Mtengenezee Mwanao kesho yake. Asije kuwa chawa wa hawa chipukizi wa leo

CONTRARIAN

JF-Expert Member
Jun 21, 2023
922
2,793
Mtengnezee Mwanao kesho yenye furaha, mafanikio, malengo n.k.

Asitarajie kuishi kwa kuamini Serikali yake itamfanyia Jambo zuri kwa ajiri yake, Mfanye awe wa kujiamini awe wa kujitegemea, ajue furaha yake mtengenezaji ni yeye, ajuae kuna disappointments nyingi sana huletwa na uliowategemea wakurahisishie mambo, Awe jasiri, atarajie asichotarajia katika safari yake ya mafanikio.

Kwa kujua hayo na suprise nyingne nyingi hata laumu yeyote, Ila mwisho wa yote Usiomugopeshe Mwambie Maisha sio Magumu, ugumu unaletwa na Binadamu, na yeye ni mwenye future yenye mwanga, yote atakayokutana nayo njiani ni safari kufuta mwanga ndani ya kiza.

Muandae kiuchumi, ki elimu, kifikra, Epuka kumtengenezea mwanao mazingira ya baade kulazimika kua CHAWA wa hawa Machipukizi, kuishi kwa kumtegemea Binadamu mwenzako ni laana, Wapo watu walimwita binadamu mwenzao "Mweh...mweh... Mwehshimiwa mungu" leo hii mungu wao yupo jikoni.

Ukileta utani ukoo wote mnaishi kwa kusononeka tuu laasi mue machawa.

Babu Alishikwa na Mkoloni akamfunga nyororo, akamtumikisha akamchapa, Babu akakata moto,
Mkoloni Akamkabidhi kijiti Mchonga

Baba akangukia mikononi mwa Mchonga, Baba akakimbizwa aijenge nchi ili mwanae uje kuishi vizuri, Mzee ruksa akaendeleza gurudumu baba akaishia Pumzi.

Wewe PENGINEukakimbizwa Kuanzia kwa BEN, Msoga, Jiwe, sasa sa100 na bado, Asaivi ubao hausomeki..

Pambana mwanao asijekukusingizia wewe,
Masula ya kulaumu nimetoka familia duni, mwisho ni miaka 30, ukizidi hapo wewe ndio familia Duni sasa.

Cc Chawa wa leo.
 
"If the end is good, then everything was good"

By reyzzap

BTW chawa wote ni wakusaga na dole gumba, yale makubwa ni yakuponda najiwe.
 
Back
Top Bottom