Ivi unaweza kulinganisha context ya lusinde (kwenye jukwaa la kisiasa)wakati wa kampeni na Katibu mkuu wa chama alipoulizwa akadefend na mawazo ya Mtei (sio kiongozi wa chama) tena akiwa nyumbani kwake??
:focus:
Ivi kawa wewe Ritz ni mrefu nikasema wewe ni mrefu natakiwa kuomba radhi sio?? Hebu geuzia upande wa pili wangekuwa ni kina john wamezidi kwenye hiyo tume si kila ijumaa kungekuwa na maandamano?? Humu si kungekuwa hakutoshi? Shukuruni mungu huu upande wa pili kuna ustaarabu na hata mteuzi najua ameliona hilo.
Ingawa waleta thread wote wametunyima nukuu sahii ya alichokisema Mzee Mtei ili tuweze kupima context (muktadha) wa kile ambacho mzee alikikusudia kama kila chembechembe ya udini wa la hasha. Lakini kusema Zanzibar inawakilishwa na Waislamu tu kuna ubaya gani kama sio kuwa Watanzania tunataka kukuza kitu. Call a spade a spade. Ukweli unabaki palepale kuwa kati ya wajumbe wote 15 toka Zanzibar hakuna Mkristo. Huo ndio ukweli kama Wakristo wenye vigezo vya kuingia kwenye committee hawapo tumwachie aliyewateua aseme kwenye muktadha wa mzee Mtei. Wachangiaji wote pamoja na mimi hapa kwa bahati mbaya tunaangalia form of what mzee said and we are falling short of the context. Tunatakiwa tuzame kwenye context ya mzee Mtei halafu ndio tutoe mawazo ambayo contractive kewa ajili ya ustawi wa Taifa letu.
Je, tukikuta mzee alikuwa na nia nzuri tena yenye faida ya dini zote mbili tutafanyaje? Maana hizi ndio dini zenye wafuasi wengi hapa Tanzania na duniani kwa ujumla. Ni kutaka kuishi kwenye falsafa ya ngamia kuficha kichwa na hali kiwiliwili kiko nje tukifikiri kunaweza kuwa na amani bila watu wa dini hizi kukaa pamoja kwa maelewano. N amuafaka wowote ule lazima uzingati equity kwenye representation ya population ya dini hizi. Watanzania wenzangu tena wana great thinkers nafikiri mzee Mtei kuna watu wako karibu naye ebu tumwombe aeleze muktadha a kile alichokusudia. Siamini sana kuwa mzee mwenye busara na akili kama Mtei anaweza sema kitu hali mradi.
Na swala kuangalia uwakilishi wa dini lipo nchi msikatae. Mfano ambao bado upo katika kumbukumbu zetu ni pale Waziri Mkuu mstaafu-Sumaye alipounda board of parole. Ilionekana ilikuwa na Wakristu wengi. Waislamu wali raise alarm na Rais wakati huo Mkapa akaliona na akavunja ile board ya awali na kuiunda upya. Kama Wakritiu nao wanaona hakuna equal represenatation kwenye hii tume walalamike ili uwakilishi uangaliwe upya. Kunungunikia chini kwa chini sio vizuri.
Nawakilisha