Mti ulioanguka zamani wasimama ghafla

Mti ulioanguka zamani wasimama ghafla

Unashangaa msufi mmoja kusimama wenyewe, kwetu sie pale kona ya uyole kila siku tunashuhudia zaidi ya hiyo.
 
Nilijua tu lazima ije topic ya maajabu watu wajikite huko. Ukisikia elimu inashuka thamani majibu yake ndo hayo wakati wenzetu wanakuza sayansi sisi tunarejea ndoto za alfu lela ulela au adili na nduguze za miti kusema na wanyama kuwa watu. Hiyo ni Tanzania at 50 au at karne ya pili BC
 
That is why Tabora is one of the poorest region in Tanzania.
 
Kama ni kweli hiyo habari, basi huo utakuwa ni muujiza wa hali ya juu na hapo mahali panafaa kujengwa mnara wa makumbusho, ili watalii wa ndani na nje ya nchi wawe wanamiminika mahali hapo kuushuhudia huo muujiza wa hali ya juu.

Mungu ni mkuu kuliko kitu chochote na huo muujiza ameufanya ili binadamu watambue uwezo wake wa kutenda miujiza ili waendelee kumuabudu na kumtukuza.
Huu sio muujiza wa Mungu, ni mizimu ya hayo maeneo, Mungu ausimamishe huo mti ili iweje? Ni sarakasi za wachawi
 
Wonders will never end....! Niliona mtu anasema nimepita hapa kwenda nyumbani, mti ulikuwa chini sasa hivi umesimama...kweli ni maajabu.
 
Tutofautishe kati ya facts na opinion, fact ni kwamba mti ulioanguka na kuungua moto miaka mitatu iliyopita umesimama wenyewe kwa mlio mkubwa huku watu wakishuhudia, picha zimechukuliwa. Sasa umesimamishwa na nini, hapo ni opinion kila mmoja, sasa ninyi kama GT mtoe opinion zenu. Maoni yangu mimi ni mizimu ya hilo eneo ikishirikiana na wachawi. Mnakumbuka msemo wa kila mbuyu na shetani wake? Wakati fulani hii miti mikubwa inakuwa na mashetani au majini/mizimu fulani, ili ijenge imani kwa watu inaweza kufanya miujiza fulani ili kuongeza wafuasi, hayo ni yangu, yenu je?
 
Hata mie ninayo hiyo ckip ila nimeshindwa kupload.
 
Habar ata mm nimeisikia kwenye taarifa ya habari Tbc fm ila imenishangaza sana

Wenye kumbukumbu za kutosha watuhabarishe hii habari kwani inasemekana kwamba kwa miaka mitatu au minne iliyopita kuna mti ulikuwa umeanguka chini kwa muda mrefu huko kitongoji cha BURONGO kijiji cha BUKUNGU kata ya BUKUNGU tarafa ya UKARA wilayani UKEREWE. Wanawake walikuwa wameshaukata huo mti kwa kuchanja kuni. LAKINI ULISIMAMA GHAFLA. Inasemekana lilikuwa ni tukio lililowashangaza watu wengi wa kisiwa hicho
 
Cha ajabu wanauharibu wa nini? Imani zingine bwana View attachment 194173

Watu waTabora, Shinyanga na Mwanza wanaamini mti ukihusishwa na tukio lolote basi unageuka kuwa dawa, mf. Mtu akijinyonga kwenye mti, huo mti utagombaniwa kama mpira wa kona, au mti ukipigwa na radi baada ya siku chache utakwisha kwa kukatwakatwa kwa ajili ya dawa, hivyo hata huu mti baada ya siku chache hautakuwepo. Mtazamo wangu ni je, nguvu iliyotumika kuusimamisha haitawadhuru watumiaji wa hiyo dawa?
 
Watu waTabora, Shinyanga na Mwanza wanaamini mti ukihusishwa na tukio lolote basi unageuka kuwa dawa, mf. Mtu akijinyonga kwenye mti, huo mti utagombaniwa kama mpira wa kona, au mti ukipigwa na radi baada ya siku chache utakwisha kwa kukatwakatwa kwa ajili ya dawa, hivyo hata huu mti baada ya siku chache hautakuwepo. Mtazamo wangu ni je, nguvu iliyotumika kuusimamisha haitawadhuru watumiaji wa hiyo dawa?

Hata woga hawana, wataanza kuuza kama dawa ya maradhi sugu, yetu macho
 
Eti Emmanuel Okwi karudi toka UGANDA nasikia FUFA walimzuia!?

Dah! Unamaanisha huamini kabisa, je ukiona kule Ileje ambako wakati wa masika chumnvi inaota kama uyoga, watu wanakusanya na kuunga kwenye mboga? Au kule Rungwe kijiji cha kanyelele ambako kuna chemichemi za maji zenye harufu Cocacola, sasa hivi eneo limeporwa na watu wa Pepsi, au kule Kalenga ambako lile eneo alilokufa mama yake na Mkwawa ukipita lazima uchume majani utupe kwenye jiwe fulani sasa ole wako ujifanye mjanja......utakoma !!
 
Mm namsubiria Mo11 akomenti kwanza kuwa " ipo cku maajabu yatashangaa vituko vya binadamu"
 
Nimeshindwa mkuu ila nipe whatsapp nambar yako nikurushie
 
Back
Top Bottom