Mti ulioanguka zamani wasimama ghafla

Mti ulioanguka zamani wasimama ghafla

Huo mti umeleta tumaini jipya kwa waathirika wa virusi vya ukimwi! Wapeni gamba lake wachemshe maji lita moja basi! Ukimwi bye bye! Oohh! Tumepata dawa ya ukimwi.
 
Hayo ndiyo maajabu ya dunia;

Wiki tatu zilizopita pale mbezi mwisho kwenye stend mpya kabla ya kukuta kale kasoko pana msitu;
kuna mtoto alikuwa analia humu mchana kweupe, walikuja polisi na mbwa wao kunusa ila hakuna kilichoonekana, lakini mtoto anaendelea kulia, mwisho kila mtu akaondoka kimya kimya;

Kisa kingine cha mti ulioota majani nikiwa nautazama huko mbeya nacho ni cha kushangaza.

Tuishie tu kusema duniani kuna vituko.

Chei Chei shangazi au??
 
Kama ni paper basi Tangopori na kama ni kitabu cha hadithi basi Kusadikika.
 
niliiona TBC km siku nne hivi zilizopita..na watu wakawa wanachukua magome...was very interesting...ila ni eneo zuri la research nahisi kuna mchezo...
Uliona nini TBC? Uliona mti ukianguka, ukiungua kisha ukaona unasimama wenyewe au ulionyeshwa na TBC mti uliosimama afu zikafuata story za paukwa pakwa? What actually did you see? Mnadanganyikaga kirahis sana kwa kukosa udadis. Nina uhakika kwa kuwajua wabongo wote watabora wanaowaaminisha ukimbana mmmoja mmoja atakwambia kasikia mwisho utagundua hakuna hata mmjoja alieshuhudia. Hapo kuna mwendawazim mmoja kaamua kulianzisha na kusepa kawaacha wafuasi watiifu wa tetes wanasambaza umbea. Uzuri wa nchi hii hata vyombo vya habari navyo havina kinga ya kuviokoa kutumbukia katika huu ujinga. Ningekuwa mmiliki wa chombo cha habari then kirushe ----- huu mtangazaji muhusika hana kazi.
 
ha haa kuna kabinti kalikua kakiona mti ukisimama mdogomdogo....akamwambia dingi ake angaliaa mti unasimama.... mysterious, myth, consipiracy, fact..
 
Mti aina ya msufi ulioanguka miaka mitatu iliyopita, na baadae kuungua na moto wilayani Uyui mkoani Tabora, leo mchana katika hali ya maajabu umesimama wenyewe huku baadhi ya wananchi wakishuhudia.
Baadhi ya wananchi wameurukia ili kupata angalau gamba lake kwa imani za kishirikina.
Fiction!
 
ha haa kuna kabinti kalikua kakiona mti ukisimama mdogomdogo....akamwambia dingi ake angaliaa mti unasimama.... mysterious, myth, consipiracy, fact..
umenikumbusha consipiracy theories. Mbaya zaidi huwa zinatumika kuhadaa simple mind people kwa manufaa ya watu fulani au kikundi. Marekani baada ya NASA kutafuna pesa nyingi ikitafiti uwezekano wa kuishi katika space kwa muda mrefu bila ya majibu ya kueleweka wamarekani wakaanza kuisakama NASA kuacha kupoteza hela zao. Kwakuogopa kunyimwa fedha za utafiti NASA ikalianzisha ikaja na kituko cha kuwa wamegundua viumbe hai vyenye akili kuliko binadam na vinaishi katika space wakasema wameokota mabaki ya chombo chao. Waandishi wakaonyeshwa mabaki hayo watu wakaamini, wakaogopa kuwa hao viumbe wanaweza kuwashinda kivita. NASA akaonekana inatakiwa kuchunguza zaidi, ikashinda vita, wajinga ndio waliwao. Wenyewe waliviita UFO yaan unidentified flying objects. USHAURI, katika dunia yetu hii ya utapeli, ujinga ni mtaji mkubwa sana wa kujipatia chochote. DAWA, ili kupona na kutogeuzwa mangungo wa leo ni kuzingatia Falsafa ya JK. ya mbayuwayu, AKILI ZA KUAMBIWA ONGEZA NA ZA KWAKO, vinginevyo utakutwa uwanja wa ndege ukisubiri kwenda iraq kuhubili injili kwa kiswahili tena bila nauli.
 
Yale yale ya watoto watatu wametekwa Mbagala! Ukiuliza majina ya hao watoto na majina ya wazazi ama walezi wao, hakuna yeyote anayeyajua.Wala hakuna yeyote ajuaye hao watoto walikuwa wanaishi nyumba zipi.
Ndio maana tulikuwa wengi mno kule Samunge kwa babu.
 
Back
Top Bottom