamba, Membe, Dk. Asha-Rose Migiro, Balozi Salum Ali na John Magufuli.Taarifa zinasema, majina hayo yalipatikanakabla ya vikao vya chama vilivyofanyika ili kumbeba mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo.Mkutano mkuu wa CCM ulioteuwa mgombea wake urais, ulianza Jumapili iliyopita na kumalizika siku iliyofuata – Jumatatu,13 Julai 2015. John Pombe Magufuli, ndiye aliyeibuka mshindi miongoni mwa wagombea 38 waliojitokeza kuomba nafasi hiyo.Taarifa kutoka makao madogo ya CCM, Lumumba na Ikulu zinasema, majina hayo matano yalichongwa kwa ustadi mkubwa na watu kutoka Idara ya Usalama ya CCM ili kumnufaisha, Bernard Membe, mmoja wa walioapa kusaka urais kufa na kupona.Pinda hakupatikana kueleza kwa undani kilichosabisha kumwaga chozi hadharani.Hata hivyo, wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema, kilichomliza Pinda, ni hatua ya Kikwete ya kumchinja katika hatua za awali, wakati alikuwa na sifa zote za kufikishwa Halmashari Kuu ya taifa (NEC) ya chama hicho.Habari zinasema, kabla ya kuchukua fomu, Pinda alikutana na Rais Jakaya Kikwete ili kuomba ridhaa ya kugombea nafasi hiyo. Kikwete aliridhia suala hilo.“Pamoja na kwamba Kikwete aliombwa na watu wengi, lakini ilitegemewa kwa kuwa Pinda ni mmoja wa wasaidizi wake, basi angehakikisha kuwa anampitisha na kumuingia NEC,” anaeleza mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Kondo Tutindaga.Msaidizi mwingine wa Kikwete ambaye alikuwa mmoja wa wagombea urais na ambaye jina lake liliondolewa katika hatua za awali, ni Dk. Mohammed Gharib Bilal, makamu wa rais wa Jamhuri.Anasema, “…uzito wa hoja yangu umejikita katika msingi mmoja. Kwamba, viongozi hawa wawili (Pinda na Bilal), walitakiwa wapigiwe kura ama katika CC au NEC.“Ilitakiwa washindwe kwa kura kidemokrasia, kuliko kutupwa na kamati yamaadili na hivyo kushindwa kuingia katika watano bora,” anaeleza.Anaongeza, “kwangu mimi, ilikuwa bora hata kubadili kanuni ili kuongeza wigo wa idadi ya wagombea kuliko kulazimika kuwaacha watu ambao ni msingi wa umojawa taifa, ikulu yetu na chama tawala.”Anasema, “watu wanajiuliza. Inakuwaje tunakuwa na waziri mkuu, makamu wa raisna jaji mkuu mstaafu ambao wana mapungufu makubwa yasiyoruhusu kupigiwa kura mbele ya vikao vya chama?”Pinda aliyekuwa ameapa kufia katika mbio za urais, jina lake liliondolewa katika hatua za awali za kinyang’anyiro hicho.
 
Waziri Mkuu asiye na maadili.

Inawezekana alionekana hana maadili kutokana na kauli yake ya 'wapigwe tu'.
 
Pinda alionyesha udhaifu wa hali ya juu kulia bungeni kipindi kile, Kuhusu jaji miye naona ni mchanga kisiasa sbb wanajeshi hawaruhusiwi kujihusisha na siasa hata majaji vile vile.
 
wote waliondolewa hawakuwa mpango wa mungu kuongoza taifa hili maana,hata vitabu vitakatifu vinasema hakuna mwanadamu ambaye anaweza kupinga mipango ya mungu alichokipanga munga hakuna mwanadamu wa kukitengua,
so MAGUFULI ni chaguo sahihi,
 
Kalale nayekitandani ukiamka utupe majibu kama kweli ni chaguo la Mungu au shetani.
 
Pinda ni aina ya watu ambao siku wakinyimwa unyumba na memsap wanalia ili tu kutafta kuhurumiwa. Yaani machozi ni kinga yake asiteswe /asishambuliwe Zaid.
 
Pinda ni aina ya watu wanaojua kulia na si kuchukua hatua,viongozi wa aina hii si msaada kwa Taifa na kuengiliwa kwake kulidhihirisha hayo.
 
Back
Top Bottom