MTEGO wa DR.ULIMBOKA uko tayari...

MTEGO wa DR.ULIMBOKA uko tayari...

Mbona humu JF tunayaongea hayo mambo ya mahakamani? Kwani yeye lazima aongee na waandishi wa habari!! Anaweza tu kuandika waraka kupitia humu JF tu kwani waandishi wengi wa habari Bongo news zao huwa wanalamba humu humu JF. Waandishi wataogopa kuandika lakini watasema habari zaidi ziko kwenye JF, bring more traffic to JF....how about that.
 
my Nionavyo! Sirikali imeshukuru kutokea ajali ya meli ya Skagit, kwani raia sasa akili/mazungumzo kwa ajali. Ilitokea kipindi cha mjadala wa Richmond na tukio la babu wa Loliondo
 
Serikali ya ccm pamoja na jeshi la polisi wakiongozwa na kova mmelaaniwa duniani na mbinguni kwa matendo yenu mnayo tufanyia watanzania ,hamna hata aibu mwogopeni mungu
 
Serikali imeshakamilisha mtego wa kumzima kabisa Dr.Ulimboka. Mtego huo umeratibiwa na Usalama wa Taifa na Polisi kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Eliezer Feleshi. Mtego huo ni upi? Ni hivi:kuna 'Jambazi' la kikenya lililofikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumteka na kumtesa Dr.Ulimboka. Kesi iko Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Sasa,kuna taarifa kuwa Dr.Ulimboka anaendelea kupata nafuu na ameshaanza kufanya mazoezi mepesi. Ni habari ya kutia moyo. Lakini,Dr.Ulimboka atakaporudi nchini,atatamani akutane na Waandishi wa Habari na kuzungumzia sakata lake. Hilo hatafanikiwa kulifanya.Na akilifanya atashtakiwa kwa kuidharau Mahakama. Kivipi?

Serikali kupitia Jeshi la Polisi litamuwahi kwa kumwambia kuwa suala analotaka kulizungumzia liko Mahakamani. Dalili za kusimamia mtego huo zimeshaanza kuonekana Bungeni.Ni juzi tu Bajeti ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ya Mambo ya Ndani ilizuiwa(baadhi ya kurasa zake) kwa kisingizio hichohicho. Swali litakalobaki ni je,mambo hayo ndio yataishia kwa 'Jambazi' la Kikenya?

Kwani, si anaweza kufanya press conference RSA. akaita mpaka TBC, ili waumie zaidi.
 
Sasa mbona hakuna siri tena. Atafanya mazungumzo na wana jf hata wakileta mizengwe.
 
Inamaana Kubenea yeye hakuliona ilo swala kama lipo mahakamani?mbona mwanahalisi ya jana imeanika kila kitu.
 
Back
Top Bottom