Geita: Mti ulioanguka miezi mitano iliyopita wainuka na kuanza maisha tena

Excel

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
19,745
10,078
Mti mkubwa ulioangushwa na upepo miezi mitano iliyopita umewashangaza watu katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita baada ya kuamka wenyewe na kuanza maisha yake kama kawaida.

Tukio hilo la kusitaajabisha limetokea katika Kata ya Nanda iliyopo wilayani Mbogwe mkoani Geita, baada ya mvua kubwa kunyesha usiku EATV imefika eneo la tukio na kuzungumza na wanafamilia wanaomiliki mti huo wanasimulia tukio lilivyokuwa.

"Niliamka asubuhi watoto wanasema mti umesimama nikasema kweli nikavaa haraka haraka na mimi kutoka nje nikaona mti umesimama kweli," amesema Samwel Somi, mmiliki wa mti.

"Usiku huo kulinyesha mvua kubwa yenye upepo hatukujua sababu ni nini kuamka asubuhi tunaona mti umeamka kama unavyoona na tulivyokuwa tumeukata matawi sasa unaanza kuchipuka tena, " ameongeza mmoja wa wanafamilia hao.

Kwa upande wao wananchi wa Kijiji hicho wanasema ni mara yao kwanza tukio kama hilo kutokea katika eneo lao.

"Mimi hili tukio nimelisikia ila mimi nilishuhudia kuna kipindi mvua ilinyesha mti huu ukaanguka baada ya siku nikasikia ule mti umeamka mmmh nikasema si waliukata eeh waliukata matawi lakini umeinuka na umeanza kuchipuka tena," amesema jirani.

Diwani wa Kata ya Nanda Matius Lugoda akizungumza na EATV amewaomba wananchi kuwa watulivu na kuacha kuusisha tukio hilo na imani za kishirikina.

#Ea
FB_IMG_1697112629212.jpg
 
Mimi siyo msoma nyota lakini...
Huu mti ulikuwa unatabiria mambo makubwa. Muda wake wa kuanguka na muda wake wa kusimama tena unaendana kabisa na sintofahamu tuliyoipitia kwa kazia ya Tanganyika na bandari zake kupelekwa utumwani Uarabuni. Mti umesimama tena maana yake mazeli ameachana na mpango huo hivyo sasa nchi yetu itachipua tena.
Kama mnabisha mwambieni arudishe tena ule mkataba muone kama mti hautalala tena :):)

Nawakumbusha tu kuwa mandamano ni tar 9/11. Ukisoma vibaya inakuwa sept 11.
 
Picha ya ulivokua umeanguka iko wap, zaidi ya hapo ni story za kubumba watu wanakimbizana na trending news, shame on EATV journalism gan bila vithibitisho.
 
Mti mkubwa ulioangushwa na upepo miezi mitano iliyopita umewashangaza watu katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita baada ya kuamka wenyewe na kuanza maisha yake kama kawaida.

Tukio hilo la kusitaajabisha limetokea katika Kata ya Nanda iliyopo wilayani Mbogwe mkoani Geita, baada ya mvua kubwa kunyesha usiku EATV imefika eneo la tukio na kuzungumza na wanafamilia wanaomiliki mti huo wanasimulia tukio lilivyokuwa.

"Niliamka asubuhi watoto wanasema mti umesimama nikasema kweli nikavaa haraka haraka na mimi kutoka nje nikaona mti umesimama kweli," amesema Samwel Somi, mmiliki wa mti.

"Usiku huo kulinyesha mvua kubwa yenye upepo hatukujua sababu ni nini kuamka asubuhi tunaona mti umeamka kama unavyoona na tulivyokuwa tumeukata matawi sasa unaanza kuchipuka tena, " ameongeza mmoja wa wanafamilia hao.

Kwa upande wao wananchi wa Kijiji hicho wanasema ni mara yao kwanza tukio kama hilo kutokea katika eneo lao.

"Mimi hili tukio nimelisikia ila mimi nilishuhudia kuna kipindi mvua ilinyesha mti huu ukaanguka baada ya siku nikasikia ule mti umeamka mmmh nikasema si waliukata eeh waliukata matawi lakini umeinuka na umeanza kuchipuka tena," amesema jirani.

Diwani wa Kata ya Nanda Matius Lugoda akizungumza na EATV amewaomba wananchi kuwa watulivu na kuacha kuusisha tukio hilo na imani za kishirikina.

#EaView attachment 2779962
Kawaida sana hiyo
 
Mimi siyo msoma nyota lakini...
Huu mti ulikuwa unatabiria mambo makubwa. Muda wake wa kuanguka na muda wake wa kusimama tena unaendana kabisa na sintofahamu tuliyoipitia kwa kazia ya Tanganyika na bandari zake kupelekwa utumwani Uarabuni. Mti umesimama tena maana yake mazeli ameachana na mpango huo hivyo sasa nchi yetu itachipua tena.
Kama mnabisha mwambieni arudishe tena ule mkataba muone kama mti hautalala tena :):)

Nawakumbusha tu kuwa mandamano ni tar 9/11. Ukisoma vibaya inakuwa sept 11.
Ikibainika mti haukuanguka itakuwaje sasa na huu ushirikina ulionao mkuu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom