Mtela Mwampamba afunguka ndani ya Passion FM

Mtela Mwampamba afunguka ndani ya Passion FM

Taswira

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2012
Posts
1,198
Reaction score
452
Wakuu kama upo karibu na Redio tune passion fm muda huu(Saa mbili asubuhi) Mtela Mwampamba anafanya mahojiano kuhusu siasa zake,
Nimesikia kwa masikio yangu,Mtela mwampamba akidai anamjua baba mzazi wa Dr.slaa na familia yake halali ilipo.Mtangazaji alipo mhoji kuhusu kwani Dr.Wilbroad peter slaa sio jina lake,Mwampamba akajibu sio jina lake.Dr.slaa anatumia jina la mzee mmoja maarufua karatu anaitwa peter Slaa,Yeye Dr.slaa anababa yake na anajina lake halali la familia yake.Hili za mzee peter slaa alipewa kulinda heshima fla" Jamani Heshima gani hiyo???

Katika hali ya kushangaa Mtangazaji akamuomba mwampamba atoe ushahidi wowote kuhusu mzee peter slaa,Duh mwampamba akampatia picha inayoonesha Mzee peter slaa ambaye si baba mzazi wa Dr.W.peter slaa.

Kupitia wall ya Mtela mwampamba(facebooka) asubuhi ya leo ameweka picha ya mzee peter slaa na Dr.slaa hii hapa

Mtela Mwampamba


Asubuhi hii nipo live kwenye mahojiano "PASSION FM" muda huu,Moja ya mambo nitakayozungumzia ni Kumtaka katibu mkuu wa Chadema(DR.SLAA) ajitokeze hadharani aseme familia yake ipo wapi,Ubini wake ninani na kwanini anatumia jina la Peter Slaa wakati sio baba yake.
Huyu Mzee pichani ndiye Mzee Peter Slaa ambaye sio baba wa Dr.Slaa.Namuomba Dr.slaa aitafute familia yake na awambie watanzania jina lake halisi na sio hili analotumia sasa la huyu Mzee peter Slaa ambaye sio baba yake na hawana uhusiano.

ONYO😛ropaganda zozote dhidi ya Katibu wangu wa Uenezi(NAPE NAUYE) za kumtaka aongelee mambo ya familia yake,Naomba DR.slaa ajitokeze kwanza aseme jina lake halali na familia yake ilipo.
Nimjua Dr.slaa hawezi kukwepa hapa,Heshima yake nimemtunzia sana sasa ni wakati wake wa kujitokeza kwa watanzania aseme jina lake halali na ubini wake na familia yake ilipo.
Mengi zaidi Tune passion Fm muda huu"

uu








 
Ya kadi ya CCM wameshindwa, unadhani Dr atajadili mambo kama haya aisee wakupamba maharusi, mshauri Nape aje hapa atuambie CCM na serikali yake wana mpango gani na matokeo ya form 4
 
Huyu masalia ni mtu wa kumpuuza tu.

Hivi huko magambani (CCM) hakuna issues za kuziongelea?! Mbona watanzania kuna mambo mengi (hasa matatizo) zaidi yanayotukabili: kwa sasa tuna hii issue ya zaidi ya 93% ya vijana wetu wamefeli kidato cha nne, huduma mbovu za afya etc. Mimi nilifikiria vijana kama mwamapamba na mwezie shonzi wangekuwa mstaari wa mbele kujadili issues muhimu zinazogusa watanzania na sio kila siku Dr. Slaa. Inavyoonekana wanatumiwa tu kama Condom au toilet paper.
 
Mbona sijaona tija ya huu uzi...kwamba uchangiwe au? Ni chizi tu ambaye atachangia uzi huu, TOPIC CLOSED
 
mdomo nao ni mtaji ati ,hata usipokuwa na elimu!!!hukumbuki ile post unaambiwa mjini hufi na njaa ?????????
 
Ni upuuzi wa muda mfupi tuu.utapita na watatulia kama alivyotulia tambwe hizza,walid kaborou na wengine.
 
Ujinga umejaa hadi unamwagika chini..... izo ndo siasa za sisiemu... Baba yake slaa anahusianaje na 60% ya div.0?
 
Dr siyo mtu wa kuja eti kujadili upuuzi kama huu!Mwambamba ni sawa na kuku aliyekatwa shingo!Nenda kamuulize Kikwete kwa nini Tanzania ni maskini.
 
Kwa hiyo Nape amekosa majibu ya swali alilowekewa mezani na Kagaila na sasa kaamua kujibu kwa staili hii!!??
mbona alivyotaka elimu ya Mh. Mnyika alitoa majibu sahihi na yeye si angefanya hivyo badala ya kutafutia wajinga wengine balaa!
 
Huu ndiyo upuuzi utakaiangamiza CCM. Hili litaisaidia nini CCM? Kama ni kupoteza dira ndo huku.
 
Unaongea nusu nusu sema baba yake ni flan anakaa wapi etc;; sio tu unamjua then inahusiana nn ni ukatibu wa chama?so kama yatma je hana haki au?ongea sera za magamba sio UMBEYa umeshindwa sana kamuombe mzee YUSUPH akutoe Taarabu inaonekana unakpaj cha majungu.UMesoma kwel Mwampambo?????hahaaaaa hongera kaka kwa kaz
 
kwa hiyo mtela mwampamba ndiye mama yake na dr. slaa hadi atueleze eti ninaujua ukweli wote,pooor and kwishney
 
Mtela!Na ww nikikuomba nenda kamuulize Mama kama ni mtoto wa Mzee Mwampamba nitakuwa nakosea au!Mwanangu kapata F masomo yote 10 chini ya utawala huu unao ulamba miguu sasa!
 
Huyu chalii ana mtindio wa ubongo. Mzazi De Slaa anatuhusu nini? Yaani ukishaitwa gamba lazima uwe taahira. Hebu tuongee siasa na sio huu upuuzi wa mchiriku.
 
Pamoja na kuwa mapandikizi, mimi nashindwa kuelewa kwa akili kama hizi walifanikiwaje hata kupata hizo nafasi walizokuwa nazo CDM. This is seriously pathetic .................. hata mtoto mwenye akili wa standard 5 hawezi kufanya haya!! Halafu kesho utamuona yuko na Nape!! Eti onyo kuhusu kuzungumzia familia ya Nape ............... si ataueleze anayoyajua kwa hiyo akili yake fupi!!!
 
Back
Top Bottom