Mtela Mwampamba afunguka ndani ya Passion FM

Mtela Mwampamba afunguka ndani ya Passion FM

Binafsi nimesikitishwa sana. Naona huruma kwa Mtela Mwampamba, ni kama amepata tatizo hivi katika ufahamu wake. Kwa bahati mbaya CCM watamtumia mpaka mwisho, kila atakachotaka kuzungumza kwenye public kuhusu cdm na Dr.Slaa wanamwambia hakuna shida, tena wanampongeza sana.
 
Hahahaha Nape lilimuuma kamtuma Mtela, doh

Sioni kama hoja ina mashiko
 
Hoja ni hoja ikiwa ina uzito na imebeba yale yanayotafsirika kuwa vigezo vya hoja kuitwa hoja.,binafsi naiona kuwa hii ni hoja kwani inatoa taswira ya namna kiongozi huyu aliyezeeka "BABU" ilivyokithiri Utata. Amedumu na Uhawara kwa muda mrefu na kupelekea mtoto wa nje ya ndoa.,lakini pia amenyang'anya mke wa mtu hadharani, amedhulumu pesa ya kanisa kiasi kupelekea kufukuzwa kanisani, lakini pia ameendelea kufanya matukio ya kutatanisha kiasi sasa tunapata shida kumpa tafsir katika jamii yetu.Babu yetu huyu anazeeka vibaya sana.
 
Yaani kijana mdogo anakuja na hoja za matusi, then zinakuwa national news? CCM mnatupeleka pabaya. Huyu kijana nahisi ndio wale walioandika matusi katika karatasi za majibu form IV
 
Unajua ni nini Mtela Mwampamba Ishu zote mbili za Dr na za Nape ni propaganda but zina tofauti sana moja itakufa coz sie kama wananchi tunaona haina mashiko as Slaa sio jina la mtu yeyote mwenye nyazifa wala hajajitanabaisha kama mtoto wa kigogo so hata akituambie huyu ndie baba yangu halisi bado tutamuangalia kwa jicho la kawaida tu as long as ni babake but angekuja na kutuambia Lowassa ndiye babake watanzania wote wangehamaki ukiwemo.

Ukija na kusema Nape ambaye tayari watu walishahamaki kusikia kuwa ni mtoto wa kigogo fulani then ukaja tena kusema yule kigogo siyo kwa kweli hilo tayari ni doa. Angekuwa ni mtu mwingine nisingekuwa na haja ya kukwambia kwa nini, lakini kwa kuwa uwezo wako bwana Mtela Mwampamba naufahamu basi wacha nikwambie sababu.

Dr. hajalitumia jina hilo kama ngazi ya kisiasa, amepanda kwa uwezo wake binafsi, but Nape katumia jina la Nnauye kama ngazi za kupanda kisiasa hilo liko dhahiri, fikiri angekuwa anaitwa Nape Taswira leo ungeweza hata kumsikia?? Tafakari chukua hatua

Hapo ndipo ilipo hoja,yakuwa flani amefikaje alipofika, its your turn now to choose material n immaterial bwana Mtela/Taswira
 
Mwapamba Acha kuchanganya, kama ni kweli una siasa hizi za kipuzi, tungekosea sana kukuchagua mwaka 2010 kuwa mbuge wetu.Jenga hoja siyo kufanya Personal Attack Ongea maswala siyo kuongelea watu nchi yetu ina matatizo mengi sana ya kuinua maisha ya watanzania kuliko kufanya uigizaji wa namna hii unavyofanya. Na kama utaenda na siasa hizi mbozi ukitegemea kuna mtu atakuunga mkono sijui, bado una muda wa kujirekebisha .
 
ccm watakagawa haka kanchi kwa kila aina ya uchafu, mara ufamilia, ukabila, udini, sijue nini tena wanataka!

Huyu mjinga mwingine naye anatuletea habari za Mwigulu na Lameck! Jamaa anahaibisha kabisa ukoo wake na watu wa Mbozi!
 
Kaka mnatutia aibu mwanyakyusa wenzako. Nilikuwa na matumaini sana na wewe, umeniangusha kaka, na utapotea muda si mrefu kwenye ulingo wa siasa. JIulize Dr lamwai yuko wapi? Hapo ndipo utakajua ccm sio.
 
njoo mbozi bas mwampamba mbona wakazania dar tu,njoo uku tukupige mawe msalit mkubwa wewe,afu umekuja kipind kigum ktk siasa za tanzania kwan saiv town ni stor za makanisa,gas,cdm aka sera za majimbo,matokeo ya form 4 so nadhan utapotea mapema sana ktk siasa za kibongo
 
Mtela na shoza toka walipofukuzwa cdm wamebaki wanatapatapa hawana point za kuongea, nawashauri watafute kazi za kufanya mana siasa zimewashinda na nawahakikishia wataishia kuropoka tuu
 
Huyu chalii hana mpya kabisa halafu namfahamu. Vizuri ipo siku nitamfungukia hadi ataenda TLP manake CCM wakimjua watamtoa mbio!'
 
Mnaoendelea kujadili ndio mnamfanya huyo Mwampamba ajilne kuwa ana jambo la kujadiliwa ....nawashauri kuwa tuishie hapa na mjadala kwani Mwampamba ni nani hata kwenye vyeo vya kisiasa? Hajawahi kuwa hata mwenyekiti wa tawi sasa huyu mnamjadili kwa lipi, hoja hana juu ya anachosema ....we should not waste our valuable time please .....
 
Huyu jamaa siasa zake sijui za wapi.Anang'ang'ania 'personal attacks' zisizo na tija. Lakini 'small minds...'
 
Wewe unaona kiongozi wa juu kabisa wa chama kudanganya baba ni issue ndogo hiyo? Mwacheni ajibu mwenyewe kama alivyojibu kuwa anamili kadi ya CCM. Mbona mke alipoguswa aliibuka na kusema yeye ni wa ukweli na kuwadhalilisha akina ROSE KAMILI na CECILIA PARRESSO.

Yeye kudanganya baba ama mzazi (kama mnavyotaka tuamini), ndo kumeifanya nchi hii kuwa masikini wa kutupwa kiasi hiki? Ndo kumesababisha migogoro ya kidini iliyozuka hivi sasa? Ndo kumesababisha matokeo ya kidato cha nne kuwa mabaya kupindukia? Ndo kunasababisha kutamalaki kwa wizi na ufisadi nchini? Ndo kunaifanya seroikali ya nchi hii kuwa dhaifu kiasi ya kwamba inashindwa hata kutatua matatizo yetu? Ama ndo kumelifanya bunge letu kuwa kichaka cha wahuni wanaotetea maslahi ya matumbo yao na chama chao, na kuwasahau wananchi waliowachagua?
Ndo kumemfanya mwenyekiti wako na chama chako kwa ujumla kuwatelekeza watanzania, kuamua kuhubiri migawanyiko na chuki za kidini, kimakabila na kikanda? Ndo kumewafanya mshindwe kabisa kutekeleza hata robo ya ilani yenu ya uchaguzi mpaka sasa?

Hebu jaribuni kujikita kwenye mambo ya msingi na yenye tija kwa taifa hili.
Hii nguvu mnayoitumia na kupotea bure mngetumia kutafuta majawabu ya matatizo yanayotukabili kama taifa, naamini tungekuwa na uchumi imara na maisha bora kama MAREKANI!

Dr Slaa sio mgeni wa siasa za taifa hili, hajaibuka jana yupo tangu miaka ya 90....Huko kote mlikuwa wapi sio unafiki na UMA.L.A.YA wa kisiasa huu?
Hebu tuache kujitoa nguo hadharani ndugu zangu.....Kwa hali hii tunawakosea wazazi wetu waliotulea kwa staha, heshima na uadilifu, tunawakosea hata walimu wetu waliotufudisha,tunaudhihirishia umma wa watanzania kuwa tulihudhulia shule na vyuo lakini HATUJAELIMIKA.
Tunadhalilisha hata vijana wenzetu ili mwaisho wasiku jamii ituone kuwa tu wapuuzi, hatufai kukabidhiwa dhamana za kuongoza!
 
siamini kama mjinga wa level hii pia alikuwa memba wa CHADEMA. CHADEMA is where geniuses belongs, sijui huyu mjinga alipenya vipi?

Even geniuses ask questions-tupac shakur. so usinishangae kuuliza huyu menye utindio wa ubongo aliingiaje CHADEMA.
 
Aanze kutuambia baba halisi wa mwenyekiti wake.....

:A S-heart-2:Yeye Mwampamba ndiye mama yake na DR Slaa sasa kamleta aliyempa mimba na kumzaa huyo Dr Slaa mbona patamu hapo? Siku zote anayejua baba wa mtoto ni mama hivyo ametoa ushahidi nani anabisha?:blah:
 
Back
Top Bottom